Kwanini wanawake Waislamu hawaruhusiwi kwenda makaburini kuzika wapendwa wao?

Kwanini wanawake Waislamu hawaruhusiwi kwenda makaburini kuzika wapendwa wao?

Ni tafsiri mbovu tu za dini yenyewe. Huko Saudi Arabia hadi mwaka 2015 wanawake walikuwa hawaruhusiwi kuendesha magari.

Ila alipokuja mwana wa mfalme Mohamed Bin Salaman akaona kuwa ni UDWANZI wala Quran haijawazuia.

Akaruhusu waanze kuendesha kuanzi mwaka 2017 hadi leo.

Waislamu acheni kukariri, kuweni extrovert
Kuendesha gari haipo katika makatazo ya dini bali ni katika desturi zao tu Saudia
Kwani nchi zote za kiarabu wanawake wanaendesha na walikuwa wanaendesha siku zote
Ni maamuzi ya Wasaudi ila halihusiani kabisa na dini
 
Kwa nini wanawake Waislamu hawaruhusiwi kushiriki shughuli muhimu za maziko kama hata kwenda makaburini kuzika wapendwa wao?
Hii ni.mojawapo ya Heshima kubwa waliopewa wanawake wa kiislamu,wanaume ndio wafanye kazi ya kuzika na kuwalisha na kuwapatia.mahitaji yao wanake na Vile vile
1:WAKIWA KWENYE SIKU ZAO,WAMEPEWA NAFASI KUPUMZIKA,WASIFANYE IBADA YA KUSWALI AU KUFUNGA.
2.Wakishajifungua pia wanapewa siku 40,za kutofanya ibada,akitoka kujifungua.
3.Vike vile pepo,iko chini ya mama mzazi(mwanamke),ikiwa mtoto amemtendea ubaya mama yake,hata afanye ibada vipi,haingii peponi.
4.Mwanamke,halazimishwi kuolewa na mume asiyemtaka.
5.Mahari ya ndoa ni pesa yake mwanamke muolewaji,na ndiye anayetaja kiwango cha pesa anachotaka.
6.Mtoto akifariki awe wakiume au wa kike,anapewa ubini wa mama.
 
Kiswahili ni cha nyinyi waarabu na dini yenu. I have my vernacular, well articulated, and then, between the two foreign languages, one from Arabia and one from the Western world, I opted for English, not Swahili!

Ujinga ni kujifunza lugha ya Waarabu! Siwezi! Na form 4 nilipata F maana sikuisoma kabisa!
Maneno ya kiarabu huwezi kuyakwepa,hata Hisabati tunayosoma ni maandishi ya kiarabu,kuanzia 0123456789,na pia maneno kama darasa,kemia,khatibu,Rais,Waziri,Dar es Salaam,msamiati,Hutuba,Hazina,Suruwali,nk ni maneno ya kiarabu.Na haya masndishi tunayoyatumia ni Kilatini,mzungu hana alphabet(neno la kiarabu),anatumia kilatini,lakini muarabu ana alphabet yake.
 
Katika Uislamu, suala la wanawake kutembelea makaburi linaweza kuhusishwa na sheria na kanuni za dini, lakini pia lina muktadha wa kihistoria na tamaduni.

1. Hadithi:
Kuna hadithi zinazosema kwamba Mtume Muhammad aliwaonya wanawake dhidi ya kutembelea makaburi. Hizi zinaweza kutafsiriwa kama tahadhari dhidi ya mazoea yasiyofaa, lakini sio kama sheria kali.

2. Qur'an:
Hakuna aya maalum katika Qur'an inayokataza wanawake kutembelea makaburi. Qur'an inahimiza kumbukumbu ya waliokufa na kujifunza kutokana na maisha yao.

3. Tafsiri za Wanazuoni:
Wanazuoni mbalimbali wanatoa tafsiri tofauti kuhusu hadithi hizi. Wengine wanaona kuwa ni muhimu kwa wanawake kutembelea makaburi kama sehemu ya kutoa heshima, wakati wengine wanaweza kuzingatia hadithi kama kanuni ya kutoenda.

4. Muktadha wa Kijamii:
Katika muktadha wa historia, wanawake walihusika katika kutembelea makaburi, na hali hiyo inaonyesha kuwa desturi hizo zilitofautiana kulingana na jamii na wakati.

Kwa hivyo, suala hili linaweza kuwa na sheria na kanuni, lakini pia linaelezwa kwa njia ya muktadha wa kihistoria na tamaduni tofauti. Kila jamii inaweza kuwa na mtazamo wake, na ni muhimu kufuata maongozo ya viongozi wa kidini.
Sheikh ila kuzuru na kuhudhuria mazishi ni mambo mawili tofauti kabisa ingawa hadithi nyingi zinasema marufuku, kukatazwa kwao ni kwa sababu wako emotionally zaidi na kilia sana kwa sauti ndio haitakiwi
Na Mungu anajua zaidi
 
Hiyo sababu itakuwa haina mashiko, Mbona kwenye huo msiba wanaume ndio wameonyeshwa wanalia kuliko wanawake!
wale ni wanaume jamii ya wanawake 😀 😀 😀 😀 😀
 
Kuendesha gari haipo katika makatazo ya dini bali ni katika desturi zao tu Saudia
Kwani nchi zote za kiarabu wanawake wanaendesha na walikuwa wanaendesha siku zote
Ni maamuzi ya Wasaudi ila halihusiani kabisa na dini
Na wanawake kutokwenda shule huko Afghanistan??
 
