Kwanini wanawake Waislamu hawaruhusiwi kwenda makaburini kuzika wapendwa wao?

Watu waheshimu imani za wengine. Mnaotaka kujua kwanini wanawake hawaruhusiwi makaburini kwenye uislamu jiungeni na uislamu ili mjifunze.
Mkuu hakuna ambaye aheshimu dini ya mtu!

Nadhani ni vizuri kama unamajibu uyaweke hapa ili na wengine tujifunze!

Ukiangalia wanawake wengi wa Kiislam huwa wanalalamika sana kunyimwa fursa za kuwasindikiza Wapendwa wao makaburini ili nao wakashuhudie wakizikwa!,sidhani kama ni vibaya!

Ndiyo maana jamaa alitaka kujua ni kwanini Dini ya Islam hairuhusu mwanamke kwenda Makaburini?

Je,Aya za maandiko ya Quran zinasemaje kuhusu hilo?,Je unaweza ukaweka hapa Aya kadhaa ili tusome sote tujifunze?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…