Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
whats wrong with this?
[/B][/COLOR]

Sijui, labda mjinga ni mimi. Hivi unakusanya pesa hadi zinazidi million 30 ndo unazibeba kifua mbele kwenda benki ili wakuone fahari au? Kama mtu anaweza kukatwa mkono kwa ajili ya simu isiyozidi laki 2 au chain ya laki 1, ni akil na busara kupita mitaani na milioni 30?

Kuna jamaa mzungu alipewa dola 1000 taslimu (Tshs 1.4mil) ampelekee mshikaji ulaya akakataa kata kata kwamba hawezi kubeba pesa nyingi kiasi hicho (cash). May be jamaa kama huyo ndo wajinga au sisi tunaotembea mjini na mamilioni ya shilingi, tena wakati mwingine tunapanda hata daladala?
 
Mkuu huenda milioni 30 ni mauzo ya biashara yake kwa nusu siku tu! Usishangae.
 
Nimesoma kitabu kimoja kinasema sababu za umasikini ni: history, bad governance, natural disasters, personal qualities and cultural practices, lack of income and power, unemployment, lack of education, globalization, overpopulation (Taylor, 2003). Some researchers also add diseases in the listing like malaria.

Nafikiri cha msingi hapa ni elimu kwanza ambayo itaondoa mengine yote na kubaki na poverty free community. Mfano Tanzania tunaongelea kilimo kwanza bila kutoa elimu kwa wakulima namna ya kulima kwa ustadi, je unategemea mavuno yatakuwa mengi, njaa itaendelea na kujikuta tunarudi kwenye wimbo wa MDGs - reduce hunger by 50% by 2015!

Kwa kifupi nafikiri elimu ni kupata habari, maarifa, ujuzi, n.k. na vitu hivi uitwa "information"/ 'knowledge - collection of info' na kuna msemo information is power, information is a resource like gold, diamond, etc. Watanzania wengi kwanza hatujisomei, tunapenda kuiba mitihani, tunapenda kununua vyeti (diploma disease), mitihani yetu mingi ni marudio ya maswali hivyo watu usoma past pepers tu na kutumia madesa kwenye elimu ya juu.
 
Mkuu upo sawa elimu kwanza
 
Ndugu Mwanamayu,

Kumuweka mtu kitako into any form of training, ilhali hajui his or her next meal ni nini, ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu. Kumtoa mtz wa kawaida hapo alipo alipo ni zaidi ya juhudi moja, inahitaji a cluster of supporting efforts. Ndipo suala la vipaumbele linapokuja na analysis mwanana ya kufikia malengo.
 
Sijui, labda mjinga ni mimi. Hivi unakusanya pesa hadi zinazidi million 30 ndo unazibeba kifua mbele kwenda benki ili wakuone fahari au? Kama mtu anaweza kukatwa mkono kwa ajili ya simu isiyozidi laki 2 au chain ya laki 1, ni akil na busara kupita mitaani na milioni 30?

Kuna jamaa mzungu alipewa dola 1000 taslimu (Tshs 1.4mil) ampelekee mshikaji ulaya akakataa kata kata kwamba hawezi kubeba pesa nyingi kiasi hicho (cash). May be jamaa kama huyo ndo wajinga au sisi tunaotembea mjini na mamilioni ya shilingi, tena wakati mwingine tunapanda hata daladala?

Abdul amekwambia labda ndio mauzo yake ya nusu siku ulitaka aweke nyumbani??mi namsifu kwa kupeleka benki kuliko akina DAU wanaoweka kwenye safe na kuibiwa.
 
watanzania ni wajinga na serikali inapenda sana tuendelee kuwa hivyo. Kutokana na ujinga wetu hatuoni kama nchi ina resources na kama zipo viongozi hawataki tuzitap hizo resources na badala yake wanaitwa watu toka nje kuja kufaidika.
 
Ruling wate Wenye NJAA na UNinformed ni Rahisi sana kuliko kongoza wasomi and wasio na njaa,
 
Mkuu huenda milioni 30 ni mauzo ya biashara yake kwa nusu siku tu! Usishangae.

Ninachoshangaa siyo wingi wa pesa. Najua kwa baadhi ya watu hapa Bongo hizo ni pesa kiduchu za kununua sigara, ni vijisenti tu. Ila nashindwa kuelewa kama huyo mtu anajua ni kwa kiasi gani anaweka si pesa tu, bali maisha yake rehani.

Abdul amekwambia labda ndio mauzo yake ya nusu siku ulitaka aweke nyumbani??mi namsifu kwa kupeleka benki kuliko akina DAU wanaoweka kwenye safe na kuibiwa.

