Kwanini wanawake Waislamu hawaruhusiwi kwenda makaburini kuzika wapendwa wao?

Kwanini wanawake Waislamu hawaruhusiwi kwenda makaburini kuzika wapendwa wao?

Wamevaa vibandiko vichwani lakini hata dini hawaijui halafu wanajinasibu mitaani kama wanazuoni.
Uislam haukatazi mwanamke kwenda kuzika, bali imeshauriea tu. Swala hilo la mwanamke kwenda au kutikwenda kuzika limepelekea hata wanazuoni kugawanyika.
Sababu zilizopelekea ishauriwe wanawake kutokwenda kuzika ni;

1. Wanawake wapo too emotional na hawawezi kujizuia, hivyo wakati wa kushuhudia safari ya mwishi ya mpendwa wao hupelekea wengi kushindwa kujizuia na kuanza kulia kwa sauti na hivyo kuingilia na kuvuruga ibada.

2. Kwa maumbile yao, na kama ilivyozoeleka uwepo wa wanawake makaburini husababisha fitna (majaribu/ushawishi), hivyo kupelekea msoma mawaiza/dua pamoja na wengine badala ya kujikita kwenye kumuomba marehemu kwenye safari yake ya mwisho, badala yake fitna ya wanawake inaweza ikapelekea wahame katika dua na mawaiza na kuanza kufikiria mengine.

Hivyo, ieleweke kwamba swala la wanawake kutotakiwa kwenda kuzika siyoamri, yaani siyo katazo bali ni ushauri tu.
Kah! kwamba mtoa dua anaweza acha kutoa dua akaanza kuwaza namna wanawake wengine walivyofungasha?? sasa hapo tatizo si litakuwa la msoma dua mwenyewe?
 
Hiyo hali inawakumbuka wanawake wa kiislamu peke yao?
maana wanawake wa kikristu huhudhiria mazishi na hakuna hicho unachokisema.
Mkuu,hapa issue sio kwamba yanatakiwa majibu, hapa hata ukitoa majibu,hawawezi kukubaliana na majibu,au hata hayo majibu watayakashifu pia,

Ngoja nikujibu halafu utaona respond yao.

Wanawake ni dhaifu ukiwalinganisha na Wanaume,
Wanawake wana shindwa kujizuwia na huathirika na huzuni.

Hulia kwa kuomboleza kwa sauti jambo ambalo kwenye uislamu hairuhusiwi kulia kwa kuomboleza kwa sauti kwenye msiba.

Au wanaweza wakapoteza fahamu huko Makaburini, wakaanguka na kuzimia, au akaanguka na mavazi yake yakamtoka coz kwenye uislamu maziko ni ibada, wakati wa kuzika Makaburini ndio wakati wa machungu zaidi kwa wafiwa,sasa Wanawake ni wachache wa subira.
 
Taratibu na Sheria mama kwenye dini yeyote Ile iwe Islam au Ukristo huwa ni Maandiko matakatifu (QURAN & BIBLIA)

Ndiyo maana binafsi ninataka kufahamu kama Quran Ina maelekezo yeyote kuhusu hili suala la Wanawake kutokwenda makaburini wakati wa mazishi!

Kama hakuna andiko na zinatumika kanuni na Sheria tu (Utamaduni) basi nadhani itakuwa Batili kwasababu Sheria na kanuni huweza kubadilishwa na yeyote lakini Msaafu haubadiliki!
Umechangia kiungwana sana, kiwerevu na kisomi sana.
Kongole kwa mchango mzuri.
 
Porojo tupu za watu hizo, hakuna hata aya moja ya Qur'an iliyokataza.
Nani anayeifahamu Qur'an zaidi ya Mtume? je aliwakusanya wanawake akaambia wajumuike kwenda kuzika makaburini pamoja na wanaume? Je haitoshi sisi kuiga kile alichokifanya mtume? .... kumbuka pale ilipobidi kuhimiza mwanamke kuhudhuria jambo ambalo kikawaida halikuoneka na ulazima basi alifanya hivo, mfano pale alipomwambia mwanawe Fatima kuwepo na kutazama pale kichinjo chake kilipokuwa kinachinjwa kwa ajili ya Eid Al-Adha. Pia mtume huyohuyo (SAW) alihimiza wanawake kuhudhuria kwenye viwanja vya Eid hata kama hawapo katika state ya tohara.

Ikiwa unao ushahidi wa kuwa mtume alishiriki kuzika pamoja na wanakawe basi naomba nielimishe na mimi.
 
