Kwanini Wanaume wengi wakiingia kwenye Ndoa wanapata kitambi?

Kwanini Wanaume wengi wakiingia kwenye Ndoa wanapata kitambi?

Ila kuna wanaokondeana kama mfupa wa samaki. Baadhi ya wanaopata vitambi ni matunzo mazuri ya wake zao.
 
Kwasababu ukioa unaanza kulazimishwa kula hata kama hauna njaa ukisema umeshiba unaambiwa umeshakula kwa wanawake zako
Unakula mara 2 kabisa kama sio mara 3 [emoji23][emoji23]
 
Iko hivi,Mwanamke kabla hamjaoana,anakupenda kwa ule muonekano wako,umbo lako zuri,uvaaji wako mzuri,pato lako n.k
Mkishaoana,mambo huwa kinyume.Atajitahidi uwe na muonekano wa ki father zaidi,ili usivutie wanawake na vibinti vingine.Atakomaa ule vyakula vyenye mafuta na wanga mwingi,ili unenepe,uwe bonge na kitambi,upoteze mvuto kabisa.
Hata nguo atajitahidi uache kuvaa cardets na jeans,atakushonea mashati ya vitenge na suruali za vitambaa zenye upana kama za Kim jong Un,ilimradi upoteze mvuto na usiwavutie wanawake wengine,uwe wake peke yake.
Duuu Mimi sikubali kuvalishwa Aina za Nguo ambazo siyo chaguo langu
 
Moja kwa moja kwenye mada, kwanini wanaume wengi baada ya kuingia kwenye ndoa tu haipiti muda wanaanza kuota vitambi. Yani kumjua mwanaume kama ameoa ni rahisi sana asilimia kubwa wanakua na vitambi.

kwanini inakua hivi, kifanyike nini ili wawe kawaida kama wale ma bachela KATAA NDOA 🙂

.......

Nina miaka 15 kwnye ndoa na sijawahi kuwa na kitambi dah😀😀🙁🙁🙁 masikitiko!! Ila mke keshazidi mara 3 ya uzito aliokua nao kabla sijamuoa, kimsingi ni kipipa flani hivi! Sijashibishwa bado labda na mke wangu mchaga mnaowasifia sana hapa
 
Nina miaka 15 kwnye ndoa na sijawahi kuwa na kitambi dah😀😀🙁🙁🙁 masikitiko!!
Prof atakuwa na furaha tele akisoma hapa
1000016734.jpg
 
Iko hivi,Mwanamke kabla hamjaoana,anakupenda kwa ule muonekano wako,umbo lako zuri,uvaaji wako mzuri,pato lako n.k
Mkishaoana,mambo huwa kinyume.Atajitahidi uwe na muonekano wa ki father zaidi,ili usivutie wanawake na vibinti vingine.Atakomaa ule vyakula vyenye mafuta na wanga mwingi,ili unenepe,uwe bonge na kitambi,upoteze mvuto kabisa.
Hata nguo atajitahidi uache kuvaa cardets na jeans,atakushonea mashati ya vitenge na suruali za vitambaa zenye upana kama za Kim jong Un,ilimradi upoteze mvuto na usiwavutie wanawake wengine,uwe wake peke yake.
🙆🏽‍♂️🙆🏽‍♂️🙆🏽‍♂️Kumbe et!
 
Inategemea, Kuna ambao ni ongezeko la bia baada ya kushinda bar akikimbia kelele.
Mbali ya kukimbia kelele, mume akishinda nyumbani anaweza kupewa jukumu la kutenga sufuria jikoni.
 
  • Kicheko
Reactions: Tsh
Moja kwa moja kwenye mada, kwanini wanaume wengi baada ya kuingia kwenye ndoa tu haipiti muda wanaanza kuota vitambi. Yani kumjua mwanaume kama ameoa ni rahisi sana asilimia kubwa wanakua na vitambi.

kwanini inakua hivi, kifanyike nini ili wawe kawaida kama wale ma bachela KATAA NDOA 🙂

.......
Ndoa tamuu..sana yaani usiku unageuziwa traaako hilooo...!
Utaachaje kutoka kitambi.!
 
Ni kweli,mimi baada ya kutoka home na kuwa na kwangu,tulikuwa tunakula mpaka naona sio poa

Afu sijui wanawake wapoje kwenye kula ni kama anakutegea unajikuta umekula chakula kingi,akipakua ukimwambia punguza hatak analazimisha ule hicho hicho alichopakuwa

Kuna wakat nikiwa nipo asubuh nilikuwa namgomea sinywi chai,maana nikishinda nyumban nakuwa kama chura tumbo ndii
😂Jaman kwann chura!
 
Iko hivi, Unapokuwa kwenye ndoa kuna namna baadhi ya majukumu yanagawanyika automatically, tofauti na ulipokuwa bachelor. Majukumu kama kupika, kuandaa chakula, kupakua, kuosha vyombo nk. moja kwa moja yanahama kutoka kuwa majukumu yako yanakuwa majukumu ya mke wako, ambaye kimsingi linapokuja suala la jikoni na mambo ya usafi wao ndiyo pro kwenye hicho kitengo. Na mara nyingi huwa wanajitoa kweli katika kitengo hicho ili wewe upate nafasi ya kuwaza mambo mengine mfano kutafuta pesa, kujenga, ada, watoto waende shule nk.
Huo mgawanyo unakuja automatically, Kwa hiyo linapokuja suala la misosi as long as unaacha bajeti, hilo sio suala lako, ni suala dogo sana kwa mkeo, Atakupikia supu chapati asubuhi, mchana utakula makange ya kuku mixer nazi, jioni atatoa kuku kwenye friji anarost mnakula biryani la kuku! Haujakaa sawa mara amekaanga vimayai vyake anakuletea, yaani tena ukute mwanamke anayependa kujaribu kupika pika na utundu wa jikoni, Kumbuka wala hautahangaika kuwaza kwamba hivyo vyakula vimeandaliwaje sijui saa ngapi sijui nani kaosha vyombo 😀 wakati huo akili yako imeshavurugwa inawaza mambo ya kazini huko na upataje pesa ya ujenzi! Maisha yakiendelea hivyo haumalizi miezi mitatu kitambi hicho hapo!
 
Back
Top Bottom