Kwani wafanyabiashara hawawezi kukaa na mabenki wakatengeneza utaratibu mzuri wa kulipana kuliko kubeba rambo zimejaa minoti? Nimeambiwa Kenya wanatumia Bank cheaques kufanya malipo. Hizi zinafanyakazi kama cash. Kwa kujifanya majuha na kubeba mipesa ndo kusema sisi ni wajanja kuliko watu wengine duniani?

watanzania ni wajinga na serikali inapenda sana tuendelee kuwa hivyo. Kutokana na ujinga wetu hatuoni kama nchi ina resources na kama zipo viongozi hawataki tuzitap hizo resources na badala yake wanaitwa watu toka nje kuja kufaidika.

Kweli mkuu, halafu tunalewa sifa kwamba sisi bab kubwa kumbe hamna kitu!
 
Japan to grant Tanzania Sh14 billion for procurement of rice

By Victor Karega
Japan will give Tanzania a grant of $10.3 million (about Sh14 billion) to help it procure rice to alleviate immediate food needs.

Documents for the grant were exchanged in Dar es Salaam yesterday between the Treasury permanent secretary, Mr Ramadhan Khijjah and the Japanese ambassador to Tanzania, Mr Hiroshi Nakagawa on behalf of their governments.

The rice to supplement food shortage in the country sparked by the 2008 drought will be procured from Japan.

"Erratic rainfall has been causing deficits of food production almost every year….implementation of this food aid project in Tanzania addresses the immediate food shortage in the country mainly caused by low rainfall during the past crop season," Mr Khijjah said.

An assessment conducted by the Ministry of Agriculture, Food Security and Cooperatives showed that 717,684 people in 47 districts were facing food shortages to the tune of 21,604 tonnes from March to May 2010.
To cover the shortage, 2,160 tonnes will be distributed freely while 19,444 tonnes will be sold at subsidised prices during that period.

Maize and sorghum stocks held by the National Food Reserve Agency (NFRA) declined to 60,694 tonnes by the end of March 2010 from 64,461 tonnes recorded at the end of the preceding month, according to the Bank of Tanzania (BoT).

"The decline in stocks was on account of the sale of grains to the Government and private traders for distribution to districts experiencing food shortages," indicated the BoT Monthly Economic Review for April 2010.

The NFRA purchased 73,280 tonnes of grains from the domestic market during the first nine months of the current financial year.

The amount is about 46 per cent of the target of purchasing 160,000 tonnes during the entire 2009/2010 financial year.

Mr Khijjah said proceeds from the sale of rice will be used to finance community-based development projects that have the potential to contribute towards increasing agricultural production and productivity in the country.
According to Mr Nakagawa, food security and improvement of food production are among priority areas of the Japanese official development assistance to Tanzania.

This forms part of Japan's commitment made at the fourth Tokyo International Conference on African Development (TICAD IV) held in the Japanese city of Yokohama in 2008.
So far, Japan has given food aid worth $141.5 million (about Sh190 billion) to Tanzania.

Source: the citizen:

Ona facts hapo chini, halafu badala ya sisi kulima ili tuwe self sufficient in food tunamwita mwarabu anakuja analima kwetu chakula chote anapeleka kwao, sisi tunabaki tunatembeza bakuli na kuomba chakula kwa watu ambao hawana ardhi kabisa. Ukiuliza hatuna hela, mwekezaji aje. Ndege, rada na richmond hatuhutaji waekezaji ni hela zetu wenyewe huu ni ujinga kabisa sio umaskini.

Kuna picha ilitoka Daily News ( towards memory lane) mwaka 1966 gereza la kidete lilikuwa linalima mpunga mechanically na lilikuwa na Combine harvester hii leo viongozi tofauti, Ardhi ile ile, wafungwa ni wengi zaidi hivi sasa kuliko ilivyokuwa 1966 lakini cha ajabu tunashindwa kulima tunaipeleka ardhi TIC . CEO wa pale anatoka magazetini with a broad smile on the face eti anafanya kazi kwa kugawa ardhi yetu kwa watu wa nje.

What the hell is wrong with us? Shame on us. Tuondokane na ujinga?

1.FACTS ABAOUT JAPAN:
Official Name: Nihon or Nippon (Japan)- Land of the Rising Sun
Capital: Tokyo
Official Language: Japanese
Chief of State: Emperor
Head of Government: Prime Minister
Monetary Unit: Yen
Population: 126,398,000 in 1998
Area: 145,883 square miles (377,835 square kilometers)

2. FACTS ABOUT TANZANIA:
Official Name:​
United Republic of Tanzania​
Area:​
945,000 sq. km
Time:​
GMT +3​
Population:​
29 million
Population Density:​
31/sq. km​
Urban/Rural Split:​
22% / 78%​
Literacy rate:​
68 per cent
 
Kwa muda mrefu, nimekuwa nikiangalia jinsi tunavyofanya mambo yetu na kuanza kuwa na wasi wasi kwamba tunaweza kuwa tunasumbuliwa na ugonjwa wa hatari sana. Kama hatutaweza kuutambua ugonjwa wetu, basi itakuwa vigumu na labda itachukua miaka mingi kutafuta tiba sahihi.

