Kwanini wanawake Waislamu hawaruhusiwi kwenda makaburini kuzika wapendwa wao?

Katika uislamu wanawake hawaruhusiwi kuhudhuria mazishi makaburini kwa kuwa wanawake wako very emotional hivyo wanaweza kuvuruga shughuli nzima ya maziko...........

Vile vile uislamu unaamini mchanganyiko wa wanaume na wanawake ambao una uharamu Kati Yao unaweza kuzalisha fitna na watu kuangukia kwenye mambo mengine yasiohusiana na mazishi( temptation)

Uislamu unaamini kuwa muunganiko usio wa kisheria baina ya mwanamke na mwanamume unaweza kuzalisha mambo ya haramu hivyo basi lazima kuwe na mipaka baina ya watu hao wawili.........


lakini wanaweza kutembelea kaburi la mpendwa wao baada ya maziko........

(nipo tayari kusahihishwa kama nimeteleza au kibinadamu nimejisahau)
 

Tatizo ni kuwa wajinga wakuelewe vipi?"
 
Waislamu wana mambo ya mzaha kweli. Mbona kwenye mabasi, sokoni, madukani, mabuchani, shopping mall tunakutana nao tu??

Hii ndiyo tofauti ya elimu ya kisasa na elimu ya madrassa
 
Ni utaratibu wa sheria ya kiislamu kuwa maziko yafanywe na wanaume, wanawake watamswalia maiti nyumbani na kutulia kisha wanaume wataenda kushughulika na mazishi huu ni utaratibu wa dini yetu na maslahi yake ni makubwa na hayaonekani isipokuwa kwa wenye imani na maarifa, vyema tuheshimiane na kila mtu afuate anachokiamini.

Retired Naona nikujibie hapa hakuna dini imekuja kumuinua mwanamke ikaushinda uislamu hata siku mtume swala na amani ziwe juu yake alipokua anafanya hijjah ya kuaga alituusia kuwatendea wema wanawake, soma historia utajua mwanamke alikuwa kiumbe wa kutwezwa kiasi gani mpaka ilipokuja sheria hii tukufu.
 
Waislamu wana mambo ya mzaha kweli. Mbona kwenye mabasi, sokoni, madukani, mabuchani, shopping mall tunakutana nao tu??

Hii ndiyo tofauti ya elimu ya kisasa na elimu ya madrassa
Hujanielewa, nisome tena tafadhali!
 
Watu waheshimu imani za wengine. Mnaotaka kujua kwanini wanawake hawaruhusiwi makaburini kwenye uislamu jiungeni na uislamu ili mjifunze.
Hakuna Swala la kuheshimu au kutoheshimu, hapa inahitajika elimu na iwe based kutoka kwenye Qur'an.

Mkuu Arsis tunaomba tupe darsa hapa binadamu hana mipaka ya kujifunza
 
Waislamu Wameanza lini kuaga maiti?
 
Sasa kwanini kwenye uislamu ni wanawake tu ndo wasiruhusiwe?? Kuna aya inayokataza hili au ni mtazamo tu?
 
Mungu hana kwanini, Dini imekataza unatakiwa kutii
Leta kifungu cha Quran kinachokataza hilo.

Kuna nchi moja huko Asia inaitwa Afghanistan nayo imekataza wanawake wasiende shule. Nao wanadai Quran imekataza.

Kila Waislam wakitaka kumfanya mwanamke ni bidhaa husingizia Quran. Acheni uwongo. Leta hilo katazo hapa kwa kunukuu Quran
 
Kuna Mashaka kwenye hadithi ndio sababu hata Mashia kuna hadithi wanazipinga ila kwenye Qur'an hakuna utata.
 
sasa magari yana husika vip na Uislamu?muwe mnaelewa kuwa Saudi Arabia sio utawala wa kiislamu ule, ni tawala za watu tu walizo jiamulia
 
Ni kmtamaduni ya kiarabu tu.
Arab Ancient doctrine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…