Kwanini waliozaliwa katika familia maskini wana nafasi kubwa na wao kuwa maskini kuliko waliozaliwa katika familia tajiri?

Wazazi maskini ushauri wao kwa watoto ni kuhusu umaskini tu, mfano utawasikia Wakinga wanaroga ndomaana wanafanikiwa au Wachaga wezi ndomaana wanafanikiwa.
Mzazi anawaambia watoto mambo ya kufikirika.
Mimi ni Mkinga najua maskini wengi hawajitumi na sio wabunifu wao wanafikiri waliofanikiwa ni Freemason au wametoa kafara. Bahati mbaya wazazi maskini huwakaririsha ujinga huu watoto wao.
 
Umasikin mbegu
 
Utajiri wa kweli ni ule unaorithishwa kizazi hadi kizazi.
 
Mazingira yanaweza kuwa shida sana.Tatizo waafrika wengi hatuamini tena katika uendelevu wa familia na mali.Tuna amini sana katika ku survive (Ajira) badala ya kuchukua hatua endelevu za kuondokana na umasikini wa familia na ukoo.
 
Like a father, like a son. Viscous circle of poverty.
 
.. kutwa nzima unawaombea mabaya.....sentesi hii unaweza iita executive summary ya andiko lako. Muda mwingi badala ya kupanga mambo yako, unautumia kulalamika na kuwaombea watu wengine mabaya.
 
hakika ndugu! .yaani tunatumia muda mwingi kulalamika kuliko kuchukua hatua
Na hata viongozi pamoja na ukwasi walio nao, akili ni za kimaskini. Wanatumiwa muda mwingi kuelezwa matatizo badala ya njia za kutatua.
 
Utajiri ulithishwa vizazi na vizazi. Wale wanaotokea kwenye familia zilizo na mali huwa na kazi ndogo ya kuendeleza. Vivyo hivyo umasikini nao urithishwa vizazi na vizazi maana watoto hukosa pa kuanzia. Kule kwetu kuna msemo wa kihenga kuwa mwenye kuwa na mali huanzia kwa baba yake.

Taikuni wa fasihi alileta uzi humu juu ya umuhimu wa kurithisha vizazi vyetu mali Ila kuna watu walimpuuza Ila ni ukweli japo ni mchungu. Agano la kale tunasmbiwa Isaka alivifukua upya visima vya baba yake vilivyofukiwa na maadui zake. Hatuambiwi alichimba. Hiyo ni one step ahead dhidi ya yule ambaye baba hakuacha hata shimo. Ni wachache sana wanaokuwa matajiri wakitokea from the scratch nao ni kwa mateso makubwa sana.
 
Nakubaliana na wewe kabisa. Mimi nina ndugu yangu yaani yeye muda wote analalamikia maisha awe na familia au mtu baki. Mfano ukimpigia simu ukamuuliza tu umeamkaje leo, weee ataanzia hapo, unadhani kuna kulala basi, yaani maskini anatoa wapi usingizi, ohh ukiwa maskini unajikuta tu ni asubuhi, ohh matajiri ndio wanalala sisi wengine tulala mbinguni ohhh hiki mara kile yaani mi mama maskini hivi au vile duh yaani utajuta kusalimia😂 yaani shida tupu. Wakati na wewe una pambana mbio mbio ye kulalamika na kuukumbatia umasikini wake.

Anaamini kwenye ushirikina haswaa, au mara yule mwanamke ana mikosi ndio maana maisha yangu hayaeleweki (mke) ohh mara nilikuwa na mwanamke huyu kidogo nilishika hata elfu 10,
(mchepuko) 😂😂😂😂 mara anapata kazi anafanya hela haoni hapo ujue anaona kalogwa😭 au mara anapata kazi sehemu wanakubaliana kimtindo tu siku akija anakuta mtu mwingine anafanya malalamiko kama kawaida yaani ni shida.

Akikitumia msg hata 10 zote analalamikia umasikini tu wake etc. yaani tunasaidiana hivyo hivyo maisha yanakwenda maana hata umshauri wala haelewi kitu. Yaani analalamikia shida zake kuliko kutafuta solution. Sasa mtu wa hivi unamsaidiaje wakuu?
 
Investing behaviour ndo zinatutofautisha huko mbele,what to invest in and how much to risk.
 
Hahaha aisee yaani bado tuna safari ndefu sana. Watu wa hivyo mara zote tunawaacha tu maana ataanza kukusimulia hapo atakwambia nilifuga kuku wakafa wote (wananiloga) nilifanya biashara fulani nayo ikafa . Hana muda wa kutafakari kwanini biashara ilikufa huenda ilikufa kwa uzembe wake tu. Mtu wa hivyo anakwambia mi nimejaribu kila kitu lakini bado masikini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…