Nakubalina na point ambazo amezileta hapa Boflo...naamini kuwa, kama lengo ni kuwaasa watu waache kula/kuliwa 'Tigo', basi approach nzuri si KUWATISHA. Hakuna kitu chenye athari kama sigara, na maDaktari wanazijua fika athari zake...lakini wengi tu ni wavutaji mahiri. Kutisha haijawahi kuwa approach ya kutatua tatizo fulani.
Kula 'Tigo' hakusababishi njia ya mkojo ya mwanaume kuziba, haijawa documented ikiwa supported na research ya kutosha. Kuna kipindi wagonjwa wa mikojo waliokuwa wanawekewa mipira (urine catheter) walikuwa wananyanyapaliwa kuwa ni wala Tigo, na wameziba sasa wanazibuliwa...hili liliwahi kumkuta hata mzee wetu Kawawa (RIP). Katika kazi ya ngu wa uDaktari, niliwahi fanya kitengo cha upasuaji njia ya mkojo (Urology) kwa miezi mi4, na nilipata cases nyingi sana (close to thousands) za kuziba mikojo...hata mmoja, haijawahi kuwa ni sababu ya kula Tigo, mara karibu zote ni kuvimba kwa tezi Ng'ombe (Prostate).
Kula Tigo yes kunapanua 'anal canal' kwa kulegeza internal na external sphincters, wakati mwingine hata kusababisha rectal prolapse...lakini hii ni very long term effect ya anal sex, na hata hivyo haitokea kwa watu wote. La sivyo kina sir Elton John wangekuwa wanavaa pampers tu. Internal na external sphincters largely zinaundwa na misuli na elastic tissue ambayo inaweza kurelax na hivyo kuweza tanuka na kuruhusu kuingiliwa bila maumivu wala damage, kisha ikarudi katika haliyake ya kawaida na kubana kwa nguvu tu baada ya huo mchezo. Inatokea mara chache kwa walioingiliwa bila kuandaliwa sphincter ikawa stretched na wwakati mwingine kuwa torn, ndio huuma na kama damage ni persistent..basi muathirika akikohoa au kupiga chafya (increase intra-abdominal pressure), basi choo haweza mtoka..lakini nayo haitokei kwa wengi.
Wanawake watakuwa mashahidi wangu...kwamba wanawake wengi, kama sio wote, hunya (hutoa choo) katika process ya kujifungua. ujue kuwa process nzima ya labor take hours (kato ya masaa 4 - 8 kutegemeana na kuwa ni uzao wa kwanza au ulishazaa kabla), na process nyingine za mwili zikiendelea including kutengeneza choo. Mara nyingi wakati kitangulizi cha hasa kichwa kikishaingia kwenye bony pelvis, kinasugua against rectum and pelvis, hivyo kusababisha mkuno kwenye rectum...hii humpelekea mwanamke kujisikia kunya hata kama hana choo. Hii inatokea kwa wanawake wengi, almost wote wakati wa kujifungua...na kama huyo mwanamke ana choo kwenye rectum, lazima tu atatoa choo (hii inatokea kwa wanawake wengi kama sio wote)! Haisababishwi na kutoa Tigo. nimeshazalisha wanawake wengi sana katika maisha yangu ya udaktari, na sikumbuki hata mmoja ambaye hakunya...ni kazi yangu, nimefuta wengi sana nikiwasaidia kuzaa.
Hii hali ya kunyanyapaa wanawake wanaokunya wakati wa kuzaa kuna kipindi ilikuwa hata kwa manesi wasiopata elimu ya kutosha kuhusu uzazi, wamama wa watu wakafinywa, wababa wakadhalilishwa kuwa wanawala Tigo wake zao, na ndoa zilivunjika sababu kama mume akilaumiwa kula Tigo wakati ye hajawahi kula...ina maana mkewe analiwa kwengine. hata mkewe ajitetee kivipi hawezi kuaminiwa cos ni nesi kasema...lakini ni uongo na mwenye data aje hapa tubishane kisayansi!
Anala sex haikuanza na generation yetu, hata enzi za Biblia...kina Lutu, Sodoma ilichomwa kwa sababu ya ulawiti....na ndipo lilipopatikana jina la 'Sodomy'. Na athari zake zimkuwa documented tangu zamani, si hizi tunazojaribu kuzizusha ili kutisha watu....narejea, hakuna tabia hatarishi ambayo imewahi achwa kwa sababu ya vitisho! tutafute njia mbadala..lakini hizi zinazoleta unyanyapaa (kuziba mikojo, na kunya wakati wa kujifungua) hazijengi na si kweli!