Kwanini Wastaafu wote wanaopigwa kwenye mikopo umiza ni waalimu tu?

Kwanini Wastaafu wote wanaopigwa kwenye mikopo umiza ni waalimu tu?

Halafu wengi ni wa kanda ya ziwa mwanza,bukoba etc kuna wa juzi karudishiwa mil 22.3 walimptoza riba ya 300% yaani ni uongo mtupu! Hawa PCCB kuna FUTUHI wanafanya sio Bure!!
 
Unatakiwa ujue asilimia 90 ya watumishi wa umma ni walimu

Asilimia 90 ya watumishi wa umma wanaostafu na kuvuta Pesa ndefu ni walimu

Kwaiyo wingi wao ndio unafanya kila tarifa za masuala ya utaperi wa fedha uhusishe walimu sababu wapo wengi na wanavutaga pesa ndefu kidogo ukifananisha na kada nyingine

Walimu tunawachukulia pouwa ila mishahara yao ipo vizuri husani hawa wazee kinachowakaba hawana marupu rupu na hakuna rushwa

Mfano sasa hivi ajira za walimu zimesimama hakuna mwalimu anayechukua mshahara chini ya laki NNE kama wapo ni wachache sana ila wengi wanaanzi laki NNE , mpaka million uko hususani Hawa wazee wanaostafu wengi wamestafu mishahara yao million na kitu

Unaweza kuona kwanini wazee wa fursa mtaani wanacheza na walimu
mama yangu amestaafu ni mwalimu last week amevuta milion 110 nikasema daa hatari sana
 
Tehe tehe, ndiyo maana wanadharauliwa. Miaka 5 sasa hawajapandishwa mishahara na mwalimu mwenzao ambaye naye hajui kiingereza (English D).
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Nakubaliana kuwa niuongo! Mwalimu wa secondary anaanza n


Wewe utakuwa mwl mwenye elimu ya farm4, Div4 ,unafundisha form4. Maana unahisi kila mjadara unaohusu waalimu ni rigi.

Soma habari yenyewe halafu njoo na hoja.
Hakuna ubishi kuwa waalimu ndio wanao ongoza kwa kusaidiwa na takukuru!
Kwahiyo km watanzania lazima tujue chanzo ili jambo hili likome, vinginevyo takukuru itakuwa ni taasisi ya kusaidiwa waalimu tu.

Kwahiyo tunatafuta sababu ili kupata suruhisho maana hili nijanga kwa waalimu.
Wewe unasema eti rig na waalimu, nikweli aliyeweka matokeo ya waalim hapa yawezakuwa ww nimiongoni maana inaonekana uelewa mdogo japo ww ni mwl.
Ligi[emoji818]=rigi[emoji777]
 
Soma alichoandika kwa Makini then angalia ulichojibu...😂😂😂😂
Mkuu unataka niangalie positions wanazoshikilia serikalini?kitu gani kipya wamefanya zaidi ya kushikilia hizo nafasi? Kuna mmoja alijiunga ofisini kwetu baada ya kusitaafu,ndani probation period tumepiga chini,yaani hana lolote zaidi ya bla bla tu
 
Matokeo ya mwalimu wa shule ya msingi
Mathematics F
History D
Geography D
Civics D
Biology D
English D
Kiswahili C
Chemistry F
Physics F
Hebu tuwaheshimu walimu hata kama walifeli. Ni kwa sababu ya hao leo hii wewe umejua kuandika vizuri.

Heshima kwenu walimu wote popote mlipo.
Hakuna mwalimu aliye na matokeo Kama huyu jemba alivyo orodhesha

Nenda kozi zote kuanzia cheti mapaka elimu ya juu Ni mwalimu pekee mwenye ufauli mzuri sana. Hizo Ni chuki tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna mwalimu aliye na matokeo Kama huyu jemba alivyo orodhesha

Nenda kozi zote kuanzia cheti mapaka elimu ya juu Ni mwalimu pekee mwenye ufauli mzuri sana. Hizo Ni chuki tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Huwa nashindwa kuelewa mtu anadharau walimu waliomtoa ujinga. Leo hii yuko nyuma ya keyboard anatype vizuri sababu ya hao walimu anaowadharau.
 
Mimi ni ticha, maticha wenzangu punguzeni kukopakopa ovyo

Punguzeni matumizi msiyoyaweza

Wekezeni kwenye biashara, kilimo, ufugaji Nk

Acheni kuendesha bodaboda, kuendesha sio dhambi lakini kuendesha bodaboda sio hadhi kwa mwalimu.

Unapohitaji hela ingia salare adivansi.

Walimu jitahidini kujichanganya na makundi mengine kwenye jamii ili ujue changamoto zao,

Kwa wanaume, hakikisha mkeo unamdhibiti kwenye matumizi. Marafiki zangu wengi walikopa ili amnunulie mkewe dila, chupi, shanga, vitenge, poda, lotion nk.

