Mimi ni ticha, maticha wenzangu punguzeni kukopakopa ovyo
Punguzeni matumizi msiyoyaweza
Wekezeni kwenye biashara, kilimo, ufugaji Nk
Acheni kuendesha bodaboda, kuendesha sio dhambi lakini kuendesha bodaboda sio hadhi kwa mwalimu.
Unapohitaji hela ingia salare adivansi.
Walimu jitahidini kujichanganya na makundi mengine kwenye jamii ili ujue changamoto zao,
Kwa wanaume, hakikisha mkeo unamdhibiti kwenye matumizi. Marafiki zangu wengi walikopa ili amnunulie mkewe dila, chupi, shanga, vitenge, poda, lotion nk.
Walimu achana na vyeo vitakavyokuweka mtegoni. Mdau fulani kasema ukiingizwa kanisani wanakupa cheo, hicho cheo ni cha kimkalati. Kila baada ya mwezi utavunwa tu, epuka uongozi kwenye vyama vya siasa, epuka uongozi kanisani au misikitini Nk
Mwl somesha watoto wako, kuna walimu wangu kibao watoto hawakusoma... Leo hii watoto ni wadangaji, house gelo na waendesha boda. Wasomeahe wanao.
Mwalimu nunua kiwanja hapo kijijini ulipo, wengi mnandoto za kuhamia mjini lakin huku mjini pamejaa walimu wa kike. Mlioko mjini nunua kiwanja pembeni ya mji. Anza kujenga taratibu hata kwa miaka 6! Usikope ukaanza ujenzi. Wengi huishia kwenye lenta.... Au anaezeka upande mmoja bati zinapelea. Weka malengo, usishindane na mtu.
Mwl tunza akiba, hata sh 80,000 kila mwezi. Ni aibu sana siku ya mshahara foleni nmb ni walimu wote. Kuweni wasitaarabu. Jiwekee utaratibu wa kuchukua hela benki.
Kwepa kujihusisha na harusi zenye gharama kubwa, harambee Nk! Niliwarika mwandamizi fulani kuwa mgeni rasimi mahafari ya tycs, alitoa mchango wa mil 2 kutoka mkopo wake, nilimnunulia konyagi kubwa akazichota. Nilimrudishia m1 nyimgine tukaingiza kwenye mfuko wa chama.
Walimu wenzangu panga uzazi. Usizidi watoto watano. Utawamudu vzr.
Mwl kuwa mwaminifu kwenye kazi maalumu, usikubari kuiba mtihani. Uzuri wa idara za kiuchunguzi na necta wako makini sana kwenye upelelezi. Hata shuleni unaposimamia chukulia kuna madarasa 10, tisa wakaiba wewe kama hukushirika wala hutapakiwa kwenye Nissan nyeupe kwenda kuhojiwa. Waliohusika watafinywa wenyewe. Ukiwa msimamizi mkuu utahojiwa lakin mkosaji atajulikana tu na atafinywa hasa. Nyongeza hapa kama huwez hizi kazi mwambie mkuu wa shule au Mwl mkuu asikupendekeze, au usiende kwenye semina ili usiape.
Kosa utakalofukuzwa au kusimamishwa kazi ndani ya wiki ni mitihani tu. Hata ukikutwa na mkurugenzi unamdinya dogo ofisi kama ded ni wa kiume atakuchimba biti tu, ukiwa mpole anakuambia andika barua uhame. Mara nyingi sana wakurugenzi, maafisa elimu na hadi madc huwaikoa walimu waliokamata na madogo wakiwa geto mubashara... Linasoviwa kikubwa linaisha.
Mwalimu hadi afukuzwe kazi, huyo habebeki. Watu wanakata miez 3 hawajulikani walipo, hadi siku mshahara unaposimama ndupo anajitokeza, analisovu linaisha anaendelea na kazi.
Jiepushe na makosa ya kukusudia, usilale na wanafunzi, epukana na siasa ndani na nje ya kazi,
Epuka mashindano, punguza kukopa na mwisho uwe unasali.
Hitimisho:
-kazi ya ualimu ni kudumu, hadi unakufa wanakulipa.
-utapata huduma ya bima ya afya wewe na mwenzi wako hadi umauti.
Mwalimu usiwe na haraka, wala kutaka utajiri.
Ndimi mwalimu wa zamu kuanzia kesho.