Kwanini wanawake Waislamu hawaruhusiwi kwenda makaburini kuzika wapendwa wao?

Kwanini wanawake Waislamu hawaruhusiwi kwenda makaburini kuzika wapendwa wao?

Katika uislamu wanawake hawaruhusiwi kuhudhuria mazishi makaburini kwa kuwa wanawake wako very emotional hivyo wanaweza kuvuruga shughuli nzima ya maziko...........

Vile vile uislamu unaamini mchanganyiko wa wanaume na wanawake ambao una uharamu Kati Yao unaweza kuzalisha fitna na watu kuangukia kwenye mambo mengine yasiohusiana na mazishi( temptation)

Uislamu unaamini kuwa muunganiko usio wa kisheria baina ya mwanamke na mwanamume unaweza kuzalisha mambo ya haramu hivyo basi lazima kuwe na mipaka baina ya watu hao wawili.........


lakini wanaweza kutembelea kaburi la mpendwa wao baada ya maziko........

(nipo tayari kusahihishwa kama nimeteleza au kibinadamu nimejisahau)
 
Mambo ya imani huwa yanabeba hisia kali na mihemko mikubwa......ili kupata jamii yenye msawazo ni vyema kila mtu kubakia kwake kiimani na kiushiriki........

Tujifunze kuheshimu mipaka yetu ya kiimani kwenye jamii

Mambo yanayohusu imani ambayo wewe sio mshiriki ni vyema kuachana nayo na kujikita kwenye imani yako ili uvune mema yanayotokana kwenye imani yako......

Kuchokonoa chokonoa imani za watu kunaweza kuleta jambo moja baya sana kwenye jamii yetu.........

Tatizo ni kuwa wajinga wakuelewe vipi?"
 
Kimsingi mwanamke amekatazwa kuzika. Makatazo haya ni makatazo ya ukaraha si makatazo ya uharamu wa kupata dhambi ijapokuwa makuruhu (ukaraha) unaweza kukupelekea ukapata dhambi.

Makatazo hayo si ya kusisitizwa yaani wamekatazwa pasi na kukaziwa kwamba wakifanya hivyo wanapata dhambi. Ndiyo maana wanawazuoni wa kiislamu wanasema ni makatazo ya kujitakasa au kujiepusha na uwezekano wa kutokea mambo ya haramu ndani yake.

Wote tunafahamu jinsi ya wanawake wanavyoombeleza. Uislamu haukukatazi kulia au kuhuzunika hata kusema kwa hakika ni pigo kubwa haukatazwi.

Ila ile kusema nitaishije, umeniacha na nani na aina kama hizo jinsi wanawake wanavyolia au kukumbatia kaburi wakati wanazika na kuanza kusema jamani mume wangu umeniacha mpweke umeaniacha na nani n.k ....

Hii ndiyo hali ya mwanamke! Uislamu huko haukuruhusu! Haukutaki utamke maneno hayo au kufanya hivyo! Kulia kwa namna hiyo ni kama kumkosoa Mungu na kwa imani ya Kiislamu ni makosa.

Waislamu tunasema kazi yake mola haina makosa. Sisi sote ni wa Mungu na kwake tutarejeshwa. Unachotakiwa kumuomba Mungu akupatie uvumilivu na akupatie mwangalizi au aliye kama yeye au aliyembora kuliko yeye na kumkumbuka marehemu kwa kumuombea dua kwa yale aliyoteleza kama binadamu Mungu amsamehe.

Kimsingi huu makatazo yao ni ya kujitakasa. Kujiepusha na mambo ambayo yanaweza kutokea uharamu ndani yake na kukupelekea kupata madhambi.

Mwanamke kwenda kuzuru makaburi ameruhusiwa.

Simba mundu Yoda
Waislamu wana mambo ya mzaha kweli. Mbona kwenye mabasi, sokoni, madukani, mabuchani, shopping mall tunakutana nao tu??

Hii ndiyo tofauti ya elimu ya kisasa na elimu ya madrassa
 
Ni utaratibu wa sheria ya kiislamu kuwa maziko yafanywe na wanaume, wanawake watamswalia maiti nyumbani na kutulia kisha wanaume wataenda kushughulika na mazishi huu ni utaratibu wa dini yetu na maslahi yake ni makubwa na hayaonekani isipokuwa kwa wenye imani na maarifa, vyema tuheshimiane na kila mtu afuate anachokiamini.

