Kwanini wamama wa siku hizi wamepoteza utisho wa kianamke

Kwanini wamama wa siku hizi wamepoteza utisho wa kianamke

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Wamama wa miaka ya 90 kurudi nyuma walikuwa vyuma kwelikweli.

Walikuwa na uwezo wa kukuchapa na kukunyoosha kwa macho tu. Nakumbuka siku nilipotoroka nyumbani kwenda na magenge ya watoto mitaani kutembea. Bahati mbaya nikakutana naye amekaa katikati ya kundi la kinamama kuna jicho alinikata nilitoka mbio bila kupumzika hadi nyumbani nikisubiri usiku yatokanayo.

Hii ilikuwa inatukuta watoto wote mtaani, ukitoroka kwenda kudoea msosi kwa jirani macho tu yatakutoa kwenye ugali.

Leo nimeshangaa sana, dada na mtoto wake nyumbani, mtoto anamuabisha mbele za wageni, mtoto anakatwa kajicho flani kakizembe anacheka na kukapotezea.

Imekuaje wamama wa siku hizi wamepoteza utisho wa kianamke. Hawana ushawishi wa zile signal za kimaadili ambazo ilikuwa ukionyeshwa tu unakaa mguu sawa na kufuata maelekezo kabla hata uchapwa fimbo.

No hilo tu.
 
Wamama wa miaka ya 90 kurudi nyuma walikuwa vyuma kwelikweli.

Walikuwa na uwezo wa kukichapa na kukunyoosha kwa macho tu. Nakumbuka siku nilipotoroka nyumbani kwenda na magenge ya watoto mitaani kutembea. Bahati mbaya nikakutana naye amekaa katikati ya kundi la kinamama kuna jicho alinikata nilitoka mbio bila kupumzika hadi nyumbani nikisubiri usiku yatokanayo.

Hii ilikuwa inatukuta watoto wote mtaani, ukitoroka kwenda kudoea msosi kwa jirani macho tu yatakutoa kwenye ugali.

Leo nimeshangaa sana, dada na mtoto wake nyumbani, mtoto anamuabisha mbele za wageni, mtoto anakatwa kajicho flani anacheka na kukapotezea.

Wapo mpaka sasa, sema tu hao wa huko hawajielewi Kwa malezi Bora.
 
Wapo mpaka sasa, sema tu hao wa huko hawajielewi Kwa malezi Bora.
Hawa wa daslam aisee bado sana. Nimeshuhudia mama anamkata kale kajicho alafu dogo anachekacheka tu na kuendelea na usumbufu. Wakati nakumbuka enzi zile mama alikuwa na macho kama sita hivi kila jicho atakaolkuangalia tafsiri yake unaielewa na kuchukua hatua fasta.

Kula lile la onyo la mwisho, na ukiendelea kuna lile kuwa hapo hutoboi lazima leo ule fimbo tu kwa fedheha uliyomsababishia. Sijui hii kitu ya asili hawa wamama na wadada wanafeli wapi.
 
Wamama wa miaka ya 90 kurudi nyuma walikuwa vyuma kwelikweli.

Walikuwa na uwezo wa kukichapa na kukunyoosha kwa macho tu. Nakumbuka siku nilipotoroka nyumbani kwenda na magenge ya watoto mitaani kutembea. Bahati mbaya nikakutana naye amekaa katikati ya kundi la kinamama kuna jicho alinikata nilitoka mbio bila kupumzika hadi nyumbani nikisubiri usiku yatokanayo.

Hii ilikuwa inatukuta watoto wote mtaani, ukitoroka kwenda kudoea msosi kwa jirani macho tu yatakutoa kwenye ugali.

Leo nimeshangaa sana, dada na mtoto wake nyumbani, mtoto anamuabisha mbele za wageni, mtoto anakatwa kajicho flani anacheka na kukapotezea.

Imekuaje wamama wa siku hizi wamepoteza utisho wa kianamke. Hawana ushawishi wa zile signal za kimaadili ambazo ilikuwa ukionyeshwa tu unakaa mguu sawa na kufuata maelekezo kabla hata uchapwa fimbo.

No hilo tu.
Hao wake zetu hawa hawa wa miaka ya 2000 wakina zuchu ndo utegemee walee watoto kweli kweli wakati na wenyewe wanatakiwa kulelewa........neenda mlinmani city unakuta mama anaramba ice cream mtoto na msichana wakazi uko wanatembea, hapo jiulize nani anaongoza mwenzie???
 
Watu wanaiga malezi ya kizungu. Mtoto hana mipaka unategemea nini?
Ni uongo wazungu hawalei hivyo hapana mtoto wa kizungu akifika miaka 18 anajitambua vizuri tu na anajiongoza vizuri kimaisha ila mtoto wa kizaramo anafikisha mpaka miaka 30 hana muelekeo hawezi kujiongoza avuta bangi pombe nk.....hapo ni nani mwenye malezi mazuri?.........
 
Unakuta familia baba mvaa vipensi vya kubana vinaishia mapajani kwenye luks ya kipensi kaning'iniza remote ya gari wakati hana gari, mama ana vaa sendoz zina manyoya na masikio kama paka hivo hivo cover ya simu ina masikio do u expect mtoto wao Junior aogope jicho la mama? Never
 
Huku huku mjini, kwanza Katoto kamepewa jina la kizungu eti "precious" alafu ni waswahili tu wa uswazi[emoji23][emoji23]
Hivi precious manaake ni nini? Hayo majina yana uhusiano gani na malezi ya mtoto. Eti junia tonny takla nk.
 
Back
Top Bottom