Sheikh ila kuzuru na kuhudhuria mazishi ni mambo mawili tofauti kabisa ingawa hadithi nyingi zinasema marufuku, kukatazwa kwao ni kwa sababu wako emotionally zaidi na kilia sana kwa sauti ndio haitakiwi
Na Mungu anajua zaidi
Sababu ya kipuuzi kabisa hii. Kuna wanaume pia ambao wako emotional mbona wanakuja makaburini??
 
Sababu ya kipuuzi kabisa hii. Kuna wanaume pia ambao wako emotional mbona wanakuja makaburini??
Wapo wanaume wa hivyo ndio wakimuona hata Raisi wanagaragara na kuonyesha hisia
Wewe una dini yako fuata dini yako tu mengine yaache
 
Tabia za ujahiliyyah (zama za ujinga kabla Uislam haujarejea Arabia) ndio miongoni mwa mambo yanayofanya wanawake wasiruhusiwe kusindikiza jeneza wakati wakuzika.

Wanawake ni viumbe wa emotion...wanaomboleza, wanajigaragaza chini,kuchana nguo, kujipiga,kujidhuru na hata kumlaumu Mungu kwa kufiwa na mpendwa wao.

Mambo ambayo yanamuongezea hali ngumu maiti. Hivyo Mtume hakupendezwa na jambo hili la wanawake kufuatilia jeneza ingawa halijawekwa kuwa uharam wake si wa kutiliwa mkazo sana.

Unaweza kusikiliza haya mawaidha, sheikh ameelezea

View: https://m.youtube.com/watch?v=12ff8a3pbA0
 
Hii ni.mojawapo ya Heshima kubwa waliopewa wanawake wa kiislamu,wanaume ndio wafanye kazi ya kuzika na kuwalisha na kuwapatia.
Vipi kama mwanamke haitaki hiyo heshima? Anaruhusiwa kwenda kuzika?
 
Sawa lakini mambo mengine unajiongeza. Africa South of Sahara, kuna joto hado 40 C sometimes , mtu anakwambia uvae burqa, nawe unatii kuwa ni taratiibu... Inabidi hapo ujiongeze
Unaelewa vilivyo dhana ya dini kweli ndugu?

Unazungumzia vazi!! Vazi kitu gani mbele ya dini (imani) ya mtu!!? Kibwetere alichoma watu Uganda kwasababu ya imani za dini. Kuna mchungaji wa Kenya kashawishi na kaaminisha watu waache kula hadi kifo sababu ya imani za dini.

West Africa akina mama wanadhalilishwa utu wao na wachungaji wa madhehebu sababu ya imani za dini.

Dini sio jambo la mzaha , sio jambo jepesi Wala rahisi.

Ni aidha unaamua kufuata taratibu za dini husika au unaachana na hiyo dini, vinginevyo utaingia kwenye migogoro isiyo ya lazima.

Hakuna utaratibu wa kuuliza maswali kanisani Wala msikitini . Ni mwendo wa kukubali tu Yale yanayoelezwa na aidha mchungaji / padre/ imamu/ sheikh na kadhalika
 
sasa unafura nini? hayo ya Kibwetele et al, ndiyo nasisitiza kutojiongeza huko!

My main point ni kuwa pamoja na IMANI ya dini, jiongeze . Dini ni IMANI na IMANI is defined as "kuamini kuwa kitu fulani ni cha kweli, kweli kabisa BILA USHAHIDI WA KISAYANSI AU USHAHIDI WOWOTE!
 
Naunga mkono wanawake kutokwenda makaburini. Wanakimbilia magari na kujaa, wanaume wanapata nafas kidogo. Wakifika n kukaa tu juu ya makaburini na kusogoa.

Kifupi hawafanyi kazi.

Nashauri wafiwa tu waende
 
Unaelewa vilivyo dhana ya dini kweli ndugu?

Unazungumzia vazi!! Vazi kitu gani mbele ya dini (imani) ya mtu!!? Kibwetere alichoma watu Uganda kwasababu ya imani za dini. Kuna mchungaji wa Kenya kashawishi na kaaminisha watu waache kula hadi kifo sababu ya imani za dini.

West Africa akina mama wanadhalilishwa utu wao na wachungaji wa madhehebu sababu ya imani za dini.

Dini sio jambo la mzaha , sio jambo jepesi Wala rahisi.

Ni aidha unaamua kufuata taratibu za dini husika au unaachana na hiyo dini, vinginevyo utaingia kwenye migogoro isiyo ya lazima.

Hakuna utaratibu wa kuuliza maswali kanisani Wala msikitini . Ni mwendo wa kukubali tu Yale yanayoelezwa na aidha mchungaji / padre/ imamu/ sheikh na kadhalika
Ndo udikteta wenyewe huo...na uzuri watu wengi washasanuka
 
Back
Top Bottom