Kwanini wanaume huwa na michepuko?

Kwanini wanaume huwa na michepuko?

wala hapo unakuwa hujafanya kilicho sawa kwani utakuwa unataka kufanya mashindano na mwanaume na kiukweli kabisa siku zote pakiwepo na mashindano kati ya me na ke mara zote me hushinda na ke hubaki kajichafua na wala hafiki popote so badala ya kutumia nguvu zako nyingi kushindana na mwanaume ni mara mia kuachika.
Alafu kama ni mimi huyo mama yani siondoki hatuachani natafuta king"amuzi changu akieda kwa kimada wake na mie huyoooo nikirudi mie hoi najilalia na wanangu maisha yanenda ya nn kuangaika uje kufa presha upate na kisukari na vidonda vya tumbo maisha yenyewe haya yashakuwa mafupi hivi aaaaggggr
 
babu Asprin usituharibie waume zetu vijana kwa hizo justification zako za cheating, kulakuso mbee!

kama wewe bibi alikubaliana na hilo its okay, plz usitake kuhalalisha dhambi hii.

nampa pole mama aliyekumbwa na dhahama hii, ila cha kujifunza hapa, kufanya fujo haibadili ukweli.. tulia, tafakari ..then ndio uchukue hatua.
 
Last edited by a moderator:
kwa vigezo vipi?mbona Mungu alipomuumbia adamu mke mbona alimuumbia mke mmoja tu?kama angejua mwanaume hastahili kuwa na mke mmoja tu kimaumbile si angemwumbia wanawake wawili?

Mke wa Adam hakuwa mzembe kama nyie. Alimtosha Adam sio nyie wachovu kazi kulalamika tu, kila saa mmechoka.
 
MKE NA NYUMBA NDOGO NANI WA MUHIMU ZAIDI?

Nimepata swali hili kutokana na kisa hiki nilichokishuhudia:

Hivi majuzi kuna mwanamke alipewa taarifa kuwa mume wake alikuwa na kimada sehemu Fulani(almaarufu kama nyumba ndogo) mwanamke huyo aliamua kwenda kushuhudia ikiwa kinachosemwa ni cha kweli au watu tu wasioitakia mema ndoa yake pendwa,kufika huko alikuta kuwa kilichosemwa ni kweli mtupu tena hamna chumvi,kwa wivu wa mapenzi kwa mumewe (tena wanasema uchungu wa mume aujuae mke!) mwanamke Yule aliamua kuisogelea nyumba ndogo ya mumewe ili kuivagaa lakini kabla hajatimiza lengo lake tayari mume wake alishafika karibu yake kwa ajili ya kuilinda nyumba ndogo yake isipigwe na mama watoto wake watatu!!!!!!!!!!!!!!!!

Kibaya na cha kusikitisha mume huyo hakuishia tu kudhibiti mke wake bali pia kumpiga makofi kadhaa na kumzuia kwa hali na mali kutoisogelea nyumba ndogo yake,ambayo na yenyewe ilikuwa ikimjibu mwenye mali kwa jeuri zote,jambo lililopelekea mke kuondoka akiwa na uchungu mkali na maumivu ya mapenzi ndani ya moyo huku nyuma akifuatiwa na mumewe msaliti,ambaye mara baada ya kufika nyumbani alianza kumshambulia kwa maneno ya kejeli bila hata walau kuomba msamaha kwa usaliti alioufanya kwa siku hiyo,mke akaongezewa maumivu juu ya maumivu.(nadhani sote tunaelewa jinsi mapenzi yanavyoumiza na kwa hiyo tunaelewa vizuri kabisa jinsi mwanamke huyu alivyokuwa akihisi kwa wakati huo)!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Kisa hiki kilinipa maswali kadhaa kwa wanaume wenye nyumba ndogo:

1.Hivi ni nani bora zaidi kati ya mke wa ndoa na nyumba ndogo?

2.kama ni nyumba ndogo,umuhimu wake uko wapi kuushinda ule wa mke anayejua usiku umelalaje,umeamkaje na kukuzalia watoto kwa moyo mmoja licha ya uchungu mkali?

3.assume ndo wewe sasa unamfuma mkeo ana mwanamume mwingine na mkeo anaanza kukuponda na kumtetea Yule mwanaume mwingine,hiyo imekaaje?utajisikiaje?unahisi itakuwaje baada ya hapo? utachukua hatua gani mkifika nyumbani?