Ukifika vijijini (kwenye maeneo mengi ya nchi yetu), unakutana na ardhi nzuri sana, majani mengi tu ya kulisha mifugo lakini watu bado ni maskini. Fursa kama hizo hazipatikani sehemu nyingine na hata kwenye mikoa iliyochangamka kama Kilimanjaro.

Ukifika mjini huko ni balaa. Kuna watu wanashinda chini ya mwembe kuanzia asubuhi hadi jioni siku saba za week. Ila kuna wale ambao wanaonekana kama wametoka kidogo nao wana vituko vyao. Leo nimekutana na mama mmoja mfanyabiashara, akiwa benki anaweka karibia shs milioni 30 taslimu.

Katika mazingira kama hayo, sisi tuna tatizo lipi hasa? Ujinga au umasikini?
\

both
 
Kwani wafanyabiashara hawawezi kukaa na mabenki wakatengeneza utaratibu mzuri wa kulipana kuliko kubeba rambo zimejaa minoti? Nimeambiwa Kenya wanatumia Bank cheaques kufanya malipo. Hizi zinafanyakazi kama cash. Kwa kujifanya majuha na kubeba mipesa ndo kusema sisi ni wajanja kuliko watu wengine duniani?

mkuu hayo ya cheques yote yapo bongo lakini sio kila biashara wanaweza kulipana kwa cheque,mfano mtu anaduka la jumla la vocha za simu anawauzia wale wa vibanda,je hawa watamlipa kwa cheki 10,000 au 100,000 zao??
 
WaTZ ni wajinga na WAVIVU.Akili zinauwezo wa kuondoa umasikini hata kama unaishi jangwani kusiko na resources.
 
mkuu hayo ya cheques yote yapo bongo lakini sio kila biashara wanaweza kulipana kwa cheque,mfano mtu anaduka la jumla la vocha za simu anawauzia wale wa vibanda,je hawa watamlipa kwa cheki 10,000 au 100,000 zao??

Una maana haiwezekani kulipana kwa bank cheque au? Haya mambo yanatokana na kuendekeza uvivu wa kufikiri. Hakuna mtu alitegemea kuwa siku moja biashara ya kulipia wafanyakazi wote dirishani ingefutika. Na pia siku hizi karo za shule zinalipwa benki. Kwa nini mengine yashindikane? People need to use their brain.
 
Kwa muda mrefu, nimekuwa nikiangalia jinsi tunavyofanya mambo yetu na kuanza kuwa na wasi wasi kwamba tunaweza kuwa tunasumbuliwa na ugonjwa wa hatari sana. Kama hatutaweza kuutambua ugonjwa wetu, basi itakuwa vigumu na labda itachukua miaka mingi kutafuta tiba sahihi.

Ukifika vijijini (kwenye maeneo mengi ya nchi yetu), unakutana na ardhi nzuri sana, majani mengi tu ya kulisha mifugo lakini watu bado ni maskini. Fursa kama hizo hazipatikani sehemu nyingine na hata kwenye mikoa iliyochangamka kama Kilimanjaro.

Ukifika mjini huko ni balaa. Kuna watu wanashinda chini ya mwembe kuanzia asubuhi hadi jioni siku saba za week. Ila kuna wale ambao wanaonekana kama wametoka kidogo nao wana vituko vyao. Leo nimekutana na mama mmoja mfanyabiashara, akiwa benki anaweka karibia shs milioni 30 taslimu.

Katika mazingira kama hayo, sisi tuna tatizo lipi hasa? Ujinga au umasikini?

