Kwanini wanawake Waislamu hawaruhusiwi kwenda makaburini kuzika wapendwa wao?

Kwanini wanawake Waislamu hawaruhusiwi kwenda makaburini kuzika wapendwa wao?

Kwa nini wanawake Waislamu hawaruhusiwi kushiriki shughuli muhimu za maziko kama hata kwenda makaburini kuzika wapendwa wao ?
View attachment 3118314

Nitie neno hapa:

Mazikoni ni mahala pa huzuni kubwa.

Ndiyo maana kuliko staarabika maziko ni jambo la kifamilia na privacy yao hupewa nafasi yake.

Inasikitisha kwa Dida privacy yake na hata ya familia imeshindwa kupewa nafasi yake.

Apumzike kwa amani Dida - mja wake Mola.
 
Msingi WA Sheria katika uislamu ni
1. Qur an
2. Hadith
Kwahiyo kuna mambo ambayo yapo direct kwenye Qur an na mengine yanapatikana kwenye Hadith.
Pia kumbuka katika kila muktadha wa elimu kuna wabobovu wa elimu husika.Kwa mtazamo wangu si busara kuita wasomi wabobovu watoa porojo kwani katika Kila nyanja ya elimu Kuna watu walijitoa kutoa ufafanuzi wa elimu husika.
Hadith haiwezi kukataza kitu au kuruhusu kitu ambacho Qur'an imekikataza au kukiruhusu.
5_44.gif

44. Hakika Sisi tuliteremsha Taurati yenye uwongofu na nuru, ambayo kwayo Manabii walio nyenyekea kiislamu, na wachamngu, na wanazuoni, waliwahukumu Mayahudi; kwani walikabidhiwa kukihifadhi Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Nao wakawa ni mashahidi juu yake. Basi msiwaogope watu, bali niogopeni Mimi. Wala msibadilishe Aya zangu kwa thamani chache. Na wasio hukumu kwa aliyo teremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri. 44
 
Perfect, uko sahihi kabisa! BUT, Utamaduni wa kuwafanya women objects of men, objects of mens sex pleasure. SIYO SAWA UTAMADUNI HUO!
 
Dunia imebadilika kweli
 

Attachments

  • FB_IMG_17280968450633406.jpg
    FB_IMG_17280968450633406.jpg
    445.5 KB · Views: 2
Huyo Sheikh alimaindi baada ya majirani wa Dida kugoma kwenda kuagia makaburini wakisema kwamba kwa nini hajapelekwa nyumbani kwake alikokuwa anaishi akaagwe kwa mara ya mwisho?

Walichofanya hao majirani, na wao wakaenda huko huko makaburini, wanaume kwa wanawake.

Sasa kama wao waliweka ratiba ya kuagia iwe makaburini walitegemea mashoga zake wasiende makaburini kwenda kuaga?

Badala ya kubwata na wanawake walioenda makaburini kuaga, wangedili na walioandaa ratiba ya mazishi.

View attachment 3118369

View attachment 3118370

Inasikitisha sana.

Yoda kwa mtaji huu uzi wako umekosa thamani ya kwanini umemhusisha Dida (RIP) kwenye kadhia hii ya maziko yake?

Ungehitaji kujua kwa nini wanawake waislam hawaendi msibani hilo si ungeuliza bayana tu? Kulikoni kuihusisha Hilo maziko ya Dida ambayo kumbe yana vionjo vya infringement ya privacy ya maziko yake kuihusisha familia?

Ama kwa hakika, kumbe uzi huu ulipaswa kushia hapa. Kongole Kingsmann kwa uthabiti wa hoja yako.

"Kwamba mleta mada Kwa kujua au vinginevyo umeendeleza kuchochea infringement ya privacy ya mja huyu, na Mod wako kimya?"

Huku si ndiyo kulidogosha jukwaa hili kuwa kama yale mengine?

Ushauri wa bure Mod kulikoni kuwa accomplice? Kulikoni marehemu asiachwe kupumzika?

Kulikoni mada ya wanawake na maziko isitenganishwe na sokomoko mazikoni kwa marehemu huyu?.
 
