Kwanini Walimu wengi ni maskini hapa Tanzania?

Kwanini Walimu wengi ni maskini hapa Tanzania?

Walimu hatutaki kuboreshewa maslahi yetu kwa kupunguzwa kipato cha watu wengine, kila mtu ale keki ya taifa kwa jasho lake, kama lililopo si tunalostahili, basi liongezwe, sio waumie wengine ili kutunufaisha sisi. Huo ni uhuni.
 
Umasikini ni jambo la kujitakia kwa wengi wao. Ardhi tele, watu tele, fedha za mkopo zipo.
 
Mimi ni mwalimu hali yangu ya uchumi sio nzuri sana kulinganisha na watu w kada nyingine, tatizo lipo wapi maana hata walimu wenzangu hali zao sio nzuri, tunakosea wapi walimu
Utakuwa na element za ualimu wew ndi maana unauliza hivo, sasa nawew jibu swali hili, kwanin wakulima wengi wa tanzania ni maskini?
 
Kwa ujumla Watanzania wote ni masikini tu. Wakulima, wafugaji, waajiriwa, wafanyabiashara ndogo ndogo (wamachinga) , wanasiasa nk
 
Hapo kwny kuchamgamka ndo penyewe
Mimi huko nyuma nilikuwa sekta ya maliasili huko vijijini na mshahara Karibu Sawa na walimu... Jamaa zangu wakanifundisha kujiongeza kwenye shughuli mbadala but issue ikawa mtaji. Tukaamua kuchukua mkopo na mwalimu mmoja niliyemkuta hapo. Sote tukachukua mkopo wa milioni tano but kwenye matumuzi mimi nikaamua kukodi shamba na kulima mpunga na pesa ingine nikaongezea kununua gunia za mpunga maana wakati wa mavuno huwa ni elfu 30 gunia. Mwenzangu licha ya kuongea vizuri mwanzoni akaamua kununua bodaboda ili aweze kwenda shuleni na kurudi home kwake kwa urahisi. Kumbuka hapo Kijijini ilipo shule anayofundisha, ambapo ndipo nilipomkuta na kwenye Kilimo kizuri na nyumba bei poa za kupanga, yeye akawa hapataki anataka akapange kwenye Makao makuu ya kata ambapo ni 15 km one way. Mwisho wa siku alishindwa hata kuhudumia pikipiki mpaka ikafa na mkopo hajamaliza. Sisi wenzie tuliendelea na Kilimo na kununua mazao kitu ambacho kilitufanya tusiyumbe na ule mkopo. Ndani ya miaka mitatu tuu sisi tuliweza kununua pikipiki kwa pesa cash na bodaboda wangu akawa ndiye anampeleka yule mwalimu shuleni maana muda mwingi pikipiki yake ya mkopo ilikuwa mbovu.
 
Mimi sio mwalimu ila nadhani zifuatazo zinaweza kua ni sababu kwa kiasi kikubwa;-
  1. Mishahara midogo. Kada ya ualimu ni miongoni mwa kada zenye mshahara midogo ukilinganisha na kada nyingine. Nakumbuka mwalimu mwenye shahada gross salary yake ni 730,000 sasa hii ikikatwa inabaki almost 400,000k. Gharama za maisha yani nyumba, nauli, usafiri, ada za watoto, umeme, chakula, n.k inakua ni shida.
  2. Kukosekana kwa posho. Katika maofisi mengi kumekuwepo na posho mbali mbali na watumishi wengi wananufaika sana na hizi posho. Mojawapo kubwa kabisa ni posho ya kazi za ziada. Yani ukifanya kazi kuzidi masaa yanayokubaliwa kiutumishi unakua subject to compensation. Ila sasa huko kwa walimu hakuna posho ya over time, hakuna house allowance, hakuna transport allowance etc. Kukosekana kwa hizi posho kunafanya walimu waishi mshahara to mshahara. Na kwakua mshahara ni mdogo, wanajikuta katika ukata
  3. Kukosekana kwa safari. Kwenye maofisi mengi kuna vijisafari safari vya hapa na pale vya training, workshops, seminars, technical commitees na kadhalika. Safari katika kada ya ualimu ni chache sana na unakuta wanachaguana mkuu wa shule au makamu wake au academic officers. Ndani ya miaka mitatu possibility ya mwalimu kusafiri na kulipwa per diem ni ndogo sana na safari yenyewe utakuta ni ya muda mfupi haizidi wiki.
  4. Kukosekana mianya ya kupiga dili. Walimu wateja wao ni wanafunzi. Hakuna dili yoyote hapo. Kwanza elimu ya siku hizi ni bure. Hakuna motisha wala hakuna mzazi atakupa laki mbili kama zawadi kwa kumfundisha mwanae vizuri. Kuna watu huko bandarini wana mijengo Mbweni kwa hizi dili ndogo ndogo za hapa na pale.
  5. Kutochangamka. Walimu wengi hua hawako sharp kwenye harakati nyingine za kimaisha ukiachana na kazi. Wengi wanakua busy kukimbizana na wanafunzi unakuta mtu yuko job had saa kumi na moja jioni anawapa wanafunzi wachelewaji adhabu wakati huo hana hata genge la kuuza nyanya pale home au wanafunzi watano wa kupiga pindi after work.

