Kwanini watangazaji na wachambuzi wengi wa mpira ni Yanga?

Kwanini watangazaji na wachambuzi wengi wa mpira ni Yanga?

Mdau jf

Senior Member
Joined
Sep 10, 2020
Posts
182
Reaction score
313
Kwa research niliyo ifanya mtandaoni hususani instagram, pamoja na radion (kupitia vipindi vya michezo) nimegundua watangazaji na wachambuzi wa mpira wengi wao ni YANGA. mf. pale wasafi sports Arena wote wale ni jangwani, EFM ukiondoa Ibrahim Maestro walio baki wote ni yanga, CLOUDS ndiyo kabisa.

Hii inasababisha hata yanga akiwa na makando kando kwenye mechi au migogoro ndani ya club utaona wanayaficha ficha.

Lakini ikiwa upande wa simba wataandika watachambua hao mpaka nucta

Wanatukosea sana sisi wasikilizaji na wafuatiliaji wa habari za michezo mitandaoni
 
Kuna yule dogo Privaldinho namkubali sana kwenye uchambuzi hasa katika maandiko yake na uwezo wa kupekenyua habari za chini chini. Tatizo anashindwa kubalance mahaba yake na chuki binafsi kwa Haji
 
Mimi nashabika Simba...pia nasikiliza sana vipindi vya michezo it's like nipo addicted yani...kila muda wa michezo na earphones zangu...
Lakini nilichogundua ni kwamba tatizo si kwa wachambuzi.

Ila sisi wasikilizaji tunapenda kusikia tunavyotaka kusikia...wachambuzi wanajitahidi kuwa neutral lakini sisi Mashabiki hatutaki timu zetu zisemwe ikisemwa Yanga basi wale Simba ikisemwa Simba vivyo hivyo.

Kifupi tumewachoka mashabiki maandazi...if u ain't no football you better find some other things to do....wachambuzi hawana shida kabisa tatizo mashabiki maandazi hampendi ukweli.
 
Kwa research niliyo ifanya mtandaoni hususani instagram, pamoja na radion (kupitia vipindi vya michezo) nimegundua watangazaji na wachambuzi wa mpira wengi wao ni YANGA
mf. pale wasafi sports Arena wote wale ni jangwani, EFM ukiondoa Ibrahim Maestro walio baki wote ni yanga, CLOUDS ndiyo kabisa.

Hii inasababisha hata yanga akiwa na makando kando kwenye mechi au migogoro ndani ya club utaona wanayaficha ficha.

Lakini ikiwa upande wa simba wataandika watachambua hao mpaka nucta

Wanatukosea sana sisi wasikilizaji na wafuatiliaji wa habari za michezo mitandaoni
Tyentye daahh.
 
Waandishi wengi hawajasoma na kwa sababu washabiki wanapenda kusikiliza ujinga ujinga na yanga ni timu ya unedicated ndio hapo utaona waandishi wengi ninwa yanga ila waandishi Simba wapo lakini hawawezi kuandika habari za upotoshaji
 
Hizi ni hisia tu, kama hisia za Haji Manara anavyo amini ana kikosi kipana anaweza shusha vikosi viwili siku moja vinapiga mechi
Kiuhalisia Simba haiwezi hilo au hujawahi kuona ikifanya hilo?
 
Mimi siku izi nmepunguza kusikiliza vipindi vya michezo inaweza pita hata wiki 2 sjaskiliza kwa sababu ya ujinga huo huo wa wachambuzi na watangazaji wa michezo
 
Back
Top Bottom