Kwanini wasambaa wanapenda sana kuongea kilugha hata mjini?

Kwanini wasambaa wanapenda sana kuongea kilugha hata mjini?

Yani nikipanda gari, mara nyingi wasambaa ndo wanapenda kuongea , utasikia nzeze nzeze, shiingi ngahi, kwani lazima kuongea kilugha mkiwa mjini? Kwanini msiongee Kiswahili
Bila Shaka we ni mzigua au mdigo? Wivu tu unqkusumbua
 
Nyerere halihalibu kizazi cha watanzania kwani kuna kosa gani mtu kuongea lugha yake ya Asili mbona kiswahili na kiingereza pia ni kilugha kwa makabil mengine. huo umoja wenyewe si uone isipo kua unafiki tu. umasikini ujinga unatupiga vile vile kama nchi zingine zenye lugha nyingi.
 
😂😂😂😂 Tate Mkuu
Mtoa mada atakuwa hajawahi kupanda gari moja na Wasukuma, au Wamasai!

NI ndani ya Wilaya mbili tu nchini (Lushoto na Korogwe) ndiyo utakutana na hao Wasambaa wakiongea kilugha ndani ya magari ya abiria/mtaani/sokoni, nk. Nje ya hizo Wilaya, ni aghalabu kukuta Msambaa anaongea kilugha hadharani.

Ila hayo makabila mawili hapo juu, hata uende Urusi, au Ukraine! Wao ni kuongea tu Kisukuma/Kimasai!!
 
Yani nikipanda gari, mara nyingi wasambaa ndo wanapenda kuongea , utasikia nzeze nzeze, shiingi ngahi, kwani lazima kuongea kilugha mkiwa mjini? Kwanini msiongee Kiswahili

Unakana ndugu zako?
 
Back
Top Bottom