Walimu achana na vyeo vitakavyokuweka mtegoni. Mdau fulani kasema ukiingizwa kanisani wanakupa cheo, hicho cheo ni cha kimkalati. Kila baada ya mwezi utavunwa tu, epuka uongozi kwenye vyama vya siasa, epuka uongozi kanisani au misikitini Nk

Mwl somesha watoto wako, kuna walimu wangu kibao watoto hawakusoma... Leo hii watoto ni wadangaji, house gelo na waendesha boda. Wasomeahe wanao.

Mwalimu nunua kiwanja hapo kijijini ulipo, wengi mnandoto za kuhamia mjini lakin huku mjini pamejaa walimu wa kike. Mlioko mjini nunua kiwanja pembeni ya mji. Anza kujenga taratibu hata kwa miaka 6! Usikope ukaanza ujenzi. Wengi huishia kwenye lenta.... Au anaezeka upande mmoja bati zinapelea. Weka malengo, usishindane na mtu.


Mwl tunza akiba, hata sh 80,000 kila mwezi. Ni aibu sana siku ya mshahara foleni nmb ni walimu wote. Kuweni wasitaarabu. Jiwekee utaratibu wa kuchukua hela benki.

Kwepa kujihusisha na harusi zenye gharama kubwa, harambee Nk! Niliwarika mwandamizi fulani kuwa mgeni rasimi mahafari ya tycs, alitoa mchango wa mil 2 kutoka mkopo wake, nilimnunulia konyagi kubwa akazichota. Nilimrudishia m1 nyimgine tukaingiza kwenye mfuko wa chama.

Walimu wenzangu panga uzazi. Usizidi watoto watano. Utawamudu vzr.


Mwl kuwa mwaminifu kwenye kazi maalumu, usikubari kuiba mtihani. Uzuri wa idara za kiuchunguzi na necta wako makini sana kwenye upelelezi. Hata shuleni unaposimamia chukulia kuna madarasa 10, tisa wakaiba wewe kama hukushirika wala hutapakiwa kwenye Nissan nyeupe kwenda kuhojiwa. Waliohusika watafinywa wenyewe. Ukiwa msimamizi mkuu utahojiwa lakin mkosaji atajulikana tu na atafinywa hasa. Nyongeza hapa kama huwez hizi kazi mwambie mkuu wa shule au Mwl mkuu asikupendekeze, au usiende kwenye semina ili usiape.


Kosa utakalofukuzwa au kusimamishwa kazi ndani ya wiki ni mitihani tu. Hata ukikutwa na mkurugenzi unamdinya dogo ofisi kama ded ni wa kiume atakuchimba biti tu, ukiwa mpole anakuambia andika barua uhame. Mara nyingi sana wakurugenzi, maafisa elimu na hadi madc huwaikoa walimu waliokamata na madogo wakiwa geto mubashara... Linasoviwa kikubwa linaisha.


Mwalimu hadi afukuzwe kazi, huyo habebeki. Watu wanakata miez 3 hawajulikani walipo, hadi siku mshahara unaposimama ndupo anajitokeza, analisovu linaisha anaendelea na kazi.


Jiepushe na makosa ya kukusudia, usilale na wanafunzi, epukana na siasa ndani na nje ya kazi,


Epuka mashindano, punguza kukopa na mwisho uwe unasali.


Hitimisho:
-kazi ya ualimu ni kudumu, hadi unakufa wanakulipa.
-utapata huduma ya bima ya afya wewe na mwenzi wako hadi umauti.

Mwalimu usiwe na haraka, wala kutaka utajiri.

Ndimi mwalimu wa zamu kuanzia kesho.
 
Tehe tehe, ndiyo maana wanadharauliwa. Miaka 5 sasa hawajapandishwa mishahara na mwalimu mwenzao ambaye naye hajui kiingereza (English D).
Nikukute central
 
Walimu ni janga la taifaaa! Huwezi amini kuna walimu kwa mwezi anapokea sh.2,000/- kwa ajili ya kukopa hovyo2 kwa watu binafsi! Maana benki wakibakiza theluthi moja, anakimbilia kwa watu binafsi! Yaani walimu ni shida tupu!
Uongo

Hakuna DED anaweza kukupitishia ukatwe hivyo
 
Hakuna mwalimu aliye na matokeo Kama huyu jemba alivyo orodhesha

Nenda kozi zote kuanzia cheti mapaka elimu ya juu Ni mwalimu pekee mwenye ufauli mzuri sana. Hizo Ni chuki tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa walimu wa nchi hii,jamaa kawapendekelea sana kwa matokeo hayo,wengi Wana zero na four mbaya
 
Back
Top Bottom