Hiyo fitna ya wanawake ndio ikoje mkuu. Uwepo wa wanawake mahala kwenye wanaume unaitwa fitna au una tafsiri ya ndani zaidi. Fitna si ni jambo baya
Nilipokuwa nafuatilia wanazuoni walilitaja kabisa kwa kiarabu kuwa ni 'fitna' halafu wakaweka brachets na kuandika 'temptation'
 
Nani anayeifahamu Qur'an zaidi ya Mtume? je aliwakusanya wanawake akaambia wajumuike kwenda kuzika makaburini pamoja na wanaume? Je haitoshi sisi kuiga kile alichokifanya mtume? .... kumbuka pale ilipobidi kuhimiza mwanamke kuhudhuria jambo ambalo kikawaida halikuoneka na ulazima basi alifanya hivo, mfano pale alipomwambia mwanawe Fatima kuwepo na kutazama pale kichinjo chake kilipokuwa kinachinjwa kwa ajili ya Eid Al-Adha. Pia mtume huyohuyo (SAW) alihimiza wanawake kuhudhuria kwenye viwanja vya Eid hata kama hawapo katika state ya tohara.

Ikiwa unao ushahidi wa kuwa mtume alishiriki kuzika pamoja na wanakawe basi naomba nielimishe na mimi.
Mtume hakuwahi kuendesha gari, mbona nyie mnaendesha sasa hivi? Si kila ambacho mtume hakufanya ni kosa
 
Nani anayeifahamu Qur'an zaidi ya Mtume? je aliwakusanya wanawake akaambia wajumuike kwenda kuzika makaburini pamoja na wanaume? Je haitoshi sisi kuiga kile alichokifanya mtume? .... kumbuka pale ilipobidi kuhimiza mwanamke kuhudhuria jambo ambalo kikawaida halikuoneka na ulazima basi alifanya hivo, mfano pale alipomwambia mwanawe Fatima kuwepo na kutazama pale kichinjo chake kilipokuwa kinachinjwa kwa ajili ya Eid Al-Adha. Pia mtume huyohuyo (SAW) alihimiza wanawake kuhudhuria kwenye viwanja vya Eid hata kama hawapo katika state ya tohara.

Ikiwa unao ushahidi wa kuwa mtume alishiriki kuzika pamoja na wanakawe basi naomba nielimishe na mimi.
 
Hakuna jibu la maana, sawa na kuuliza ni kwa nini kanisa Katoliki lisiruhusu wanawake kuwa mapadri.
 
Kama ni hivyo ni swala la kuwambia tu hatutaki kulialia na kujitupa.. au kama hutoweza kujizui hisia zako basi usifike màkaburini!!
Hii nakumbuka kuna msiba wa kiislam ulitokea mtaan....shee bila kupepesa macho aliwaambia wakina mama hatutaki kusikia mtu akilia,mwili wa marehemu ulikuwa unatoka ndan kwenda makuburini.
 
Sio utamaduni wa Dini ya Kiislam kuchangamana wanaume na wanawake. Full stop

Waislam Wana Dini yao na wengine Wana Dini zao, kila mtu afuate Dini yake.
 
Mambo ya imani huwa yanabeba hisia kali na mihemko mikubwa......ili kupata jamii yenye msawazo ni vyema kila mtu kubakia kwake kiimani na kiushiriki........

Tujifunze kuheshimu mipaka yetu ya kiimani kwenye jamii

Mambo yanayohusu imani ambayo wewe sio mshiriki ni vyema kuachana nayo na kujikita kwenye imani yako ili uvune mema yanayotokana kwenye imani yako......

Kuchokonoa chokonoa imani za watu kunaweza kuleta jambo moja baya sana kwenye jamii yetu.........
 
Hapa nimeitwa naona watu wanabishana sifahamu mada ni nini?

Mada ni maziko ya mtu fulani au ni vipi?

Kama ni maziko ya mtu fulani, tuelewe kuwa maziko ni faragha ya warithi, wao ndiyo wenye kuamua nani akazike na nani asizike.

Hata wanaume wanapokwenda makaburini, siyo wanaoruhusiwa kuingia ndani ya kaburi kumzika marehemu. NI faragha ya warithi na maharim zake.

Kiislam kuanzia kuosha maiti, kuiaga maiti na kuizika maiti ni faragha ya wahusika niliowataja hapo juu tu.

Wengine wote, iwe mwanamke au mwanamme wanaruhusiwa kwenye mkusanyiko, wa kuanzia kusalia na kuisindikiza maiti.

haya, swali lenu ni nini haswa?
Al maktoum njoo huku
 
Back
Top Bottom