Nyooolooo siwezi maisha ni mafupi, hela hata uzibanie elfu 50 haiwezi kununua gari.
Mwezi wa 11 nilikuwa naenda nyumbani kijijini nikafika mjini gari za nyumbani zimeisha nikasema siendi kwa shangazi staki jam afu mbali na stend.
Nikawauliza washikaji zangu hotel nzuri wakanambia kuna lodge za 20 nzuri nikasema nataka hotel. Nikawaza hivi hotel nzuri lazima nilale nikiwa nimetoka na mwanaume?
Nikaingia Google map location hapo nilipo simama stend hotel zote nikawa nikaziona.na hiyo hotel walonambia ikiwemo. Chap naita tax wakasema sister iko karibu tukubebee mabegi, chap tukafika dah mazingira safi , wakasema sh 50, 000 sikutaka hata longolongo wakanionesha room.
Sasa wale washikaji walonisindikiza wakauliza nina shemeji.? Yaan hawaamini nalala pale mwenyewe.. kuingia mule chumba kina kila kitu cha muhimu. Nikaoga maji safi msosi nikaletewa, nililala kama beibi mashuka makali duvet coton ile ya kiwango ,achana na zile za kariakoo za elfu 30 dah, dah sikujutia hela yangu
Asubuhi naamshwa chai ya nguvu na supu ya kuku dah.
Saa 3 asubuhi wale washikaji zangu , ni wa kitambo tangu nasomaga sekondari wakogo hapo stend wakaijia mabegi yangu nikawapiga breakfast ya maana nkaenda zangu kijijini kujilia ndizi.