TheChoji
JF-Expert Member
- Apr 14, 2009
- 5,771
- 17,849
Tunakubaliana kabisa, jamani eeh kesho tukutane saa tatu kamili asubuhi. Watu wote wanaitikia "Sawa, saa tatu imekaa vizuri kabisa!"
Wewe unawahi saa tatu kasoro dakika 5 unafika eneo la tukio unakuta hakuna mtu hata mmoja. Unaanza kusubiri... saa tatu kamili, saa tatu na dakika 10, saa tatu na nusu.... saa nne!
Ndio watu wanaanza kujitokeza mmoja mmoja huku ikijichekesha chekesha "Ooh unajua bana mambo mengi asubuhi..." Sasa si mngesema tukutane saa nane?
Hivi kweli Waafrika tutaweza mambo serious kama swala la muda tu linatushinda!