sab
sababu zipo nyingi. Ila kubwa inaonekana ni kujiamini kupita kiasi hasa baada ya kuwashinda waasi wa M23. Kumbuka lile group lililoenda mwanzo na kuwashinda m23 lote limerudishwa nyumbani na wanapokezana linaenda group lingine. Kwahiyo kuna kujisahau na kuona kazi imebaki kidogo baada ya ushindi wa m23; kuna kupoteza umakini sababu ukiona kushambuliwa na kujeruhiwa na kuuwawa kwa idadi kubwa kiasi hicho ni dhahili walishtukizwa na hawakuwa na taadhari yoyote. Pia wanaliamini jeshi la DRC na kufanya nalo joint operations je wana uhakika ndani ya jeshi la DRC hamna mamluki wa waasi wanaovujisha siri? Tatu mbona askari ya nchi nyingine zenye askari katika kikosi cha UN kama Africa kusini na Malawi hawauwawi au wanajeshi wetu hawafati weledi?