Kwanini wanawake wengi wanabweteka kwenye mahusiano akishakuzoea

Kwanini wanawake wengi wanabweteka kwenye mahusiano akishakuzoea

Habari wanajf

Ukijaribu kuwasikiliza wanawake wengi unakuta wanasema wanapenda wanaume wapole na ambao hawana mambo mengi sio kwamba hawapati wanaume dizaini lahasha lakini wakiwashawapata vituko haviishi. Nina bro wangu hivi mpole, na si mtu wa mademu alipata demu mapenzi yalikuwa moto na kila nikikaa nae lazima anipe feedback ya mahusiano yake baada ya miezi miwili kupita changamoto zikaanza ni baada ya huyo manzi kupata kazi unaambiwa bro akimtumia message saa 10 jioni anajibiwa saa 7 usiku hapo akiwa tayari kashauchapa usingizi, muda mwingine hajibiwi message, akipiga simu sometime haipokelewi na hatafutwi.


Ana muda wa miezi 6 hajapewa mbususu sababu anaambiwa uchovu, stress n.k sasa baada ya kuona kuwa ni kama yeye Ndio anajipendeza sana basi akaamua asiwe anamtafuta kabisa ajikite kuwa busy na mambo yake ikapita almost mwezi mmoja Yule manzi akaanza kumpigia simu bro cos ameshakasirishwa alikuwa hazipokei Ila baada ya siku nne kupita Ndio akapokea angalia huyu demu alivyo mjinga akaanza kumpa lawama bro umeanza umalaya nini uko mbona simu zangu upokei na unitafuti bro akamkatia simu.

Siku hiyo hiyo huyo manzi akatimba mpaka ghetto la bro, bro wangu anakawaida ya kuacha sehemu ufunguo kabla hajasepa basi huyo manzi anajua na wengi wanajua Ndio demu wa bro aliingia ghetto unaambiwa ghetto lilifanyiwa usafi kitu ambacho hakuwahi kufanya hapo kabla na akapika na chakula na kuna zawadi kaleta nyingi kwa bro.

Tangu siku hiyo mapenzi yalikuwa si ya mchezo

NB: kwanini wanawake wengi wanaendekeza hizi tabia anajiboost mpaka aubostiwe tofauti na hapo wanabweteka akishajua au kuhisi una mchepuko Ndio anachangamka kwanini isiwe ni desturi yake ya kuboresha mahusiano yake bila kuchangamshwa? Mbona kuna wanaume wametulia tu hawana mambo mengi lakini still wanasumbuliwa na mahusiano na wenza wao shida ni nini?
Wanawake wanapenda heka heka kwenye mahusiano na hii inatupa sana shida wanaume ambao tuna haiba ya upole na tabia ya kupuuzia drama zao, wanawake wanatuchukulia kama wanaume dhaifu fulani hivi
 
NO Mimi napenda nifanye nice kwa upande wangu kama mwanaume sitaki kuwa harsh ili ukisepa ukose Cha kuniongelea vibaya, ila ukilinga ujue Mimi sijali kabisaa, mwanamke ukimdekeza dekeza hovyo ndo utapoteza ela na muda
Nimekupata mwamba
 
Bora huyo demu alijirudi mwenyewe na kuamua kurudi kwa jamaa.Wengine ingekuwa ndo imetoka hiyo humuoni tena eti kwa Sababu anajimudu kiuchumi
 
Back
Top Bottom