Kwanini wanafunzi wa International schools wao huwa hawatolewi Darasani kwenda kushangilia watawala

Hata wa private school huwa hawatoki, nadhani hao wa sirikali tu ndio mali ya sirikali
 
Mtoto wa Mwigulu Nchemba anasema Hizo shule za kimataifa na mikutano ya siasa ya CCM huhudhuria na yeye huyo.mtoto NI kiongozi wa kitaifa wa Chipikizi CCM kitaifa

Naona huna taarifa Wengi wanashiriki na wengi NI viongozi Chipikizi na umoja WA vijana WA CCM
 
TUNAWASOMESHA BURE SO LAZIMA WAJE KUWASHANGILIA SERIKALI
 
Umeelewa kweli hoja ya mleta uzi!!???
Jitahidi uwe unarudia kusoma na kutafakari kabla ya kutoa mchango wako.
 
Ukisima shule za serikali ujue wewe ni sehemu ya serikali na Chama. Ujue wewe ni mteule kama walivyo wakuu wa wilaya, madas na wengineo hivyo unapaswa kushiriki shughuli za serikali kila utakapotakiwa.
 
Umeenda nje ya beat.
 
Hivi mtoto wa Jerry Silaa na yule mwenyekiti wa chipukizi wanasoma International pia?
 
Ukisima shule za serikali ujue wewe ni sehemu ya serikali na Chama. Ujue wewe ni mteule kama walivyo wakuu wa wilaya, madas na wengineo hivyo unapaswa kushiriki shughuli za serikali kila utakapotakiwa.
Raisi ndie mwajiri na mkuu WA ajira wa wafanyakazi wote WA serikali ndio kiongozi wa huo Muhimili uko sahihi
 
Sababu ni kwamba hizo zinamilikiwa na taasisi binafsi ila hizo zingine zinamilikiwa na serikali hivyo huwezi kumdindia bosi wako unless uko tayari kuacha kazi ndivyo serikali inavyotumia udhaifu huo kuwapelekesha walimu wa hizo shule na Wanafunzi wao.
 
Swali ni kwanini hao wanaokusanywa hawakatai? Kwanini wazazi wao hawakatai?. Yani wabongo bwana,nyie raha yenu ni watu mteseke wote
Hayo maelekezo wanapewa ma afisa elimu anachofanya afisa elimu anapgia wakuu wa shule...mkuu wa shule akiwatangazia walimu wanafurahi wanachekelea wa kike kwenda kudanga mtaani nawa kiume kwenda kunywa pombe
 
Dar es salaam international schools wako mbele Sana kushiriki shughuli za kitaifa

Mfano michezo ya halaiki ya kiwango cha kimataifa wao ndio hufanya uwanja WA taifa
Ni njia mmojawapo pia ya katangaza shule zao
IST Dar es Salaam wakienda Uwanja wa Taifa kwenye michezo siku hiyo iko kwenye kalenda yao toka January First. Hakuna masomo siku hiyo.

Hawakurupuki tu wakafuta ratiba zao kuendana na upepo wa kisuli suli cha Rais ambae hajali ratiba za watu na taasisi zao

Kama umesoma chuo nje ya nchi you know siku ya kwanza ya mwaka mwalimu anagawa schedule ya jinsi mtakavyo spend kila sekunde ya muhula mzima wa masomo, na haibadiliki hata chembe. Na shule zao za awali ni hivyo hivyo!

Ikitokea amekuja mtu muhimu na maarufu chuoni kwenu, basi watakaokwenda kumsikiliza ni wanafunzi ambao at that particular time hawana kipindi. Au, kama unataka kutega darasa kwenda kumsikiliza unaenda kivyako. Darasa litakuwepo. Hulazimishwi kwenda hata kwenye auditorium ya hapo hapo chuoni, sembuse jitu linapita mtaani huko limesimama juu ya Land Cruisers kijijini liwaswage kama mbuzi tukamsikilize! Hawawezi! What if siku ile ni siku ya mid term exam kwa darasa fulani na fulani ?????? Wataacha mitihani ?????
 
Kwasababu mbili
  1. Watoto wa hao watawala wanasoma huko kwenye hizo shule
  2. Wenye shule hawapo tayari kugharamia usafiri kwenda kushangilia upuuzi
 
Kwasababu mbili
  1. Watoto wa hao watawala wanasoma huko kwenye hizo shule
  2. Wenye shule hawapo tayari kugharamia usafiri kwenda kushangilia upuuzi
Ila CCM huwa inagharamikia usafiri some time
 
Hawa shule za walala hoi hakuna ratiba?
 
Hayo maelekezo wanapewa ma afisa elimu anachofanya afisa elimu anapgia wakuu wa shule...mkuu wa shule akiwatangazia walimu wanafurahi wanachekelea wa kike kwenda kudanga mtaani nawa kiume kwenda kunywa pombe
Hahaaa kusitisha masomo kwao ni furaha sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…