Kama ndivyo watakuwa wanakosea sana mkuu!
Ukweli Quran haijakataza bali ni tafsiri mbovu tu. Kwa uchache iko hivi:-

1. Je, wanawake wanaweza kuhudhuria mazishi katika Uislamu?

Ndio, wanawake wanaweza kuhudhuria mazishi katika Uislamu; Japo inaruhusiwa kwa ujumla, wanawake wanapaswa kuzingatia unyenyekevu, kuepuka hisia kupita kiasi kama vile kulia kwa sauti, na kuvaa mavazi yenye staha. Baadhi ya wanazuoni wanakataza wanawake kuhudhuria mazishi endapo kuna hatari ya tabia zisizofaa, lakini sio marufuku kabisa.

2. Hukumu ya Kiislamu kuhusu Wanawake Kutembelea Makaburi

Hukumu ya Kiislamu kuhusu wanawake kutembelea makaburi inathibitishwa na hadithi mbalimbali na inaonyesha kuwa haijakatazwa. Hadithi zifuatazo zinatoa ushahidi kwa maoni haya:

a) Tukio la Mtume Muhammad na Mwanamke Anayelia
Mtume Muhammad (PBUH) alikutana na mwanamke aliyekuwa akilia kwenye makaburi. Badala ya kumkataza asitembelee kaburi, alimshauri kumcha Allah na kuwa na subira. Kwa tukio hilo inaashiria kwamba wanawake wanaruhusiwa kutembelea makaburi.


b)Swali la Aisha Kuhusu Kutembelea Makaburi

Aisha , mke wa Mtume, alimuuliza kuhusu kutembelea makaburi. Mtume alimfundisha asome dua ya amani na rehema kwa waliozikwa makaburini. Mwongozo huu unadokeza kwamba wanawake wanaruhusiwa kutembelea makaburi na kuomba dua kwa ajili ya wafu.
 
Kwani wanawake walienda makaburini

Ova
 
Inasikitisha sana.

Yoda kwa mtaji huu uzi wako umekosa thamani ya kwanini umemhusisha Dida (RIP) kwenye kadhia hii ya maziko yake?

Ungehitaji kujua kwa nini wanawake waislam hawaendi msibani hilo si ungeuliza bayana tu? Kulikoni kuihusisha Hilo maziko ya Dida ambayo kumbe yana vionjo vya infringement ya privacy ya maziko yake kuihusisha familia?

Ama kwa hakika, kumbe uzi huu ulipaswa kushia hapa. Kongole Kingsmann kwa uthabiti wa hoja yako.

"Kwamba mleta mada Kwa kujua au vinginevyo umeendeleza kuchochea infringement ya privacy ya mja huyu, na Mod wako kimya?"

Huku si ndiyo kulidogosha jukwaa hili kuwa kama yale mengine?

Ushauri wa bure Mod kulikoni kuwa accomplice? Kulikoni marehemu asiachwe kupumzika?

Kulikoni mada ya wanawake na maziko isitenganishwe na sokomoko mazikoni kwa marehemu huyu?.
Dida ni public figure huko Daslam,
 
Dida ni public figure huko Daslam,

Kwa hiyo kumbe hoja yako ni ipi?

"Dida public figure au kwanini wanawake waislam kutokwenda mazikoni?"

Si uwe wazi tu ndugu?

Kulikoni kuingiza familia kwenye vita vyenu binafsi?

Issue kama dini si unavua gloves zikachapwa kavu kavu tu ikibidi, bila kuumiza familia zisizohusika tena zilizopo kwenye majonzi?

Au huoni hivyo ndugu?
 
Mkuu hakuna ambaye aheshimu dini ya mtu!

Nadhani ni vizuri kama unamajibu uyaweke hapa ili na wengine tujifunze!

Ukiangalia wanawake wengi wa Kiislam huwa wanalalamika sana kunyimwa fursa za kuwasindikiza Wapendwa wao makaburini ili nao wakashuhudie wakizikwa!,sidhani kama ni vibaya!

Ndiyo maana jamaa alitaka kujua ni kwanini Dini ya Islam hairuhusu mwanamke kwenda Makaburini?

Je,Aya za maandiko ya Quran zinasemaje kuhusu hilo?,Je unaweza ukaweka hapa Aya kadhaa ili tusome sote tujifunze?
Kimsingi mwanamke amekatazwa kuzika. Makatazo haya ni makatazo ya ukaraha si makatazo ya uharamu wa kupata dhambi ijapokuwa makuruhu (ukaraha) unaweza kukupelekea ukapata dhambi.

Makatazo hayo si ya kusisitizwa yaani wamekatazwa pasi na kukaziwa kwamba wakifanya hivyo wanapata dhambi. Ndiyo maana wanawazuoni wa kiislamu wanasema ni makatazo ya kujitakasa au kujiepusha na uwezekano wa kutokea mambo ya haramu ndani yake.