Mkuu tatizo ni mfumo, Mfumo mfomo

Kwa jinsi mambo yalivyo kwa mazingira ya vijijini hata ukijitahidi vipi huwezi kutoka hata kidogo, ntatoa mifano michache mfano mkulima anaelima mahindi maharage, karanga ´kutokana na kukosa viwanda vya kati wafanya biashara wanaenda mpaka vijijini wao ndo wanapanga bei mkulima hana maamuzi hata kidogo bei hailingani na garama za uzalishaji wewe unafikiri huyu Mkulima ataendelea nini mfano utakuta dhamani halisi ya gunia la mahindi ni shilingi laki mbili mkulima aliyelima ataambulia hapo elfu ishirini na Bakhresa anayesaga hayo mahindi atakula hapo zaidi ya laki na hamsini,,, Makampuni ya Muhamed enterprises yalianza kwa kuwaibia wakulima vijijini

Huo ni mfano moja hali iko hivyo kwa Wafugaji, wavuvi, wachimbaji madini wadogodogo nk,,Huwezi amini mfanya biashara anatoka Yemen anaenda mpka chunya kununua Gold kwa mchimbaji mdogo kapita wapi kote je huyo mchimbaji mdogo bei itaijulia wapi, mfumo unamruhusu, mtu anatoka nairobi mpaka mufindi kununua mbao,, mfumo unamruhusu,,,

Nimejionea kwa wenzetu wazungu vyama vya ushirika ndio vinatafuta masoko, Ndivyo vina toa link kati ya muuzaji na mnunuzi, hivi vyama ndio vinaongeza dhamani kwa bidhaa wanazolima wakulima sisi vyama vya ushirika tuliuwa, vingine tukageuza vitega uchumi tutegemee nini???hapa kwetu anayemunganisha ni DALALI tena mwizi, mwenye njaa,

hakuna aliyetuloga Watanzania, wapo watu wanajitahidi lakini jasho lao linaishia mifukoni mwa wafanya biashara wachache na wanasiasa,
 
[/SIZE]

Hayo yote ni kweli. Kwa nini hayatekelezwi? Na kama wananchi wanaona hawatekelezewi, kwa nini wanakaa kimya? Wameridhika na umaskini au bongo imelala (wajinga)? Na ukizingatia kuwa kila baada ya miaka 5 wanapika kura!
 
Ujinga,Uswahili,uroho na kujifanya kujua kumbe hakuna kitu.
Tuna maji mengi,Lake Victoria,Tanganyika,Nyasa ,Bahari ya Hindi etc.

Hakuna hata large scale irrigation ingeweza kusaidia kilimo mwaka mzima.
Na sasa global warming ,mvua hazinyeshi.
Baada ya miaka 50 ya Uhuru,watu wanalala njaa ,maana mvua hazinyeshi,kwa hiyo hakuna kuvuna.

Hakuna kitu kinachoniuma ukisikia kuwa MZUNGUanakwambia you cant run your affairs and feed your people!
Kuna watu somewhere nchini wanakula panya,sababu hakuna mlo wa kawaida.
 
Kwa TZ naona ule msemo usemao kwenye miti hakuna wajenzi uko applicable we have everything lakini bado tuu maskini sometimes huwa nawaza Tz ingekuwa located SAHARA desert tungetia akili
 
Charity what you think should be done?

Hayo ndo makosa tunayofanya. Huwezi kutafuta suluhu kabla ya kujua tatizo. Walau tukiweza kujua kuwa tatizo letu kubwa ni ujinga basi tunaweza kuelekeza nguvu huko kwenye kufuta ujinga. Au kama wengi tunaamini kuwa tatizo ni umasikini pia mikakati inaweza kulenga kutatuta tatizo la umasikini, kwa kuanzia na mtu mmoja mmoja hadi Taifa.

Ujinga,Uswahili,uroho na kujifanya kujua kumbe hakuna kitu.
Tuna maji mengi,Lake Victoria,Tanganyika,Nyasa ,Bahari ya Hindi etc.

Hakuna hata large scale irrigation ingeweza kusaidia kilimo mwaka mzima.
Na sasa global warming ,mvua hazinyeshi.
Baada ya miaka 50 ya Uhuru,watu wanalala njaa ,maana mvua hazinyeshi,kwa hiyo hakuna kuvuna.

Hakuna kitu kinachoniuma ukisikia kuwa MZUNGUanakwambia you cant run your affairs and feed your people!
Kuna watu somewhere nchini wanakula panya,sababu hakuna mlo wa kawaida.

Je ni wote katika nchi hii ni wajinga, waroho na wajuaji? Hakuna walau mmoja nayeweza kupigiwa mfano ambayo ana sifa kinyume na hizo?

Kwa TZ naona ule msemo usemao kwenye miti hakuna wajenzi uko applicable we have everything lakini bado tuu maskini sometimes huwa nawaza Tz ingekuwa located SAHARA desert tungetia akili

Mkuu miti ipo lakini wajenzi hakuna kwa nini? Ni vipofu kiasi kwamba wao miti hawaioni? Au wana nyumba nzuri sana kiasi kwamba hawahitaji kujenga nyingine? I think there is something that is missing in most of us,... and what is that thing?
 
Back
Top Bottom