Kwanini wanyama hawafanyi mapenzi kinyume na maumbile?

ungejibu swali langu, usiwe mwoga kujibu maswali kwa lengo maalum, napata mashaka pengine wewe ni victim wa haka kamchezo.
 

Ahsante kwa mawazo yako unayodhania kwamba ndiyo yako sahihi. Nilitegemea umesoma hii thread na kuona ilikusudia nini kumbe wapi? nilikuwa nahangaika na mtu ambaye tayari ana majibu yake kichwani, hapo unategemea nini? kama una muda unaweza ukaandika thread yenye kutaka reasons ya kwanini wanafanya hivyo sawa? lengo la hii thread ilikuwa katika mfumo wa swali ukiwataka wote wanaohusika na tendo hilo wajihoji na kuona kama kile wanachofanya ni salama? Je, watufarahi wakiona wake/dada/mama na binti zao wakifanyiwa hivyo kama wao wanavyowafanyia wengine? na akishajioji na kuona nafsi yake inamsuta katika hilo analolifanya, then achukue hatua yeye mwenyewe.

Sikuwa nimetaka sababu za kwanini wao wanashiriki huu mchezo. Na hata ukisoma thread yangu vizuri utagundua kwamba kuna baadhi ya sababu zimejitokeza hasa katika mfumo wa maswali. Hivyo, samahani kama hilo unalotaka liandikwe halijajitokeza hapa. Wewe si ulitegemea waje hapa waanze kukuambia sababu zao za kushiriki huo mchezo ndipo uridhike?

Ni mara ngapi baadhi ya wakina dada/mama wamelalamika humu JF wakionyesha jinsi wanavyoteseka na hiyo hali ambayo mara nyingi wanaume ndiyo wameonekana kuwa chanzo? wengine waliangukia huko kwasababu ya tamaa za kazi, wengine tamaa za pesa, wengine wamelazimishwa na waume/BF zao, wengine wamefanywa hivyo kwa kushawishiwa na kuwekewa vileo kwenye vinywaji, wengine wamebakwa, n.k . Wewe ni shuhuda zipi unazotegemea hao watu wakuletee hapa ndipo uone validity ya hii thread?

Nani kakuambia kwamba kuna hukumu hapa? nani katoa hukumu? mbona unakimbilia hitimisho kumbe hata thread hukuelewa lengo lake ni nini? Hivi unajua kwamba kuna mada nyingi sana unazoweza kuibua katika hii thread? je unategemea yote yanayohusiana na hii thread yajadiliwe ndipo uridhike? Ni bora ujifunze kwamba kunaweza kuwa na mada nyingi lkn mtoa thread yeye anatoa kile alichokikusudia, kwani anafanya hivyo kwasababu anazoona kwamba leo kwenye hii mada amabyo ni pana sana niiandikie katika kipengele fulani ili iwe focused katika eneo fulani tu.

Hapo kwenye Red, do you really expect me to give them a resonable environment for their acts? Do you really think that they don't know what they ared doing? and motives for their acts? forgive me for that, because these people they know for sure what they are doing and my focus/target was to remind them to have a break and think more on the impacts to victims before they act positively or negatively to anal sex.
 

naomba nikufahamishe tu kwamba mimi siyo mnafiki, hivyo siwezi kuwa sehemu ya mchezo halafu nipoteze muda wangu mwingi toka jana kufanya kazi ya kinafiki. kama ulivyoniomba hapo kwamba nisikuhusishe kwenye kundi lolote hapo juu, nilitegemea na wewe kuwa mstaarabu hivyo hivyo.

Kuhusu maswali yako;
1. haikuwa lengo la thread hii kutaka kujua hili tatizo lilianza lini na litaisha lini au lilianzishwa na nani au wapi, kwani hata bila kuuliza hayo maswali bado hakuondoi lengo la hii thread. Kama ungependa kujua hayo pia unakaribishwa kuanzisha thread nyingine ili tujadili chanzo na wapi ilikoanzia na nani mwanzilishi wa huu mchezo.
2. Sikuwa nahitaji mtu yeyote atoe ushuhuda hapa, kwani tayari hapa JF kuna watu wengi tu wameshawahi kuleta jinsi wanavyoumia kwa kitendo hicho walichofanyiwa na baadhi ya watu ktk mazingira na sababu mbalimbali.
3. Kukuemea kiaina-ndiyo (hasa ilikuwa ni kuwapa muda wahusika wajiulize maswali kadhaa kama hicho wanachoshiriki ni salama, then wafanye maamuzi).
4. wadhani watajiona wajinga na kughairi? - sidhani, isipokuwa naamini kwamba walio na utu na uchungu na familia zao wanaweza kughairi na kuachana na hiyo tabia, kwani ni suala la maamuzi ya mtu binafsi na hilo linawezekana; na hili ndilo lengo hasa ya thread hii.
5. Dini zinawakataza? - ndiyo naamini kwamba dini zote zinakataza hata dini ya asili. Kwani ni mambo mangapi ambayo dini hairuhusu lkn bado waumini wanaendelea kufanya? ni mengi tu ; lkn nilitaka hawa watu wapate muda na kujihoji kuona kama wanachofanya ni sawa hata kiimani?
6. Unadhani hawaulizwi maswali magumu juu ya nafsi zao? - yawezekana wanajiuliza au hawajiulizi maswali magumu, lkn kikubwa hapa ni kushiriki kwao katika hilo tendo. Kama watakuwa wanajiuliza maswali magumu na kufanya maamuzi sahihi nadhani tatizo lisingekuwa kubwa kama lilivyo leo. Na kama wanajiuliza, siyo vibaya kwani hata mimi nimewaongezea tu wigo wa maswali ya kujiuliza.

Ahsante.
 
Yote unayozungmza ni ukweli mtupu.
Naamini unasononeka sana unapoyaona yanayotokea na ni wajibu wako kukemea na huna haja kujihami kupita kiasi.
Nakushauri utafute katika dini tofauti na pia wataalamu wa saikolojia ili uweze kujua HULKA ya binadamu.
Pia utaweza kujua kwa nini kuna TOBA na pia utaweza kuelewa kitu kinachoitwa KUSUTWA NA DHAMIRA (quilty consciuosness).
Binadamu ana mapungufu mengi mno na hata pale atakapokuwa amejitahidi kumkaribia Mungu bado kuna hitilafu.
Mambo ya ngono ni mengi,kuna wanaopata furaha kwa kuumiza,kwa kuingilia watoto,kwa kuvutiwa na watu wa jinsia na hata kwa kuvaa nguo kama chupi ambazo sio za jinsia yako.
Binadamu ana mapungufu mengi na ndo maana kuna TOBA,otherwise Mungu angeangamiza tu.
 

Telo, inasomeka hautaki mambo ya msingi yajadiliwe, hatuwezi kuwa na mjadala unaofaa bila kuwa na malengo mazuri, ieleweke kuwa wewe ni binadamu kama walivyo wengine usijifanyizie utukufu machoni pako, muda haujawahi kupotea hata mara moja chini ya jua!
kumbe daktari anapokuuliza historia ya kuumwa kwako huwa anakupotezea muda sio? naam kwani lengo lako si kuandikiwa dawa? ya nini akuulize umeanza kuhara lini! unahara majimaji ya rangi gani, maumivu ya mgongo ulianza kuyasikia lini, umeshawahi kupata tiba popote kuhusu tatizo hili n.k,
Tuliza kichwa, bado naamini kuwa maswali yangu ni ya msingi kwenye mjadala huu ulioanzisha, uyajibu tafadhali, lau kama hujui majibu yake kwa ufasaha wana-jf watajadili. oh siyo lengo la mjadala, hii sasa itakuwa re-examination! tuwe na cross examination too.
wakati tunasubiri majibu mazuri ya maswali naliyokuuliza mapema, tafadhali tutajie neno kwa kabila ya kwenu lenye tafsiri ya "kufira"
nasubiri majibu hapa hapa jf.
 
asante sana ,sio sahihi kabisa siku nyingine uwe una summarize kidogo
 
hahahahaha.ukitaka ujue unafiki wa watu subiri siku ikitolewa thrid ya tigo.comment kibaoooooo
 
Nakubaliana nawe,siyo kitu kizuri,among many other things binadamu tunafanya..
 

Maelezo mengi sana, just try to be precise, unakosea sana when you write with emotions. . .the wise keep their emotions aside when discussing critical matters. . .hata kama una mtu wa karibu yako amefanyiwa kitendo kama hicho, just keep your emotions aside ndipo unatoa mada, mada huwa zinaboa sana when watu wakichangia with emotions, sorry to say that.ninaposoma comment zako zote natambua una mzigo wa emotions katika mada hii. Tulia panga hoja taratibu watu watakuelewa. . .
 
Naamin ushapata majib!

Kwn ilikuwa kama research

Hvyo andika findings ktk new thread,

Eleza kwa nin watu wanafanya huo mchezo na sababu zao kwa urefu na upana!
 
kabla sijasema chochote nikuulize maswali kadhaa.....
1. umewahi kushiliki hicho kitendo majuto ni mjukuu?
2. umewaza nini mpaka ukajitoa muanga kusema haya?
3. umeoa au kuolewa?
4. unamtoto wa kike au wakiume?
5. umewahi kusikia sodoma na gomora?

nitatoa ushirikiani baada ya majibu send even in private.
 
well, it is a free world... ; and judging by what is happening in our society today, it looks like this tiGo thing is going to be around for a very very long time...
 

Karibu uendelee na mjadala.
 

Inaelekea kuna incident imekudrive kuuliza swali hili, it just did not come out of the blue. Seems like it have hurted you so much. . .i do understand the way you are feeling about this.a piece of advice, if you open more clues might come out. Seems like you are holding something just more than this thread.
 
Jamani naona badala ya kujadili hoja sasa tunahitaji taarifa binafsi za mtoa hoja. Nisichokielewa hapa ni kwamba hili siyo tatizo katika jamii yetu na watu hawaumii kwa matendo haya? Ni kweli kwamba tunafurahia haya matendo yanapotokea kwa ndugu na jamaa zetu. Mimi binafsi nampongeza mtoa hoja kwasababu hili ni tatizo katika jamii japo kuna watu hawako tayari kukubaliana na hilo. Labda nimshauri tu mtoa mada kwamba anapaswa kujua kwamba hili ni tatizo kubwa sana na wengi sana wanaathirika lakni kuna watu hasa wanaume wanaufurahia sana, hivyo asitegemee kupata msaada wa kimawazo kutoka kwa watu kama hao.

Lakini kuna watu kama mimi ambao tumefurahia hii thread kwasababu inatupa changamoto katika suala zima la kimahusiano na kijamii kwa kujaribu kuangalia au kufikiri ni kwa jinsi gani kuna watu wameumizwa sana na hii tabia ya kufanya mapenzi kupitia hiyo sehemu.
 
Don Mangi na Jogi;

Sijui unachohitaji ni kitu gani zaidi? kama maswali yako nimekujibu kutokana na nafasi yangu. Lkn inaonekana hauko tayari kupokea hayo majibu uliyohitaji toka kwangu. Naanza kuamini kwamba tayari una majibu yako kinywani na hivyo unachohitaji ni majibu kulingana na uelewa wako. Hilo inaweza ikawa vigumu kupata, kwasababu watu wanatofautiana ktk kutoa majibu. Swali inaweza ikawa 1 lkn majibu yakawa tofauti, kwasababu tu ni swali la maelezo na si la A,B, au C.

Sasa nikuulize wewe, nini position yako katika jambo hili? kwani umekuwa wa kulalamika tu lkn hakuna sehemu yoyote ambapo umejaribu kuelezea jambo linalojadiliwa hapa ukionyesha ni kwa namna gani wewe unalichukulia hili swala. Je, kwako ni tatizo au siyo tatizo? kwasababu kila wakati umekuwa wa kuuliza tu maswali ambapo kila unapojibiwa inaonekana haujaridhika na hivyo unaishia kutoa maneno mengi ya kebehi tu kwangu badala ya kuelekeza hoja zako kwenye tatizo. Naona umekuwa na visingizio vingi sana katika jambo hili. Kumbuka, toka mwanzo nilifahamu kwamba watu kama wewe watatokea tu kwenye thread, ambao kazi kulaumu lkn hawasemi nini position yao. Naomba pia ukae ukijua hili kwamba lengo langu ilikuwa ni watu wengi sana kusoma hii thread ili wale watakaoguswa na waweze kufanya mabadiliko katika mfumo wa mahusiano yao. Haikuwa lengo langu kutaka watu waje hapa na kutoa ushuhuda wao, na badala yake nilitaka watu wasome hapa na wale watakaoguswa waweze kubadili mfumo wa maisha yao.

Hivyo basi, ni jukumu lako langu, wewe, yeye na yule ambaye sehemu ya jamii kuona kama ni tatizo na kila mtu kufanya sehemu yake ili tuweze kuwasaidia wale wanaoumizwa na matendo haya.

