Kapumpuli
JF-Expert Member
- Aug 11, 2018
- 2,040
- 2,674
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Samia Suluhu Hassan ndio Rais wa jamhuri ya muungano wa TanzaniaKwani tatizo nini? Mbona mnaonekana hamjaridhika samia kushika nchi? Mlitakaje labda ? Aapishwe majaliwa?
Kwa maoni yangu ni kuwa Mama samia Amerithi serikali ambayo yeye alikuwa sehemu yake na ilikuwa na malengo kulingana na ilani ya uchaguzi iliyowaweka madarakani pale, kwa hiyo swala ni ukamilishaji wa ilani ile.
Ni maoni yangu tu, siyo kuwa kwa vile karithi serikali na yeye ndiyo bosi basi ilani yao haina maana tena ila yeye ataleta ya kwa kwake tofauti; sidhani kama kweli mambo yanatakiwa yawe hivyo. Wenzetu husema elections have consequences, ambazo yeye atatakiwa azisimamie siyo kuwa azifute.
Nadhani shida kubwa kwake itakuwa ni katiba,hivi mkiangalia mle bungeni kuna watu wengine zaidi hao wanaomzunguka?Ni ukweli usiofichika kuwa kuna mkakati wa ndani ya Bunge na baadhi ya Mawaziri wakiongozwa na PM mwenyewe kum pre empty Rais Mama Samia ili ajikute anafanya kazi bila kwenda kinyume na mtangulizi wake JPM.
Mkakati huo unaoendeshwa kimahesabu sina hakika kama Rais ameshaushtukia au kwa vile timu ya wasaidizi wake ni ileile anaweza kuwa anafunikwa na blanketi na halioni hilo?
Je, ni kwa nini mbinu hizo chafu zinafanywa? Je, mama haoni kuwa kuendelea na wasaidizi wasio kubaliana kifikra kuwa yeye ni Rais kwa sasa itakwamisha mipango yake?
Hakuna Ramli za matusi labda kama neno tusi lina maana tofauti.yaani mnadharau mpaka ripoti ya CAG kulinda kivuli cha huo mzoga wenu? Mnamshangilia mpumbavu kibajaji kuua hoja za wasomi wa nchi hii???Kamanda hivi mnafikiri kwa upuuzi mnaweza kuifitinisha serikali? Muda unakuja, hamtapata mnayoyata mrudie kazi yenu ya ramli na matusi
Kwa sababu 1. Mambo aliyotekeleza magufuli chini ya usaidizi wake ni mazuri sana kwa watanzania. 2. Yeye anafuata ilani ya CCM hivyo ni muendelezo tu nothing else. Asituletee mapaya hatuyataki. Mapya ataanzisha akigombea na kushinda 2025 alete maono yake na azitafute pesa za maono yake!Ni ukweli usiofichika kuwa kuna mkakati wa ndani ya Bunge na baadhi ya Mawaziri wakiongozwa na PM mwenyewe kum pre empty Rais Mama Samia ili ajikute anafanya kazi bila kwenda kinyume na mtangulizi wake JPM.
Mkakati huo unaoendeshwa kimahesabu sina hakika kama Rais ameshaushtukia au kwa vile timu ya wasaidizi wake ni ileile anaweza kuwa anafunikwa na blanketi na halioni hilo?
Je, ni kwa nini mbinu hizo chafu zinafanywa? Je, mama haoni kuwa kuendelea na wasaidizi wasio kubaliana kifikra kuwa yeye ni Rais kwa sasa itakwamisha mipango yake?
Nanaamini kila mmoja anahitaji kufanya kitakachomjenga kiutendaji na kihistoria.
Kwa uelewa au matendo asilazimishwe mtu kuyaridhi kwani sio kila cha kuridhi ni hekima kama sio hivyo hakuna haja ya kuufuata mfumo wa mwenye mamuzi yake.
Wakina Job Ndugai wanataka kumpanda kichwani Rais wetu kipenzi, wakichekewa hawa vichaaa watatuletea majanga kama ya Magufuli ipo haja ya kuwashughulikia ASAP.Ngoja mfungo uishe.
Atawatimua woote wajuaji
Magufuli hakustahili kuwa Rais wa nchi hii, sema tu mifumo yetu ya mibovu ndiyo ilimfikisha pale."Kodi ya dhuluma, hapana"! Hii ni moja kati ya departure nzuri sana. Naamini na ule uozo na unyang'anyi wa DPP kwenye kesi za kubumba za uhujumu uchumi na money laundering hawezi kuendelea nao.
Ilani ya uchaguzi ya ccm haina shida. Shida ilikuwa ni namna inavyotekelezwa.
Unaweza kupambana na ufisadi bila kuonea watu. Unaweza kukusanya kodi bila kuonea watu. Kuwapa watu uhuru wa maoni, habari na kufanya siasa ni haki za kikatiba.....kunyima haki Hizi haikuwahi kuwa ilani ya ccm.
Sasa mama aki depart kwenye hayo mambo ya hovyo hovyo ya JPM kuna shida gani?
JPM alikuwa ana abuse sana madaraka yake makubwa kama Rais, hakuwa na staha pia unazotegemea Rais wa nchi awe nazo (e.g. Rais anawezaje kumwambia mwananchi wake kuwa " abaki na mavi yake nyumbani" ....tena hadharani! Alikuwa anatia aibu tu)