4.kama utaumia,unapomfanyia mkeo kisa kama hicho unafikiri yeye anahisi vipi?au unaamini kabisa hana hisia ila ni jiwe?au unaamini kuwa kwa wewe ni halali kabisa kumtenda hivyo ila sio yeye?

5.hivi nini unachokosa kwa mke na kukipata kwa nyumba ndogo?

6.kama kuna unachokikosa umewahi kujaribu kukaa chini na mkeo na kumweleza akupe unachokosa?

7.ikiwa ni wewe mwenyewe tu umejitune kuwa na mwanamke zaidi ya mmoja,hivi inashindikana kuonyesha heshima licha ya kuwa na nyumba ndogo?

8.ikiwa umeshindwa kuonyesha heshima na mambo yako kujulikana na mkeo kufika eneo husika ukiwa na nyumba ndogo yako,hivi unahisi kupungukiwa ikiwa utaamua kuwa upande wa mkeo walau mara moja?walau kuthibitisha yale maneno yako uliyoahidi ya kumpenda nyakati zote kwenye shida na raha siku ya ndoa yenu?


Najua wapo baadhi ya wanaume walio na nyumba ndogo na wasio nazo pia, kwa hiyo karibuni wote tuchangie mawazo yetu kuhusu hili suala kwa wale wenye nazo watupe majibu ya:

Ni nani bora wake zao majumbani au nyumba zao ndogo? na nini kinawapelekea kuwa na hizo nyumba ndogo?ikiwa nyumba ndogo ni muhimu zaidi,umuhimu zaidi wa nyumba ndogo unatokana na nini?

Na kwa wasio nazo pia nao wanakaribisha kutueleza

Wanawachukuliaje wanaume wenzao walio na nyumba ndogo na kuzithamini zadi nyumba ndogo kuliko wanavyowathamini wake zao?

Karibuni wana MMU.

Mada yako ni nzuri,muhimu na ya kufikirisha kama mwanaume nimekaa nakajitafakari bila upendeleo nikajiuliza maswali muhimu kuliko yote JE NIMEWAHI KU MCHEAT GIRLFRIEND WANGU? JIBU NI NDIYO.JE NIMESHAWAHI KUMVUNJIA HESHIMA? JIBU NI HAPANA.JE NIMESHAWAHI KUMDHALILISHA MWANAMKE KWA SABABU YOYOTE IKIWEMO YA MAPENZI JIBU NI HAPANA.SASA KWANINI NILI CHEAT? JIBU NI UPUUZI NA MALEZI YETU KAMA WATOTO WA KIAFRIKA TUNAVYOLELEWA TUNALAZIMISHWA KUWA MA HERO TUSIOSHINDIKA TULIOZUNGUKWA NA WANAWAKE KAMA KING MSWATI YAANI KUWA WANAWAKE NI ALAMA YA UFAHARI NA BAHATI MBAYA NA WANAWAKE WAMEATHIRIKA NA SAIKOLOJIA HIYO TAZAMA MWANAUME MWENYE KUPENDA KUCHEZEA WANAWAKE VILE WANAWAKE WANAVYOMPAPATIKIA HATA KAMA AWE NA SURA KAMA YA DIAMOND.KWA HIO SISI SOTE NI VICTIM WA MFUMO DUME.NDIYO MAANA WANAUME WANAWAOGOPA WANAWAKE WALIOJITEGEMEA SABABU WAKO HURU TOKA MFUMODUME.
 
USILOLOPENDA KUTENDEWA WEWE USIMTENDEE MWINGINE - Blue G
 
Last edited by a moderator:
asante mkuu.
usijali mkuu kawaida hiyo tatizomatamanio sometimes huwa yanatushinda nguvu na kupelekea kuchepuka but ni jukumu letu kuyashinda kuendekeza kuchepuka sio dili wala nini??
 
nimeipenda hiyo attitue yako lakini nia swali moja tu kwako mkuu Tarime one,hapo kwenye red em naomba nikugeuzie kibao wewe ni sababu ipi anayoweza kuitoa mkeo kama kigezo cha kuchepuka ili uweze kumwelewa na kuona kuwa hakukosea kuchipuka?

Mkuu Blue nimesema swala la michepuko limegawanyika katika sehemu 2,kwanza wale wanaochepuka kwa kuwa ni tabia yao,na wale wanaoamua kuchepuka coz kuna kero na karaha ndani ya ndoa,.kuchepuka hakuepukiki kwa mwanaume rijali Ila najitahidi kutomwonyesha wife.
 
