Ila tukiacha utani, mleta mada unachuki na walimu.
Nikweli kabisa ninachuki na walimu wenye tabia za hovyo hovyo ambao wamesababisha kazi ya ualimu ionekane haina maana.
Nilisema kazi ya ualimu nikazi ya heshima Enzi na enzi.
Tangia kwa Bwana YESU.... aliitwa mwl.
Asilimia kubwa nchi hii imeongozwa na Walimu, hata waliowahi kuwa wake wa Maraisi nchi hii ni walimu.
Hata rais wa sasa na mkewe ni walimu.
Mimi naandika hapa kwa sababu ya mwalimu.
Wewe mwalimu unaefundisha sasa hivi nikwasababu ya ...mwalimu.
Hivyo mimi sina chuki na walimu, ila ninawachukia baadhi ya walimu wenye tabia za hovyo hovyo ambao badala ya kufanya kazi za kitaaluma wanajiingiza kwenye mambo ya kifedheha.
Nakundi hili kubwa la baadhi ya walimu wenye tabia za kutaka vimichango kwa wazazi wapo s/m na sekondari za kata.
Hi school na vyuo huu upupu huwezi kuusikia.
Ndio maana nikauliza swali ambalo hakuna hata mmoja aliyejibu ya kwamba?
Nikwanini WAHADHIRI WA VYUO VIKUU walikataa kuitwa waalimu?
Hamuoni kwamba waamua kukwepa fedheha zinazofanywa na baadhi ya walimu kujiingiza kwenye mambo ambayo hayawahusu?
Kwani mwl. Ulisomea kuchangisha michele?
Ulisomea kuchangisha pesa wanafunzi?
Nani alikufundisha chuo kwamba watoto wakila watafauru?
Mbona walimu wazamani ambao mnawaita ni walimu wa UPE kwanini wao waliheshimika kuliko nyie?
Hujawahi kujiuliza mbona walimu wa zamani waliheshimika kuliko walimu waleo?
Sichukii walimu! Nachukia baadhi ya walimu wanatekeleza majukumu yasiyo wahusu hasa michango michango.
Acheni kutumiwa na vyama vya siasa ili wananchi waichukie serikali yao na chama chao wakati huu wa uchaguzi
Mbona kabla ya uchaguzi hamjaja na michango ya 10kg za mchele na 2000@ mwanafunzi.
Nawathamini sana walimu , fanyeni kazi zenu msikubali kufanya mambo yasiyo wahusu.
Kama ww ni mwl. Unaependa tumichango michango kwa wanafunzi na watoto wa shule kiukweli nachukia kwa sababu mnamaliza heshima ya walimu weledi wachapa kazi na wanaosimamia misingi ya taaruma zao.
Wapo wengi tu. Na nilafiki zangu sana2! Wachapa kazi , wana mashamba yao nje ya jiji, wanafuga nguruwe, kuku nk.
Wana maduka na maduka yao ya vitabu.
Chapa kazi mwl.