Kwanini wanawake Waislamu hawaruhusiwi kwenda makaburini kuzika wapendwa wao?

Kah! kwamba mtoa dua anaweza acha kutoa dua akaanza kuwaza namna wanawake wengine walivyofungasha?? sasa hapo tatizo si litakuwa la msoma dua mwenyewe?
 
Hiyo hali inawakumbuka wanawake wa kiislamu peke yao?
maana wanawake wa kikristu huhudhiria mazishi na hakuna hicho unachokisema.
 
Umechangia kiungwana sana, kiwerevu na kisomi sana.
Kongole kwa mchango mzuri.
 
Porojo tupu za watu hizo, hakuna hata aya moja ya Qur'an iliyokataza.
Nani anayeifahamu Qur'an zaidi ya Mtume? je aliwakusanya wanawake akaambia wajumuike kwenda kuzika makaburini pamoja na wanaume? Je haitoshi sisi kuiga kile alichokifanya mtume? .... kumbuka pale ilipobidi kuhimiza mwanamke kuhudhuria jambo ambalo kikawaida halikuoneka na ulazima basi alifanya hivo, mfano pale alipomwambia mwanawe Fatima kuwepo na kutazama pale kichinjo chake kilipokuwa kinachinjwa kwa ajili ya Eid Al-Adha. Pia mtume huyohuyo (SAW) alihimiza wanawake kuhudhuria kwenye viwanja vya Eid hata kama hawapo katika state ya tohara.

Ikiwa unao ushahidi wa kuwa mtume alishiriki kuzika pamoja na wanakawe basi naomba nielimishe na mimi.
 
Hiyo fitna ya wanawake ndio ikoje mkuu. Uwepo wa wanawake mahala kwenye wanaume unaitwa fitna au una tafsiri ya ndani zaidi. Fitna si ni jambo baya
Nilipokuwa nafuatilia wanazuoni walilitaja kabisa kwa kiarabu kuwa ni 'fitna' halafu wakaweka brachets na kuandika 'temptation'
 
Mtume hakuwahi kuendesha gari, mbona nyie mnaendesha sasa hivi? Si kila ambacho mtume hakufanya ni kosa
 
 
Hakuna jibu la maana, sawa na kuuliza ni kwa nini kanisa Katoliki lisiruhusu wanawake kuwa mapadri.
 
Kama ni hivyo ni swala la kuwambia tu hatutaki kulialia na kujitupa.. au kama hutoweza kujizui hisia zako basi usifike màkaburini!!
Hii nakumbuka kuna msiba wa kiislam ulitokea mtaan....shee bila kupepesa macho aliwaambia wakina mama hatutaki kusikia mtu akilia,mwili wa marehemu ulikuwa unatoka ndan kwenda makuburini.
 
Sio utamaduni wa Dini ya Kiislam kuchangamana wanaume na wanawake. Full stop

Waislam Wana Dini yao na wengine Wana Dini zao, kila mtu afuate Dini yake.
 
Mambo ya imani huwa yanabeba hisia kali na mihemko mikubwa......ili kupata jamii yenye msawazo ni vyema kila mtu kubakia kwake kiimani na kiushiriki........

Tujifunze kuheshimu mipaka yetu ya kiimani kwenye jamii

Mambo yanayohusu imani ambayo wewe sio mshiriki ni vyema kuachana nayo na kujikita kwenye imani yako ili uvune mema yanayotokana kwenye imani yako......

Kuchokonoa chokonoa imani za watu kunaweza kuleta jambo moja baya sana kwenye jamii yetu.........
 
Al maktoum njoo huku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…