Walishiriki kuharibu uchaguzi mkuu 2020 pia wamekuwa wakikamata watu pasipo makosa kwa sababu za kisiasa siasa kulinda chama tawala kwa namna yoyote ili,ona Mbowe yupo ndani kwa sababu tu ya kudai katiba mpya ambacho siyo kipaumbele cha ccm na akapewa kesi ya ugaidi na uhujumu uchumi,hata marehemu Hamza inasemekana alidhulumiwa dhahabu kimakusudi na jeshi hilo,kwa vile sheria ni yao jamaa akaona hana kitu mbele yao basi nikiua hata askari mmoja nao wakiniua nitakuwa nimefanikiwa kufikisha ujumbe kama Mkwawa kwa Wajerumani.Hivyo Polisi wajifunze kuwa jukumu lao siyo kulinda ccm na serikali bali usalama wa raia na mali zao.
 

Hawa jamaa:

"Polisi katika hili wajitafakari sana hii siyo kawaida, sasa watafanyaje kazi ikiwa raia hawatawapa Tena ushirikiano?"

Bila damu masikioni? Mbona hata Hamza kama kijana wa nyumbani labda hata aliwaasa?
 
Your browser is not able to display this video.
 
Baada ya kuteuliwa kuwa IGP Kamanda Sirro alifanya kazi kubwa sana kutokomeza Ugaidi huko Kibiti baada ya hawa magaidi kuua askari wetu.Leo nashangaa sana baada ya Askari wanne kuua na Gaidi asiyekuwa na huruma kwenye mitandao watu badala ya kuungana na kulaani mauaji hayo bado wanatoa kauli za ajabu dhidi ya Jeshi la Polisi. Napenda kuwajulisha hawa magaidi leo wameua hao Askari lakini tusipoungana na kushirikiana kupambana nao watakuja kufanya mauaji makubwa sana. Tumeona juzi huko Kabul Afghanistan kwenye uwanja wa ndege mauaji ya raia zaidi 100 walivyouwawa na hao magaidi. IGP Sirro watanzania wengi wanajua jinsi unavyojitahidi kuwalinda watanzania na hawa wahuni wachache ama wanasiasa wasikukatishe tamaa.
Ulikuwa na haki ya kuwaonya wazazi wanaoshindwa kutoa taarifa za mienendo ya watoto wao zinapoanza kubadilika na kuwa na muelekeo wa Ugaidi.
Mungu Ibariki Tanzania Mungu Ibariki Jeshi la Polisi
 
Utakapo soma sheria ya Roho, Damu na mwili nadhani itakusaidia saaana tu na utafuta post yako, mpaka hapoo? Haya ka Google kwanza halafu nitakurudia baadaye au vp?
 
Rest In Eternal Peace "HAMZA".

Wemekusema vibaya, wamekugeuzia maneno, wamekuchafua na wamekushushia matusi ila hawaja thubutu kusema "UKWELI JUU YA UONEVU/UTAPELI/MAUWAJI YA RAIA/MAUWAJI YA WAANDISHI WA HABARI/MAUWAJI YA WANASIASA MIKONONI MWA POLISI".

Mauwaji ya askari polisi uchunguzi umekamilika na majibu yametoka ndani ya siku 4, ila ni miaka mingi ishapita uchunguzi na hatujapatiwa bado majibu ya;

1) Kushambuliwa kwa Tundu Lissu.

2) Kupotea kwa Ben Saanane.

3) Kupotea kwa Azory Gwanda.


● Raia waliopotezwa, kuuliwa, kutupwa kwenye viroba, kutekwa, kuonewa, kutapeliwa na kuibiwa katika mikono ya polisi ni mamia kwa mamia, ila hakuna majibu ya uchunguzi mpaka leo??? Au ni kwakua hao mamia ya raia sio muhimu kuliko askari 3???

● IGP Sirro ana majibu gani kwenye hizo hoja? Zaidi ya kutukana na kukebehi wazazi wa watu wenye uchungu wa kupoteza kijana wao?????

"HAMZA" hata hao CCM wenzako uliokua unawadhamini, ukiwasaidia na ukiwaunga mkono kwa hali na mali wamekaa kimya juu ya kifo chako.

Umekufa kifo cha kiume na damu yako imemwagika kishujaa kuliko ungetekwa na kutupwa kwenye kiroba kama mzoga na hao jamaa.
 
hao wahuni wa Chadema ni wa kupuuzwa wala sio wa kuhangaika nao, na tutaendelea kuwalinda wao na mali zao, na ole wajiingize kwenye vitendo vya kigaidi tunashughirika nao tena bika huruma
 
Ni kweli kuna wakati watendaji wetu wanatenda kwa MIHEMUKO lkn ni kweli pia tunawasababishia hiyo Mihemuko.
Na kizazi hiki cha Uovu ukatiri ni njia ya kupunguza uovu, japo ni temporal.
Kwa kuwa dhambi inaenea kama kansa. Dawa pia ni Mionzi MIKALI na UPASUAJI.
No more
 
Mtoa maada yupo sahihi,Kuna Mambo ukisikia unashindwa kujua hivi taifa Lina watu wa namna gani
 
Siro yuko sahihi. Ni magenge ya wahuni tu na magaidi yanayompinga Siro.
 
Nashangaa kwanini bado hajatimuliwa, labda wale Axis of Evil hawataki aondolewe.
Kwa kauli kadhaa za hivi karibuni za sirro ni wazi amelemewa, anahitaji kusaidiwa kazi na mamlaka yake ya uteuzi.
 
Usitukumbushe kibiti raia waliopotea hadi muandishi wa habari aliyetaka kufichua ukweli
 
Hiyo familia ya SIMON SelO inajisikiaje? Fikiria wewe ungekuwa baba yake SIMON SelO, mama yake SIMON SelO, mdogo wake ungejisikiaje kuzaa kwako UMETULETEA BALAA WATANZANIA? Kwahiyo naomba Watanzania wengine wasituzalie watoto kama SIMON SIRRO
 
Kwanza ndugu yangu ukiweka ushabiki pembeni alieuawa(Hamza)sio gaidi na kauli ya IGP haikuwa ya kiungwana kwa wazazi wote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…