Nimechokoza mada
You said it all [emoji457][emoji375]
 
Jamaa ni wajinga sana.
Mimi mlinzi wa taasisi moja hivi ya serikali. Posho ya headmaster ambayo ni laki 2 Mimi napewa hiyo kama nauli.
Bado posho zingine , badala ya kudai haki zao wao wanajiona sehemu ya serikali
[emoji16][emoji16]
 
Tumewahi kuwa na Ma Rais wawili walimu, waziri mkuu mwalimu...
Marais wawili ... waziri wakuu wawili ... out of how many walimu's ? Umeshawahi kusoma kitu inaitwa statistics?

Kuna walimu wengi mno mno mno wansota kinoma noma af we unasema mambo ya marais wawili kuwa walimu
 
Kwa ujumla umaskini kwa yeyote awe mwalimu au mwajiriwa mwingine ni kujitakia. Wengi HATUPAMBANI IPASAVYO!
Yaani matajiri wako BIZE kuzidi maskini, hiki kitu Huwa sielewi.
Hadi ule mtazamo kuwa maji hutiririka kutoka nchi kavu kufuata yaliko maji mengi baharini, ziwani, bwawani umepata umaarufu.
 
Unazungumzia wale wa UPE bila shaka au unataka wawe na ukwasi kama Bakhresa.

Sijawahi kusikia kuna mwalimu mnufaika wa TASAF.
 
Vijijini kuna fursa nyingi sana kwa Mwalimu kuzitumia na kuondokana na umasikini. Kilimo, kukusanya mazao, kufuga nyuki, kutengeneza matofali na vigae vya kuchoma, kutengeneza sabuni, kununua mjini bidhaa za mahitaji ya kila siku kwa jumla mjini na kuzisambaza kwenye viduka vya vijijini hapa uhitaji kuwa na duka, kukusanya mifugo.
Muhimu ni kutenga mda wa serikali na mda binafsi.
 
Hakuna mshahara uliwahi kuwa mkubwa hata siku moja, mm ni mwalimu japo sio wa shule na maisha yangu japo sio ya shida lakini pia sio ya raha saaana.
Nina drive ninaishi kwangu nina nyumba za wapangaji. Sina biashara naishi kwa mshahara
Maisha inkujipanga tu walimu wenzangu wamaejisahai sana mikopo ndo shetani mkubwa kwa walimu wanapenda kukopa sana
Kuna mwalimu alikopa 2.5mil akaenda kununua simu ya laki saba pia akaenda kulewa ie ovyoovyo akiw na birungutu lote mfukoni, bila kusahau malaya, kesho yake asubuhi akakodi boda imrudish home maana alikuwa anafundisha vijijini akagundua simu imedondoka, akamwambia boda geuzaaaaaa akaenda kununua ingine mpya ya laki 7 , pombe zimekuja kumtoka amebakiwa na less than a million. Na mkopo ulikuwa ni topup wanakata karibu laki3 kwa miaka 5
 
Mimi sio mwalimu ila nadhani zifuatazo zinaweza kua ni sababu kwa kiasi kikubwa;-
  1. Mishahara midogo. Kada ya ualimu ni miongoni mwa kada zenye mshahara midogo ukilinganisha na kada nyingine. Nakumbuka mwalimu mwenye shahada gross salary yake ni 730,000 sasa hii ikikatwa inabaki almost 400,000k. Gharama za maisha yani nyumba, nauli, usafiri, ada za watoto, umeme, chakula, n.k inakua ni shida.
  2. Kukosekana kwa posho. Katika maofisi mengi kumekuwepo na posho mbali mbali na watumishi wengi wananufaika sana na hizi posho. Mojawapo kubwa kabisa ni posho ya kazi za ziada. Yani ukifanya kazi kuzidi masaa yanayokubaliwa kiutumishi unakua subject to compensation. Ila sasa huko kwa walimu hakuna posho ya over time, hakuna house allowance, hakuna transport allowance etc. Kukosekana kwa hizi posho kunafanya walimu waishi mshahara to mshahara. Na kwakua mshahara ni mdogo, wanajikuta katika ukata
  3. Kukosekana kwa safari. Kwenye maofisi mengi kuna vijisafari safari vya hapa na pale vya training, workshops, seminars, technical commitees na kadhalika. Safari katika kada ya ualimu ni chache sana na unakuta wanachaguana mkuu wa shule au makamu wake au academic officers. Ndani ya miaka mitatu possibility ya mwalimu kusafiri na kulipwa per diem ni ndogo sana na safari yenyewe utakuta ni ya muda mfupi haizidi wiki.
  4. Kukosekana mianya ya kupiga dili. Walimu wateja wao ni wanafunzi. Hakuna dili yoyote hapo. Kwanza elimu ya siku hizi ni bure. Hakuna motisha wala hakuna mzazi atakupa laki mbili kama zawadi kwa kumfundisha mwanae vizuri. Kuna watu huko bandarini wana mijengo Mbweni kwa hizi dili ndogo ndogo za hapa na pale.
  5. Kutochangamka. Walimu wengi hua hawako sharp kwenye harakati nyingine za kimaisha ukiachana na kazi. Wengi wanakua busy kukimbizana na wanafunzi unakuta mtu yuko job had saa kumi na moja jioni anawapa wanafunzi wachelewaji adhabu wakati huo hana hata genge la kuuza nyanya pale home au wanafunzi watano wa kupiga pindi after work.

Nimechokoza mada
Nimependa majibu hayo yameahiba.
 
Back
Top Bottom