1. Sipendi tabia ya ugomvi / kupigana hasa hadharani.
2. Wanawake hawajui kupigana na muda mwingi wanakuwa wanavutana nywele au kusukumana au mmoja kumkalia / kumlalia mwenzake. Hii hupelekea kuvutana nguo ambazo kama ni gauni au sketi au khanga basi rahisi kutoka/ kuvuka hatimaye mtu kubaki mtupu/ wazi. Badala ya kurusha ngumi au teke kama wanaume wanavopigana wanawake wao mikono yao na miguu haina asili hiyo au balance hivo huishia kuvutana na kufinyana au kung'atana.
3. Asili ya mavazi ya kike ni gauni sketi na chupi ni laini, rahisi kukatika kwenye purukushani kumbuka hata hereni mkufu pete ndala hukatika pia kama sehemu ya ugomvi sio nguo tuu. Na wenye mawigi au nywele za kushonea hapa wanaipata maana wanawake wanapigana kwa kuviziana amshike wapi ili amuweze mpunzani wake.
4. Wako wanawake wagomvi ambao hujiandaa na ugomvi, mfano huyo mwenye kaptura ya jeans hapo hadi uje kuivua labda uwe ushampiga na amezirai. Viatu alivobvaa pia (raba) si rahisi kutoka.
5. Wengi hutumia hiyo kama silaha sababu hawajui kupigana, kawaida binadamu tumeumbwa na aibu hivo akifanikiwa kumtoa nguo ya juu au ya chini basi yule aliyevuliwa nguo atakosa nguvu na kuhangaika namna ya kujisetiri hatimaye atadundwa.
Halafu gomvi za wanawake huwa watazamaji hawaziamulii sababu wanataka kuona nyuchi au chupi na sindiria, ila gomvi za kiume zinaamuliwaga haraka.
Hawa utasema wamepagawa na mapepo ya kupigana.... halafu ukiuliza chanzo cha ugomvi ndo utachoka..... kanichukulia bwaba wangu, kwenye pati alinisonya, amenitangazia mie malaya na blaah blaah blaah kibao.
Hapo ni kuvutana nywele, kuangushana chini na kuburuzana.
Nachukua sana kupigana, sana sana...... bora niitwe muoga kuliko mjuaji au mbabe wa kuoneshana mabavu. Sababu mwili wangu hauna spea, jicho langu likitoka au nikipata kovu au jeraha ambalo halitatoka milele.... ntajichukia. Nipate hayo kwa ajali ingine ila sio kupigana.
Kasinde Mtata kwenye Mahaba tuu.