Kwanini Wanachadema wanalamikia teuzi za Wakuu wa Wilaya?

Fikra duni sana kutoka kwa mtu duni. Hivi mtu kutokuwa DC, anateseka na nini? Wewe ambaye siyo DC, ina maana upo katika mateso.

Tuna watu wenye upungufu mkubwa katika fikra. Kwa uelewa wako mdogo, ina maana Mashinji, Lijuakali, Nasari, wamepewa hizo nafasi ili kuwaondolea mateso? Mateso gani?
 
Pro-Chadema walichoumia ni wale wafuasi wao wa zamani kupewa vyeo hamna lingine.
Nchi hii inaonesha kuna maskini wengi wa akili kuliko mali. Hivi uDC, nao ni cheo kikubwa sana, hata watu wamwonee wivu mtu. DC mshahara wake sh 4m, yaani milioni 4, nayo kweli ni hela ya kuweza kukubadilisha katika maisha yako? 4m, ni wastani wa kama 40m kwa mwaka, na wewe unajiona umefanikiwa sana.

Ukiwa huja chochote, 40m kwa mwaka utaona ni hela, lakini ukiipata, ndiyo utatambua kuwa si chochote. Yaani hata usitumie hata sh moja kwa mambo mengine, mshahara wako wa mwaka mzima huwezi kujenga hata nyumba ya kawaida.

Nampa pole Mashinje, kushuka kutoka sh milioni 7 mpaka milioni 4. Watu wanaenda juu, mwenzetu anaenda chini.
 
Kisu kimekata mfupa...kaaa! siasa ni sayansi....Samia kapiga jiwe la gizani limewapata jichoni lazima wabweke
 
Mimi binafsi, kwa dhamira ya moyo kabisa, siwezi hata kuufikiria uteuzi wa uDC. Ni straight answer, NO. Yaani mtu na hekima yako, na professionalism yako, ukawekwe kundi moja na watu ambao hawana ujuzi wowote zaidi ya kupiga mapambio, unprecedented disgrace!
 
Vijana wenyewe, ndiyo hao akina Mashinji? Siku hizi age limit ya ujana ni miaka mingapi?
 
Hawalalamiki bali wanashangaa inakuwaje vilaza wanateuliwa na kuacha majembe? Lengo letu wote ni maendeleo sasa unapokuwa na viongozi wasio na dira mashaka yanakuwepo. Inaelekea Mama anataka kuwa na kikosi cha kumsujudu na kukiburuza!
 
Na bado.yapo meengi sana yajayo watatofautiana raisi Samia.

Huu mradi wa kumlazimisha Samia ajitofautishe entirely na serikali ya awamu ya tano ambayo yeye alikuwa sehemu yake ni mgumu mno.

Ni wazi Rais Samia na aliyekuwa bosi wake ni binadamu wawili tofauti..leadership styles haziwezi kukosa, hiyo ni nature.
Ila sio kwa 100% kama baadhi ya watu wanataka iwe.

Fukuza pm, Mara Dc's na Rc's wote weka wako.vunja cabinet teua yako.

Fukuza kila mteule wa serikali ya Jana weka safu yako.huo sio ushauri.
Rais kafanya teuzi kadhaa.sio mbaya.akitengua wanafurahia.akiweka replacement shida.
Rais samia hawezi kufanya kazi kwa matakwa nje ya chama kilichomwajiri.hiyo ni never.hili mbona lipo obvious.
 
Tuwekee malalamiko yao hapa,huenda Yana mashiko kushindwa kufanya hivyo tutakuhesabu kama mmoja wa wawawinda teuzi uliyeangukia pua.
 

80% ya wateule ni kutoka viunga vya Manyema na mtambani
 
Mzee umerudi tena kwa ile ID yako nyingine baada ya utawala wa ''makafiri'' kuondoka? Karibu sana kwani namna Magufuli alikuwa ametubana wengi.

Hahahaha enzi zao za kula halua na tende za bure kwenye vile vibaraza vyao umerejea
 
Nani anakujua kwa hii Id fake? Yoyote anaweza kusema amepata cheo chochote, ungekuwa verified user hapo sawa.
unapingana na nyumbu wengine wanaoshinda wakizomea watu humu kwamba hawajapata uteuzi.

sijui wanajuaje!!
 
Mzee umerudi tena kwa ile ID yako nyingine baada ya utawala wa ''makafiri'' kuondoka? Karibu sana kwani namna Magufuli alikuwa ametubana wengi.
Hata dada yake faizafox alikuja hapa na kukiri kuwa jiwe hakuwa mtu kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…