Wote tunafahamu jinsi ya wanawake wanavyoombeleza. Uislamu haukukatazi kulia au kuhuzunika hata kusema kwa hakika ni pigo kubwa haukatazwi.

Ila ile kusema nitaishije, umeniacha na nani na aina kama hizo jinsi wanawake wanavyolia au kukumbatia kaburi wakati wanazika na kuanza kusema jamani mume wangu umeniacha mpweke umeaniacha na nani n.k ....

Hii ndiyo hali ya mwanamke! Uislamu huko haukuruhusu! Haukutaki utamke maneno hayo au kufanya hivyo! Kulia kwa namna hiyo ni kama kumkosoa Mungu na kwa imani ya Kiislamu ni makosa.

Waislamu tunasema kazi yake mola haina makosa. Sisi sote ni wa Mungu na kwake tutarejeshwa. Unachotakiwa kumuomba Mungu akupatie uvumilivu na akupatie mwangalizi au aliye kama yeye au aliyembora kuliko yeye na kumkumbuka marehemu kwa kumuombea dua kwa yale aliyoteleza kama binadamu Mungu amsamehe.

Kimsingi huu makatazo yao ni ya kujitakasa. Kujiepusha na mambo ambayo yanaweza kutokea uharamu ndani yake na kukupelekea kupata madhambi.

Mwanamke kwenda kuzuru makaburi ameruhusiwa.

Simba mundu Yoda
 
Ina wahusu wavaa kobazi hii mwanamke kama sio mvaa kobazi haikuhusu makaburi sio mali yenu watu waende kuzika bila kujali jinsia

Kwa hiyo Yoda ameleta hii ni hoja ya kidini siyo kumhusu Dida?

Uthibitisho tafadhali ikikupendeza ili tupige hatua kama watu wazima.

Au nasema uongo ndugu?
 
Mbona hamna Pope mwanamke na waislamu wala hawaulizi?Huu ni ubaguzi au ni utaratibu wa Kanisa la Roman Catholic?
Kama walikuwepo huko nyuma kwanini walisitisha?
Tuheshimu imani za watu.Na imani haziwezi kuwa za aina moja.
 
Wanawake katika uislam hawaruhusiwi kwenda kuzika ila wanaruhusiwa kwenda kutembelea makaburi.

Hawaruhusiwi kwenda kuzika kwasababu wengi wao huwa wanalia kupitiliza na hata wakiona maiti anafukiwa huwazidishia uchungu na mara nyingine wanaongea maneno yanayopelekea kukufuru mfano "Mungu kwanini umemchukua"

Kuzika katika uislam ni ibada na kila ibada ina utaratibu wake hivyo utaratibu wa ibada hii ya kuzika ni mwanamke kubaki nyumbani akimuombea dua maiti wake na mwanaume ni kwenda makaburini kuzika.
 
Mkuu hakuna ambaye aheshimu dini ya mtu!

Nadhani ni vizuri kama unamajibu uyaweke hapa ili na wengine tujifunze!

Ukiangalia wanawake wengi wa Kiislam huwa wanalalamika sana kunyimwa fursa za kuwasindikiza Wapendwa wao makaburini ili nao wakashuhudie wakizikwa!,sidhani kama ni vibaya!

Ndiyo maana jamaa alitaka kujua ni kwanini Dini ya Islam hairuhusu mwanamke kwenda Makaburini?

Je,Aya za maandiko ya Quran zinasemaje kuhusu hilo?,Je unaweza ukaweka hapa Aya kadhaa ili tusome sote tujifunze?

Mkuu nimependa hoja yako japo kuna ka ukakasi kwenye maandishi.

Nipendekeze u edit haya makosa ya wazi ikikupendeza:

1. "Aheshimu" - hii haipo vizuri kama ilivyotumika pale. Labda ingerekebishwa?

2. Kama ni nia njema kama ni kufanya mjadala kiungwana, unaonaje huu mjadala usiwe na cha kufanya na Dida au familia yake?

a) Hudhani ni busara marehemu akaachwa kupumzika na familia kumwomboleza, privacy yao ikiheshimiwa?

b) Huoni kutokea hapo mjadala ungekuwa na mashiko kwamba waungwana wanajadiliana?

Au nasema uongo ndugu yangu?
 
Back
Top Bottom