Last edited by a moderator:
si rahisi kama unavyosema nkungwe123 mtu anaweza kuamua kukaa kimya tu lakini ukweli ni kwamba mapenzi hayagawiki nenda uendako mkuu huwezi kuta mtu karidhikika tu kushare penzi la mume/mke na mtu mwingine,na mara zote ukianza michepuko tu,jua lazima kuna upande utaegemea tu no way na ndo hapo unapoazna kuleta hisia za mashaka na kuleta udadisi kuwa kuna nini kinacheondelea,au wewe ukiona mabadiliko kwa mkeo utanyamza tu?au kwa kuwa wewe ni mwanaume ni ruksa kumfuatilia ila yeye akuache tu?
Hakuna kilicho bora au aliye bora kwa mazingira yote na wakati wote. Take note.
Ndoa za Leo ni comparison ya fatuma vs Sarah. Unategemea nini hapo.... hapo hata iweje kuna siku atammic Sarah au fatuma na kumtafuta kwa shughuli. Mhm usitafute hbr itakayokuumiza nafsi. Kwa usalama wako, ishi kwa assumption kuwa mko wawili tuu na watoto wenu
 
Last edited by a moderator:
kwa nini usimwombe kama ni vizuri na vinafaa kimaadili? haya hata kama ikitokea umekutwa na mkeo,kwa nini uwe upande wa huyo kimada wako?ina maaana yeye ndo wa maana kuliko yule aliyeamua kuwa na wewe?kwa lipi kwanza?kukupa mambo ambayo mkeo hawezi kukupa? umeyatolea wapi hayo mambo?vijiweni na kutoka kwenye stori za washkaji wako?porn movies?kama usingeenda huko ungevijuaje hivyo vitu unavyoviita kuwa ni adimu?

Kwa mfano wewe mmeo akiomba umpe tigo utampa au utamchukuliaje? Sasa nyumba ndogo zina akili sana. Zinajua wake huwa hawatoi hiyo makitu kwa waume zao. Sasa wao hawasubiri kuombwa, wanatoa wenyewe.... na bado kuna vingine tu kibao.
 
Heshima gani aliyoionyesha hapo mkuu? Kwa kumpiga mkewe mbele za kimada au?

Lile ni somo la vitendo juu ya mipaka ya kitafuta hbr za mume. Je, km asingekwenda angepogwa? Na alijiamini nn kwenda kuanzisha ugomvi kwenye nyumba ya watu?
 


laiti ingefaa ningekupa like 100 TIMES nami nimeaambia huku kweye blue ndo ukweli wenywe

watakufa waache watoto yatima au apate kovu la uzeeni kisa nini...

sifuatili mtu yoyote as long as ananipa mhitaj yangu

Hakika wewe ni mwanamke muelewa. Wife material na mama bora.
 
Owen i wanawake mnao wapenda wawili, watatu mpaka wanne tu. Shida iko wapi mwache wampige makofi tu😛eace:
 
si rahisi kama unavyosema nkungwe123 mtu anaweza kuamua kukaa kimya tu lakini ukweli ni kwamba mapenzi hayagawiki nenda uendako mkuu huwezi kuta mtu karidhikika tu kushare penzi la mume/mke na mtu mwingine,na mara zote ukianza michepuko tu,jua lazima kuna upande utaegemea tu no way na ndo hapo unapoazna kuleta hisia za mashaka na kuleta udadisi kuwa kuna nini kinacheondelea,au wewe ukiona mabadiliko kwa mkeo utanyamza tu?au kwa kuwa wewe ni mwanaume ni ruksa kumfuatilia ila yeye akuache tu?

Mm simfuatilii mtu mzima na akili zake. NEVER WILL I DARE DO THAT.
 
Last edited by a moderator:
babu Asprin usituharibie waume zetu vijana kwa hizo justification zako za cheating, kulakuso mbee!

kama wewe bibi alikubaliana na hilo its okay, plz usitake kuhalalisha dhambi hii.

nampa pole mama aliyekumbwa na dhahama hii, ila cha kujifunza hapa, kufanya fujo haibadili ukweli.. tulia, tafakari ..then ndio uchukue hatua.

Siwaharibu mimi dada bali necha..... Mwanaume kuwa na mchepuko haipukiki. Waangalieni mafahari, mabeberu na majogoo. Mitetea haina akili lakini inaelewa.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom