uungwana classic
JF-Expert Member
- Jun 9, 2014
- 2,324
- 2,085
Kama ni hivyo kweli pongezNafsi yangu haijafurahi wala kusikitika....kwa kifupi maisha yao hayanigusi tena kwa chochote, nasonga mbele na yangu!
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama ni hivyo kweli pongezNafsi yangu haijafurahi wala kusikitika....kwa kifupi maisha yao hayanigusi tena kwa chochote, nasonga mbele na yangu!
Bora useme mwenyewe maana mimi nimemwambia ila hakunielewa kabisa [emoji4] [emoji4]Ahahahaaaaaa jamani, mbona unanimaliza kiasi hicho rafiki yangu?
Mimi na kipenzi chako ni majirani tuu hakuna kingine
Asante. Hivyo ndivyo ilivyo! Sina haja ya kuhangaika nao kwa lolote wala chochote kwani najua ipo siku Mungu atanipa kilicho bora
Ndo hivyo kisicho riziki hakilikiAsante. Hivyo ndivyo ilivyo! Sina haja ya kuhangaika nao kwa lolote wala chochote kwani najua ipo siku Mungu atanipa kilicho bora
Haswaaa....!
Asante sana
Asante! Ila umenichekesha[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Hali yangu iko vyema, niko imara kama chuma. Nashukuru kwa ushauri wako ila sina haja ya kuharakia haya maisha tena. Lililopangwa na Mola litatimia kwa muda muafaka!Hali yako ikoje baada ya hilo tukio
Je bado hujampata mwenzi wako kama bado nakushauri usipoteze muda nenda fasta
Sent using Jamii Forums mobile app
Itachukua muda nafsi zenu kupata pumziko hasa wewe na jamaa maana nyundo aliotumia kukuadhibia ni hiyohiyo imetumika kumuadhibu.Asante! Ila umenichekesha[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Rafiki mimi ni binadamu wala sio malaika hivyo nina madhambi yangu pia, sipingani nawe katika hilo. Lengo la kushare hapa sio kwamba namhukumu la hasha bali nimeshare ili watu wajifunze kitu kutokana na mkasa huu kwani najua mimi sio wa kwanza kutendwa hivi wala sio wa mwisho.Kumbe wewe ni She? Nimekuja kugundua mwishoni kabisa. Nilichokiona una hulka ya kiume huenda pia ungemtesa kijana wawatu angekuoa.
Namaanisha kwamba:-
Wadada wengi/Wakaka wengi hujiaminisha kuwa eti X-wake aliyemuacha angemuoa yeye angekuwa na maisha mazuri kuliko anavyoishi na huyo aliye naye. Hii haina tofauti na kupiga ramli.
Maisha hubadilika kulingana na mazingira usishangae wewe ndiyo ungezaa mwarabu badala ya huyo mwingine.
Chakusema hapo ni pole na mapenzi ya Mungu yatimizwe siyo kujiosha kwa chupa ya asali ili hali ukijua wadudu wakitua watang'ang'ania mgongoni mwako na hatimaye kufa na kuleta harufu mbaya mwilini mwako. (Oga hakuna mkamilifu).
naomba summary tafadhali ThadTulipendana sana, tukapanga mipango kedekede ya maisha yetu ya baadae na kuahidiana kila aina ya ahadi tamu tamu lakini yote hayo hakuyajali na kwa kuwa moyo wa mtu ni kichaka sikuweza kung'amua lolote mpaka siku ile ambayo sitakaa niisahau maishani mwangu!
Kama ilivyoada aliniaga kwa mabusu moto moto, nilijua ni moja kati ya safari zake za kibiashara, nilimwombea kila la heri huko aendako. Na safari ikaanza na kuniacha mwenye majonzi kwani nilijua nitamkosa kwa muda usiopungua wiki moja, kilichoniumiza zaidi ni kujua fika kuwa baada ya masaa yapatayo 12 nisingeweza kuwasiliana naye hata kwa simu maana aliniambia kuwa huko aendako ni maporini kusiko na network. Nilimwamini pasipo shaka. Naam baada ya masaa 12 sikuweza tena kumpata kwenye simu zake zote ila haikunipa shida kwani nililijua hilo.
Siku tatu baada ya kuondoka kwake, mida ya jioni nilishtushwa sana baada ya kupigiwa simu na rafiki yangu mmoja na kunipa pole kabla ya kuniuliza imekuwaje? Badala ya kumjibu nilimwuliza kwa wasiwasi mwingi, ananipa pole ya nini? Na imekuwaje nini? Jibu lake ndilo lilinifanya mpaka leo nisiisahau hiyo siku! Alicheka kwa kejeli kisha akanijibu ina maana hujui kama fulani(alitajajina la mpenzi wangu aliyesafiri siku 3 zilizopita) kanilipia mahali leo na kesho tunaenda kuandikisha ndoa kanisani? Sikusikia kingine alichokiongea bali nakumbuka mwangwi wa maneno yale yaliendelea kujirudia masikioni mwangu kwa masaa kadhaa kabla ya kulala (sina uhakika kama nililala au nilizimia)
Nilipoamka nilikuta simu ikiwa chini huku kioo cha simu kikiwa kimevunjika na betri ya simu imedondokea upande wake, nikajua kuwa baada ya taarifa zile nilidondosha simu pasipo kujijua.
Baada ya wiki moja mpenzi wangu alirudi kama alivyoniahidi akiwa na zawadi lukuki, nilizipokea na nilijaribu kuficha hali niliyokuwa nayo lakini aligundua kuwa sikuwa sawa akaniuliza nina tatizo gani nikamwambia ninaumwa na nimeshauriwa na daktari kupumzika muda mwingi. Alinionea huruma akataka alale kwangu ila nikamkatalia, nikamwambia nahitaji kuwa mwenyewe ili niweze kutumia muda mwingi kwa kulala. Alinielewa na akaondoka.
Sikuonana naye tena kwani kesho yake asubuhi na mapema nilisafiri kwenda mkoa mwingine na nilibadilisha namba ya simu. Tulionana tena siku ya harusi yake na rafiki yangu kipenzi, ilinibidi kwenda kanisani kushuhudia ndoa yao kama nilivyoshauriwa na mwanasaikolojia wangu. Aliniambia hiyo itanisaidia kuamini kuwa yule jamaa si wangu tena. Wakati wanatoka kanisani baada ya ndoa, nilihakikisha maharusi hao tunaonana ana kwa ana, kisha nikatokomea.
Haikuwa rahisi hata kidogo kuendelea na maisha ila kwa msaada wa ushauri wa mwanasaikolojia niliweza kuendelea na maisha japo ilinibidi kubadilisha mtindo wangu wa maisha.
Miezi 6 baada ya ndoa nilipata taarifa kuwa wanandoa wale walipata mtoto wa kiume, ila mtoto mwenyewe ni mwarabu wakati wazazi wake ni Wandengereko wenzangu. Hahahahaaaaa....nacheka kama mazuri mie. Wambea ikawa kutwa kucha wananilitea habari, ile ndoa si ndoa tena bali imegeuka ndoano baada ya kuzaliwa mtoto wa kiarabu. Nikasema pole yao, wavumilie tu maana kitanda hakizai haramu.
Juzi jamaa kanifuata anasema nimsamehe, yalopita si ndwele tugange yajayo. Ameachana na mkewe (rafiki yangu) kama niko tayari tukafunge ndoa ya bomani, niwe mkewe. Ametambua kuwa alifanya kosa kubwa sana kuniacha. Nimemwambia nilishamsamehe kitambo sina kinyongo nae hata kidogo ila "PEMA NI PEMA USIPOPEMA, UKIPEMA SIO PEMA TENA"!
Bora umeona jirani
[emoji23] [emoji23] [emoji23]Bora umeona jirani
inabidi nikubali tu sina namna ingine, nikimuuliza mwenyewe anasema ni majirani tu ila karoho kanauma kwa ndaniAhahahaaaaaa jamani, mbona unanimaliza kiasi hicho rafiki yangu?
Mimi na kipenzi chako ni majirani tuu hakuna kingine
Yaan umemjibu kistarabu hadi nimezidi kukupenda. Yaan watu wenye mioyo kama yako(majibu yenye staha)ni wachache sana.Rafiki mimi ni binadamu wala sio malaika hivyo nina madhambi yangu pia, sipingani nawe katika hilo. Lengo la kushare hapa sio kwamba namhukumu la hasha bali nimeshare ili watu wajifunze kitu kutokana na mkasa huu kwani najua mimi sio wa kwanza kutendwa hivi wala sio wa mwisho.
By the way, kwanini umesema nina hulka za kiume?