Retired Naona nikujibie hapa hakuna dini imekuja kumuinua mwanamke ikaushinda uislamu hata siku mtume swala na amani ziwe juu yake alipokua anafanya hijjah ya kuaga alituusia kuwatendea wema wanawake, soma historia utajua mwanamke alikuwa kiumbe wa kutwezwa kiasi gani mpaka ilipokuja sheria hii tukufu.
 
Waislamu wana mambo ya mzaha kweli. Mbona kwenye mabasi, sokoni, madukani, mabuchani, shopping mall tunakutana nao tu??

Hii ndiyo tofauti ya elimu ya kisasa na elimu ya madrassa
Hujanielewa, nisome tena tafadhali!
 
Watu waheshimu imani za wengine. Mnaotaka kujua kwanini wanawake hawaruhusiwi makaburini kwenye uislamu jiungeni na uislamu ili mjifunze.
Hakuna Swala la kuheshimu au kutoheshimu, hapa inahitajika elimu na iwe based kutoka kwenye Qur'an.

Mkuu Arsis tunaomba tupe darsa hapa binadamu hana mipaka ya kujifunza
 
Huyo Sheikh alimaindi baada ya majirani wa Dida kugoma kwenda kuagia makaburini wakisema kwamba kwa nini hajapelekwa nyumbani kwake alikokuwa anaishi akaagwe kwa mara ya mwisho?

Walichofanya hao majirani, na wao wakaenda huko huko makaburini, wanaume kwa wanawake.

Sasa kama wao waliweka ratiba ya kuagia iwe makaburini walitegemea mashoga zake wasiende makaburini kwenda kuaga?

Badala ya kubwata na wanawake walioenda makaburini kuaga, wangedili na walioandaa ratiba ya mazishi.

View attachment 3118369

View attachment 3118370
Waislamu Wameanza lini kuaga maiti?
 
Hapa nimeitwa naona watu wanabishana sifahamu mada ni nini?

Mada ni maziko ya mtu fulani au ni vipi?

Kama ni maziko ya mtu fulani, tuelewe kuwa maziko ni faragha ya warithi, wao ndiyo wenye kuamua nani akazike na nani asizike.

Hata wanaume wanapokwenda makaburini, siyo wanaoruhusiwa kuingia ndani ya kaburi kumzika marehemu. NI faragha ya warithi na maharim zake.

Kiislam kuanzia kuosha maiti, kuiaga maiti na kuizika maiti ni faragha ya wahusika niliowataja hapo juu tu.

Wengine wote, iwe mwanamke au mwanamme wanaruhusiwa kwenye mkusanyiko, wa kuanzia kusalia na kuisindikiza maiti.

haya, swali lenu ni nini haswa?
Sasa kwanini kwenye uislamu ni wanawake tu ndo wasiruhusiwe?? Kuna aya inayokataza hili au ni mtazamo tu?
 
Mungu hana kwanini, Dini imekataza unatakiwa kutii
Leta kifungu cha Quran kinachokataza hilo.

Kuna nchi moja huko Asia inaitwa Afghanistan nayo imekataza wanawake wasiende shule. Nao wanadai Quran imekataza.

Kila Waislam wakitaka kumfanya mwanamke ni bidhaa husingizia Quran. Acheni uwongo. Leta hilo katazo hapa kwa kunukuu Quran
 
Msingi WA Sheria katika uislamu ni
1. Qur an
2. Hadith
Kwahiyo kuna mambo ambayo yapo direct kwenye Qur an na mengine yanapatikana kwenye Hadith.
Pia kumbuka katika kila muktadha wa elimu kuna wabobovu wa elimu husika.Kwa mtazamo wangu si busara kuita wasomi wabobovu watoa porojo kwani katika Kila nyanja ya elimu Kuna watu walijitoa kutoa ufafanuzi wa elimu husika.
Kuna Mashaka kwenye hadithi ndio sababu hata Mashia kuna hadithi wanazipinga ila kwenye Qur'an hakuna utata.
 
Ni tafsiri mbovu tu za dini yenyewe. Huko Saudi Arabia hadi mwaka 2015 wanawake walikuwa hawaruhusiwi kuendesha magari.

Ila alipokuja mwana wa mfalme Mohamed Bin Salaman akaona kuwa ni UDWANZI wala Quran haijawazuia.

Akaruhusu waanze kuendesha kuanzi mwaka 2017 hadi leo.

Waislamu acheni kukariri, kuweni extrovert
sasa magari yana husika vip na Uislamu?muwe mnaelewa kuwa Saudi Arabia sio utawala wa kiislamu ule, ni tawala za watu tu walizo jiamulia
 
Ni kmtamaduni ya kiarabu tu.
Arab Ancient doctrine
 
Back
Top Bottom