Kwanini wanataka kuzuia Rais Samia Suluhu asiende kinyume na Hayati Magufuli?

Kwani tatizo nini? Mbona mnaonekana hamjaridhika samia kushika nchi? Mlitakaje labda ? Aapishwe majaliwa?
Samia Suluhu Hassan ndio Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania
Samia Suluhu Hassan ndio mweyekiti wa chama kubwa CCM
Samia Suluhu Hassan ndio mama wa kwanza wa taifa

Kazi iendelee
 
Mimi naamini Rais yuko kipindi cha mpito anajipa mda,hata Magu aliwateua Wana JK lakini alipojipa mda hawakuchukua round akawatema wote ko hata hao hawana miaka 2 alishasema wataachwa njiani
 

Mkuu uko sahihi lakini sidhani Mama anataka kufuta matokeo ya ilani. Nadhani anataka kutumia njia nyingine na ni njia hizo ndio wengi bungeni hawataki zibadilishwe.

Kufunga shughuli za siasa ilikuwa na faida kwa CCM kwa sababu marehemu alitumia nafasi yake kama mwenyekiti kufanya siasa!! CCM haitaki uhuru wa habari, inataka Polisi ifanye kazi kwa mabavu badala ya sheria. CCM inataka kushika hatamu na huenda mama anadhani taasisi ya uRais ndio ishike hatamu.

Matokeo hayana shida, shida ziko kwenye njia. Na ni bahati mbaya njia za marehemu zinaanikwa na Mama kama hazikuwa sahihi na zikome. Anataka haki, jambo gumu sana kufanywa na CCM.
 
Nadhani shida kubwa kwake itakuwa ni katiba,hivi mkiangalia mle bungeni kuna watu wengine zaidi hao wanaomzunguka?
 
Kamanda hivi mnafikiri kwa upuuzi mnaweza kuifitinisha serikali? Muda unakuja, hamtapata mnayoyata mrudie kazi yenu ya ramli na matusi
Hakuna Ramli za matusi labda kama neno tusi lina maana tofauti.yaani mnadharau mpaka ripoti ya CAG kulinda kivuli cha huo mzoga wenu? Mnamshangilia mpumbavu kibajaji kuua hoja za wasomi wa nchi hii???
Ukiwa ccm unakuwa mpumbavu tu
 
Kwa sababu 1. Mambo aliyotekeleza magufuli chini ya usaidizi wake ni mazuri sana kwa watanzania. 2. Yeye anafuata ilani ya CCM hivyo ni muendelezo tu nothing else. Asituletee mapaya hatuyataki. Mapya ataanzisha akigombea na kushinda 2025 alete maono yake na azitafute pesa za maono yake!
 
Kwa mtu yeyote aliyefanya kazi kama makamu atakubaliana nami kuwa wakubwa hukera na pia hufurahisha.
Ikitokea unashika madaraka kuna utakayoyatupilia mbali na utakayoyaendeleza.
Tusilazimishe hiyo ndiyo hali haalisi
 
Nanaamini kila mmoja anahitaji kufanya kitakachomjenga kiutendaji na kihistoria.

Kwa uelewa au matendo asilazimishwe mtu kuyaridhi kwani sio kila cha kuridhi ni hekima kama sio hivyo hakuna haja ya kuufuata mfumo wa mwenye mamuzi yake.

Rais hatekelezi majukumu yake kwa sababu ya kutaka kujijengea historia nzuri, bali anatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa kanuni za kisheria na kikatiba zilizopo wakati huu. Historia itamfuata yenyewe baadaye. In fact viongozi ambao hujiaribu kufurahisha historia, huwa wanakuja kuumbuliwa sana na historia hiyo kwani historia huwa haiandikwi na watu unawafurahisha sasa hivi bali huandikwa kwa ujumla wake kuangaliajinsi mtu alivyotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa kanuni zilizokuwapo.
 
Magufuli hakustahili kuwa Rais wa nchi hii, sema tu mifumo yetu ya mibovu ndiyo ilimfikisha pale.
 
Ni kazi sana kujua jinsi mambo yanavyofanyika bongo
 
Na mandumi la kuwili yamejaa 'mjengoni'!
Mama yetu Raisi Samia (Iron lady) kuwa makini sana na hawa wanafiki wakubwa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…