Kwanini Walimu wengi ni maskini hapa Tanzania?

Kwanini Walimu wengi ni maskini hapa Tanzania?

Narudia tena. Hatuwezi kudharau taaluma ya ualimu tutegemee muujiza.

The best brains waende ualimu. Lakini lazima wawe the best paid civil servants.

Walipwe zaidi ya madaktari, wahasibu, wahandisi nk. Mazingira yao ya kazi yawe the best! Ifike mahali kila mfanyakazi atamani kuwa mwalimu lakini wachukuliwe walio bora tu.
 
Mimi sio mwalimu ila nadhani zifuatazo zinaweza kua ni sababu kwa kiasi kikubwa;-
  1. Mishahara midogo. Kada ya ualimu ni miongoni mwa kada zenye mshahara midogo ukilinganisha na kada nyingine. Nakumbuka mwalimu mwenye shahada gross salary yake ni 730,000 sasa hii ikikatwa inabaki almost 400,000k. Gharama za maisha yani nyumba, nauli, usafiri, ada za watoto, umeme, chakula, n.k inakua ni shida.
  2. Kukosekana kwa posho. Katika maofisi mengi kumekuwepo na posho mbali mbali na watumishi wengi wananufaika sana na hizi posho. Mojawapo kubwa kabisa ni posho ya kazi za ziada. Yani ukifanya kazi kuzidi masaa yanayokubaliwa kiutumishi unakua subject to compensation. Ila sasa huko kwa walimu hakuna posho ya over time, hakuna house allowance, hakuna transport allowance etc. Kukosekana kwa hizi posho kunafanya walimu waishi mshahara to mshahara. Na kwakua mshahara ni mdogo, wanajikuta katika ukata
  3. Kukosekana kwa safari. Kwenye maofisi mengi kuna vijisafari safari vya hapa na pale vya training, workshops, seminars, technical commitees na kadhalika. Safari katika kada ya ualimu ni chache sana na unakuta wanachaguana mkuu wa shule au makamu wake au academic officers. Ndani ya miaka mitatu possibility ya mwalimu kusafiri na kulipwa per diem ni ndogo sana na safari yenyewe utakuta ni ya muda mfupi haizidi wiki.
  4. Kukosekana mianya ya kupiga dili. Walimu wateja wao ni wanafunzi. Hakuna dili yoyote hapo. Kwanza elimu ya siku hizi ni bure. Hakuna motisha wala hakuna mzazi atakupa laki mbili kama zawadi kwa kumfundisha mwanae vizuri. Kuna watu huko bandarini wana mijengo Mbweni kwa hizi dili ndogo ndogo za hapa na pale.
  5. Kutochangamka. Walimu wengi hua hawako sharp kwenye harakati nyingine za kimaisha ukiachana na kazi. Wengi wanakua busy kukimbizana na wanafunzi unakuta mtu yuko job had saa kumi na moja jioni anawapa wanafunzi wachelewaji adhabu wakati huo hana hata genge la kuuza nyanya pale home au wanafunzi watano wa kupiga pindi after work.





Nimechokoza mada
Hapo Kwa no 4. ni sahihi kabisaa...Kwani walimu most of the time wanatumia Muda wa ziada kama huo kuangalia discipline za wanafunzi
 
Mimi ni mwalimu hali yangu ya uchumi sio nzuri sana kulinganisha na watu w kada nyingine, tatizo lipo wapi maana hata walimu wenzangu hali zao sio nzuri, tunakosea wapi walimu
Tatizo siyo uwalimu. Tatizo ni mind set
Chukulia mwalimu yupo masasi vijini akiamua kujihusisha na biashara na kilimo cha korosho ndani ya miaka 20 atakuwa masikini?
Mwalimu aliyepo mufind akiamua kupanda miti ndani ya miaka 30 ya utumishi atakuwa masikini?
Issue ni kwamba watumisi wengi wa umma wanategemea wizi kama chanzo mbadala cha mapato! Which is wrong
Unajilinganisha na wezi na wala rushwa utahangaika sana. Hata TRA kuna masikini
 
Unazu
usidharau kazi za watu aise
Kwa taarifa yako walimu na wenyewe wanajenga nyumba za kuishi kama wewe na wengine wana usafiri
sio kila mwalimu anategemea mshahara wa ualimu yapo mambo mengi ya kufanya ambapo hata wewe unayewakejeli huwezi fanya.
Kuna mama mmoja hapa mchaga jina namuhifadhi ni mwalimu wa primary lakini ni agent wa kuuza bia na soda sehemu tulipo ana ukwasi wa kutosha kuliko hizo njugu zako unazohesabia mfukoni.
Nilishawahi muuliza kwanini haachi ualimu akanijibu ni kazi iliyompa huo utajiri maana alianza kuuza visheti shuleni kwa wanafunzi anaiheshimu sana hiyo kazi zaidi ya yote inampa security na pia inampa contacts na wakubwa wa serikalini maana afisa elimu wa wilaya,mkoa waziri wa elimu,RPC wote ni rafiki zake unaona wewe mtoa mada?
Una comment ukiwa shule gani mkuu
 
Back
Top Bottom