1. Maskini hana urithi wa mali
2. Maskini hana wazazi wenye connections kwasababu watu wengi wanaojuana huwa katika level moja ya uchumi, mara nyingi matajiri circle zao ni za matajiri na wazazi wake wakiwa maskini, basi circle zao zimejaa maskini wenzao
Suluhisho.
1. Atengeneze connections zake kwa jasho lake yeye mwenyewe
2. apambane kwa bidii awe juu sana kwenye kitu anachofanya, kama ni shuleni basi afaulu mpaka vyuo vinambakiza awe lecturer, kama ni biashara inabidi ajibane kweli kweli ili mtaji uongezeke, n.k
3. atumie kipaji chake, hapa wenye vipaji wengi (sio wote) wanatokeaga maisha magumu kuanzia kina pele, maradona, messi, ronaldonho, michael jackson, n.k. tumia ulichojaaliwa kikunufaishe.
Vitu ambavyo havina msaada:
Tamaa - hapa atageuka kuwa kibaka anaweza kuishia kuchomwa moto, anaweza kuwa malaya akaishia kufubazwa kwa magonjwa na kujishusha utu.
Kulalamika kuzaliwa maskini - kuzaliwa maskini si uamuzi wako lakini kufa maskini kwa kiasi kikubwa ni uamuzi wako, kama nguvu unazo, akili unazo, n.k pambana mpaka kieleweke, hapa nikianza kuweka listi ya matajiri waliokuwa maskini tutakesha maana hata Mengi (r.i.p) alizaliwa familia ya kimaskini.
kuendekeza kauli za kimaskini - tumevikuta na tutaviacha, kulikuwa na matajiri flani ila leo wako wapi, cha muhimu kupumua, n.k achana na taka taka hizi aisee, umevukuta na utaviacha lakini hakikisha na wewe vikupitie hata kwa mbali, ukiendekeza hizi kauli za kijinga utateseka sana.
Kutafuta connection kwa kujishusha utu wako - tafuta connections bila kuondoa utu wako, kuwa chawa inapobidi kwa mbali lakini usiwe kupe ambae hata unapoona kabisa watu wanakuvumilia uwepo wako wewe unang'ang'ania, yani unalazimisha sana ukaribu lakini watu unaona kabisa wanakuvumilia tu kinafki wanatamani uondoke na hawana muda na wewe, mfano mzuri hapa nahisi pana Steve Nyerere, yani huyu hata kwa mwaka huu kuna semina ilikuwa ya viongozi wa kike pale Dodoma, jamaa alienda aisee, Pia huko kwa viongozi wengine analazimisha sana connection anabaki kituko tu maana washamkariri yupo kwa maslahi yake tu, matokeo yake hata michongo ama teuzi hapati kwa tabia hizi.
Wivu na chuki kwa wenye navyo - Wivu hautakusaidia chochote zaidi ya kukuumiza tu na mwishowe kuwa mshirikina tu na ushirikina haunaga maendeleo, wivu wako na chuki kwa waliofanikiwa utakuumiza sana hii dunia, kutwa nzima utawaombea mabaya wenzako na utazidi kuumia wanavyozidi kutoboa.
kuwekeza muda mwingi kwenye anasa - Sio tatizo ukiwa na ratiba maalum lakini ni tatizo ukizidisha,,,,iwe ni pombe, ngono, sigara, bangi, n.k hivi vitu vitakufanya usahau kabisa malengo yako huku afya yako ikizidi kuzorota.