Kwanini wanawake mnakimbilia kupanga mkipata kazi?

Kwanini wanawake mnakimbilia kupanga mkipata kazi?

Kwani mwanamke akipanga chumba na akachelewa kuolewa kwani hazeekei hapo alipo panga chumba?
Tena huku kwenye kupanga ndio anazeeka vibaya maana wengi huwa wanakuwa na mahusiano ya watu wengi ili walipiwe bili so uaminifu ni zero na hakuna mwanaume anapenda mwanamke mwizi mwizi wa mahusiano.
 
Kama yapi mkuu? Mm nitamrusu binti yangu kupanga iwapo atakuwa amepata kazi nzuri na yenye mshahara mzuri mbali na nyumbani kwangu, tofauti na hapo haondoki nyumbani na akirazimisha kuondoka akatufute baba yake mwingine.
Ni kweli kuna mdogo wetu wakike aliondoka nyumbani kwenda kupanga chumba kwa kisingizio nyumbani ni mbali na chuo na wenzake wanajisomea usiku na yeye hana kosa kuwa nao pamoja, alivyoenda kupanga chumba na wanachuo wenzake baada ya miezi 6 akarudi nyumba naisi maisha yalimshinda, nilimwambia kama unaenda kupanga kwa kutegemea mkopo wako wa chuo husituombe pesa ya chakula.
 
Kukaa kwa ndugu mtihani aisee. Mimi nilianza kupanga nina miaka 25
 
Huwa wanapenda kuwa huru na hakuna binadamu asiyependa uhuru.
 
Mshahara wa Laki 2 unasema anakimbilia kupanga kweli humu kilamtu yupo BOT aisee

Ukiwa na mashara wa 200K kwa Mwezi kwasasa shukuru Mungu labda hujui watu wamepanga hawana uhakika wa kipato kabisa tuounguze standerd hizi standard za Mtandaoni tofauti kabisa na huku mtaani
 
Hata kama, Laki na nusu sio hela mkuu Kwa maisha ya Sasa amabyo Kila kitu kinahitaji pesa..
Yaan unakuta manzi hata sura haieleweki maana imemkomaa hatari hela ya lotion hana
Ukizungumzia maisha ya sasa kupata kazi yenye mshahara mzuri sio rahisi unaweza fika miaka 35 usiipate nenda jukwaa la ajira na kazi uone watu kwahio utakaa home mpaka 40 inafika pia na kupata hio kazi unaweza usiipate....90% ya watu mtaani kipato chao hakizidi 300K kwa Mwezi na mwenye 300K anavimba na kila kijana anatamani awe na hio kazi

Napofanya kazi Kuna jamaa ana miaka 35 mshahara wake hauvuki 150K kapanga na ana mke na mtoto na week kadhaa alikuwa anauguza ndugu yake huyu unasema kakimbilia kupanga maisha hayana fomula
 
Kama Hana Ndugu mjini anabidi wakae gheto moja watu watatu ili wafanye cost sharing hii kwa kipato Cha 200k anaweza kuishi vizuri tu.
Hii ni sawa kabisa na itawasaidia mabinti wengi mjini hapa, tatizo lao wanaona wanajiweza in reality hali zao ni mbaya kiuchumi.
 
Wewe unataka kuhalalisha uongo wako kuwa ukweli, yaani akuambie tu ondoka kwangu kwa sababu ya makosa madogomadogo hapana, kwanza unarudishwa kijijini kwenu Moshi Arusha ili akawaeleze wazazi sababu ya kukurudisha nyumbani, au ulikimbia nyumbani mwenyewe kwa sababu unazozijua wewe.
Sass unabisha nini?... nilogombana na mke wake...akaniambia niondoke nyumbani kwake
Baada ya kipigo kikali.

Nikasepa nikaenda kaa na bf wangu chumba kimoja.. akasema ndugu zake hua wanakuja kwaiyo nitafute chumba changu...kwakua nlikua nakazi...nikapanga
 
Me hapana jamani. Sina tabia za kuhitaji uhuru wa hivyo.
Ningekuwa mtaa mmoja na wazazi wangu. Wallah nisingechezea pesa kulipia kodi na kujilea.
Kabisaaaa yaani[emoji2]
 
Back
Top Bottom