Kwanini wanajeshi wanapenda sana kukopa vitu ovyo?

Mimi Sina hamu nao kabisa nilipataga tenda ya kupaua nyumba ya hawa walinda nchi basi tukakubaliana kupaua milioni Moja na laki 5 akagoma akasema anatoa milioni nikaona sio haba kimoyo moyo nikajisemea hii napiga siku moja dawa Kuwa na mafundi wengi nikaandaa vijana wa kazi akaniuliza kazi itachukua muda Gani Nikamwambia siku mbili au tatu lkni Mimi target yangu na Ile pesa ilikuwa namaliza siku moja vifaa vyote aliandaa nilivyomwambia asubuhi mapema tukatimba panga vijana ikapigika kazi pale kufika saa kumi na unusu tumemanua wanangu wanashuka juu waende kuoga mara mwamba huyu hapa karudi ana furaha sana nikajua nimemfurahisha boss akasalimia pale akaingia ndani sisi tukawa tunamsubilia atoke atulipe mara akaniita fundi hongera kazi nzuri sana Nikamwambia Ahsante Nikamwambia kiza kinaingia mafundi wengine wanakaa mbali naomba Amana yangu niwalipe akasema sawa akaingia chumbani naona ametoka kashika mkwaju na chambi mkononi akaweka mezani ananipa laki 5 nikamuuliza vip mbona hela haijatimia ananiambia hkna mtu analipwa milioni Kwa KAZI ya siku moja hapa chagua mawili nikulambe na mkwaju au uchukue hiyo laki 5 dah nikajuta kufanya Ile kazi Kwa uharaka nikakunguta matako yangu nikasepa hao raia ni dhuluma vibaya sana

Sent from my Infinix X6816 using JamiiForums mobile app
 
Polee sana kaka mimi baada ya miezi kibao na kupelekana hadi kazini kwao leo ndo kanilipa pesa yangu
 
Aisee
 
Wa Tanzania wengi ni Mbumbumbu
Wakiwaona wanajeshi wanahisi wameona Kitu cha Maana Sana na kuanza kuwaabudu.
Ndio Maana kuna Mmoja anasema Mwanajeshi alianzisha Mazoea na Mkewe halafu akawa anajikesha
Wanadanganyana vijiweni jamaa wana maisha kisa wana aaona kwenye kirikuu second hand waanaendesha uku wamevaaa midosho

Ukiwa na akili timaru nq unajitambuq uwezi kuwa askari
 
Ukiwa wewe na simu yako ndio unajiamini hivyo? Au unadhani kuna mtu wa kukusifia hivyo TABIA YA MTU USIHUSIANISHE NA KAZI
 
Hili jibu linatosha kabisa kufunga huu mjadala
 
Aisee mi sijui niseme nn kuhusu hawa jamaa... binafsi sehemu kubwa ya maendeleo yangu nimeyapata kupitia hawa watu...nilianza kwa kumjengea mwanajeshi mmoja mwaka 2013..nikafanya kazi kwa uaminifu mkubwa sana maana jamaa alikuwa ananipa pesa ya material halafu anasepa...anakaa siku mbili au tatu anakuja kuchek anakuta kazi yake iko fresh... basi akawa ananipa Connection mpka kwa wenzake... huwezi amini sasahiv nimewajengea zaidi ya wanajeshi 31 wananiconect tu na napiga kazi kwa uaminifu..nina nyumba kwa hela za haohao jamaa...kwa mtazamo wangu nadhani miongoni mwa wafanyakazi wa serekali wenye maendeleo na hawa jamaa wamo...wana ushindani sana na kingine ukijua kuishi nao hawana tabu kabisa... mimi huwa nachacha siku zingine naomba wanikopeshe na wananipa mpka laki 3 na nalipa...aisee sijui hao uliokutana nao ni wa wapi ila mimi hawa jamaa Asante Mungu kwa kuniletea kwenye maisha yangu...japo nao ni binadamu wapo wenye mapungufu...ila ukijua kuwa sote hatujakamilika unafunika kombe mwanaharamu apite...
 
Unawazungumzia wanajeshi gani wanaoogopwa na polisi!! Kama TZ nakataa ila ninachojua hivi vyombo wanabebana ndio maana mara kadhaa nimeshuhudia wanajeshi wamekamatwa na polisi then maafisa wa jeshi wanaenda kituoni kuomba,wanawatoa lock up na kwenda nao kambini kwao kwa hatua zaidi.
 
Kaka nakaa mtaa wenye wanajeshi wengi sana mbona wengine wananilipa kwa wakati ila huyu mmoja ndo ananifanya mimi kama nyani anipi pesa yangu kwa wakati
Kama wengine wamekulipa na mmoja ndiye anakusumbua kwanini useme ni tabia yao wakati aliyekufanyia ni mmoja una shida wewe Kama sio wivu na roho mbaya basi ushawahi kufanyiwa kitendo kibaya umeamua kuwachafua
 
Mwanajeshi akukope laki tatu hivi mnatuonaje nyie
 
Sio lazima kumkopesha..
 
Nachingwea. Nilikuepo juzi tu hapo πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…