WALOLA VUNZYA
JF-Expert Member
- Nov 20, 2020
- 7,154
- 7,155
Walishiriki kuharibu uchaguzi mkuu 2020 pia wamekuwa wakikamata watu pasipo makosa kwa sababu za kisiasa siasa kulinda chama tawala kwa namna yoyote ili,ona Mbowe yupo ndani kwa sababu tu ya kudai katiba mpya ambacho siyo kipaumbele cha ccm na akapewa kesi ya ugaidi na uhujumu uchumi,hata marehemu Hamza inasemekana alidhulumiwa dhahabu kimakusudi na jeshi hilo,kwa vile sheria ni yao jamaa akaona hana kitu mbele yao basi nikiua hata askari mmoja nao wakiniua nitakuwa nimefanikiwa kufikisha ujumbe kama Mkwawa kwa Wajerumani.Hivyo Polisi wajifunze kuwa jukumu lao siyo kulinda ccm na serikali bali usalama wa raia na mali zao.Katika pitapita zangu mitaani nimeshtushwa sana na wananchi badala ya kuhuzunika kwa gaidi kuuwa polisi wetu na badala yake wamegeuka wanawalaumu pili kwa matendo yao ya kubambikizia kesi,dhuluma,uonevu,kuchochea chuki,kuuawa raia wawapo mahabusu nk. Hii inaashiria kiti gani mbona si kawaida?
Napata mshituko mkubwa sana kuona rais wamekosa uzalendo wa kuliamini jeshi lao kiasi hiki. Polisi katika hili wajitafakari sana hii siyo kawaida, sasa watafanyaje kazi ikiwa raia hawatawapa Tena ushirikiano?
Lipo tatizo nadhani, hili jeshi linahitaji Reformation tena ya kikatiba kabisa. Recruitment ya polisi iwe ya hali ya juu sana, jeshi kulaumiwa kiasi hiki si kawaida.