Nafikiri utakuwa umenielewa. Naomba niishie hapo kuhusu maoni na maswali yako. Na nikuombe tu na wewe uweze kuchangia hii thread kama unaona una chochote kitakachoweza kusaidia jamii katika hili tatizo. Jamii inahitaji mchango wako ktk hili na si maswali ambayo hatahivyo hauko tayari kuyatolea majibu ya namna gani unafikiri majibu yawe.
 
Nakupongeza sana Telo kwa kupost mada kama hii, hizi ndio mada zinazotakiwa kujadiliwa ili kubadilisha fikra potofu na mtazamo wa hasi wa jamii ya sasa. Tatizo linakuja pale malumbano ya yanapochkua nafasi katika kujadili mada, sidhani kama hapa si mahali sahihi pa kunyoosheana vidole au kuonyeshana umwamba wa kudefend mada. Ushauri wangu ni kwamba kila mchangiaji achukue nafasi yake, aisome mada kwa umakini, atafakari kwa kina, aingalie nafasi yake katika kuijenga jamii,kama ni mwana dini aingalie imani ya dini yake inamhitaji afanye nini, kisha atoe suluhisho la mada na ushauri wake. Swala la kwamba unafanya au hufanyi, we ni msafi au sio msafi lisichukue nafasi katika kuchangia bali ni usahihi wa tendo hili. Mengine yajadiliwe kwa muda wake utapofika maana jamii yetu inajengwa kwa mambo mengi.Wako wanaofanya hili mengine hawafanyi na wako wasiofanya hili lakini mengine wanafanya kwa hiyo kila moja lijadiliwe kwa wakati wake ili tuijenge jamii yetu pale inapoonekana kupotea kwa mambo yasiyokua ya lazima na yanayoepukika.

SASA Nachangia mada kwa kusema kufanya ngono sehemu ya haja kubwa sio sahihi :
-Kiimani(kwa dini yoyote). Kupotea kwa hofu ya Mungu na Kumkosoa Mungu katika uumbaji wake, Kuacha miili yetu itutawale badala ya kumwacha Mungu atutawale, kupotea kabisa kwa hofu ya Mungu na kuruhusu imani za kishetani kimatendo itawale dunia.
-Kiafya (si kwa wanawake pekee hata kwa wanaume). Kwa wanawake ni kuzaa kwa taabu,kuvuja vinyesi wakati wowote,kutokwa na harufu mbaya n.k, kwa wanaume ni kuziba kwa mirija ya mkojo na uzazi, kupungua kwa nguvu za kiume n.k
-Kiakili/saikolojia(wanaofanya wanahisi ni sawa na ni muhimu na wapo tayari kwa gharama yoyote hata ikiwezekana kubaka, kufanya/kufanyiwa hivi pindi hisia zao zinapowatawala na kuacha kwao ni tabu/ugonjwa hapa hawana tofauti na wanaotumia madawa ya kulevya).
Mwisho naomba kuwashauri wale wanaofanya haya watafute sehemu tulivu,wakae chini wajiangalie wenyewe bila kuruhusu hisia zao ziwatawale, na wajihukumu wenyewe, kisha wachukue hatua, wawe wajumbe wema katika kuishuhudia jamii yetu na wajasiri wa kuijenga jamii yetu katika mambo yenye msingi na maedeleo.
Hayo ni machaache tu niliojitahidi kuchangia, naomba wanajamii wengine waongezee bila kuweka ubinafsi(selfishness) bali wajali utu wao na busara zaidi itumike. Tukumbuke kwamba mabadiliko hayatokei ghafla bali taratibu na kwa mpangilio bila kusababisha madhara.
Ahsanteni
 
nakubaliana na wewe bishanga, si vizuri kujaji watu sana.

Lakini ulipotaja kanisa katoliki umenivutia kuchangia hapa.

Je waufahamu msiamamo wa kanisa katika hili??
Nakumbuka katika mafundisho ya kanisa katoliki dhambi zimegawanywa katika makundi mawili, dhambi za kawaida na na dhambi za mauti.

Katika dhambi za mauti hii ni included kwa hiyo kwa kanisa hii ni kati ya makatazo makuu.

Padri anavyosema maneno yale naamini, ni kusihi sadaka ile ipokelewe pamoja na udhaifi wake wa kibinadamu.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…