Habari jioni wanajamvi na hongera kwa busy Monday.
Kwa ufupi nipo njia panda hivyo ningependa kupata ushauri wenu ndugu zangu. Story iko hivi, nina familia ya mke na watoto 4. Mtoto wa kwanza Form 6, form 4, form 1 na wa mwisho Std 5. Sasa mwanzoni mwa corona pandemic nikajikuta nimepata ka mchepuko ka single mother na kwa sababu ya work from home nikajikuta tumekuwa karibu sana. Tukaendelea kuwa pamoja na nikampa support ya maisha ya kila siku maana kazi yake ilivurugwa sana na corona.
Mpaka sasa tupo wote huu mwaka wa 2 na kinachoendelea sasa ni madai kwamba age yake imesonga sana na angependa apate angalau mtoto wa pili kabla ya kufikisha 40yrs maana sasa yuko na 38yrs. Demand ya mtoto wa pili imeendelea kuongezeka siku adi siku lakini mimi baada ya kutafakari nikamwambia kwamba sipo tayari kwa sasa maana yeye kwa sasa hana kazi so gharama za maisha yake na mtoto wake ni juu yangu 100% kwa sababu baada ya corona ofisi yao ilifunga operations Tanzania. Lakini yeye anasema mimi nipo selfish maana mimi tayari nina watoto 4 na yeye ana kamoja tu so ni kwanini nisimsaidie akapata katoto ka pili ??
Baada ya kuzozana kwa muda wa miezi kama 2 sasa amekuja na pendekezo kwamba nimruhusu ajiunge kwenye dating site/app inaitwa Bumble ambayo aliisoma kwenye app ya Mange ili apate mwanaume wa kudate naye na kama akifanikiwa kumpata basi waoane wazae mtoto maana anaona natural process ya kupata mtu wa kuzaa naye itachukua muda na atajikuta amevuka 40 bila mtoto wa pili. Mwanaume alozaa naye mtoto wa kwanza hawana mawasiliano tena na mimi ndo namsaidia kumtunza na kumsomesha mtoto wake ( yupo darasa la 2 sasa)
Baada ya kuja na mapendekezo ya kujiunga na dating site nikakasirika nikamwambia mimi na yeye then basi (though ki ukweli roho ilikuwa inauma kukaacha maana yaliyomo yamo saaana.) Yeye anasema kama sitaki kuzaa naye yafaa nimruhusu kwenda dating wakati tuko wote ili akipata mwanaume ndo tuagane maana nikimuacha hatokuwa na wakumtunza. Akaenda mbali zaidi anasema nikimuacha kabla ya kumpata mwanaume mwingine anakuja nyumbani kwangu kufanya fujo.
Naombeni ushauri wanajamvi
Asanteni sana.