Mleta mada umechambua vizuri sana. ila kwa utamaduni wa ccm waliozoeshwa kuwa zidumu fikra za viongozi na taswira ya ccm mbele kwa mbele. wengi watalifumbia macho hili NIA NI kukiludisha Chama hiki kinachoitaji ukarabati mkubwa. CCM kikikarabatiwa ni chama kizuri. ila ukarabati wake sharti kipaki gereji kwa 10 yrs kikijipanga upya.
Tuingize mfumo mpya kama wenzetu Kenya walivyofanya
 

Umaskini wa Tanzania unasababishwa na mambo matatu makubwa kwa mtazamo wangu.Kwanza ni watawala wetu kukumbatia,kuabudu na kusujudia sera kandamizi za mashirika mumiani ya Btettonwoods yaani WB na IMF ambapo watawala wetu hugeuka. mawakala wa sera hizi za kibeberu zinazofukarishatt nchi yetu.Pili ni kukithiri kwa wizi serikalini,mashirika ya umma,idara na taasisi za serikali na halmashauri.Tatu ni kukosekana kwa uwajibikaji,hasa uzembe,kufanya kazi kwa mazoea na kutojali.
 
Mi nakubaliana na wewe , sehemu moja tu ukawa mmechemsha ni kukubali kuweka watu waliokuwa sehemu ya uozo huo kwa miaka 30, Leo wanasimama wanaisema ccm wakati na wao walikuwa viongozi wakuu na hawa ndio mnataka muwape nafasi za juu , aww hapa mmechemsha ila mengine yote nakubaliana na wewe
 
Sababu kubwa ni lowassa,Rostam la mtajiri wengine walioko nyuma yao kujilimbikizia mali la kuwafanya watanzia pamoja la serikali yao kuwa maskini

Sababu kubwa ni ccm na mtambo wake wa kupika mafisadi wadogo na wakubwa kuanzia ngazi za mitaa hadi taifa
 
Mfumo wa kifisadi umepumbaza watu walionadhamana ya kusimamia na pia kupumbazwa kwa watanzania kumefanya watu wasione na kuelewa namna tunavyoweza kuuondoa umaskini wetu kwa kutumia resources zetu
 
uwezo wa kuyachimba mnao?,technology mnayo ili myachimbe wenyewe.
unadhani mtu aje na vyote hivyo,awekeze mabilioni ya dola kisha nyie mchukue hela?,,,,
 
uwezo wa kuyachimba mnao?,technology mnayo ili myachimbe wenyewe.
unadhani mtu aje na vyote hivyo,awekeze mabilioni ya dola kisha nyie mchukue hela?,,,,

Ni serikali dhaifu ya CCM inashabikia mawazo ya kipumbavu kama yako.

Kwahiyo nchi nyingine za Afrika kama Botswana wana vifaa na utaalamu?
 
wanajamvi amani iwe kwenu. kama ni kusema ukweli taifa letu linafanana na ile nchi ya ahadi ya wana wa israeli, ina kila uzur wa kupendeza na ardhi yake yote ni mali ina madini haina mfano, mito, maziwa na bahar hakika mungu aliziumba mbingu na dunia ametupendelea ila umaskin wetu unatia aibu sana ebu hawa walioko madarakan mda mrefu tuwatoe jaman kwa miaka mitano tujaribu wengine, mana tunadhalilika dunian
 
Serikali ya CCM iliwathamini sana wawekezaji kutoka nje hata ikafikia hatua ya kuwapa miaka 5 kufanya biashara bila kulipa kodi (grace period) lakini raia waTanzania anatakiwa kulipa kodi fast mara tu anapoanza biashara yake bila kujali ni ndogo au kubwa wakati mwingine inatia hasira.
 
Juzi juzi nilifika ofisi za TRA lindi ili niweze kukadiriwa kodi kwaajili ya biashara yangu ndogo niliyotaka kuianzisha, lakini kilichinishangaza ni pale nilipoambiwa niiende bank nikalipe kodi kabla ata sijaanza biashara, tena ni vijana wenzangu wanaoitwa tax officers ndo walikuwa wakinikomalia kwa nguvu zote
 
Unaposema atii wataka anzisha biashara, ni biashara gani weye waweza hata ya kuuza ukwaju?? Profesa Muongo kamwambia Dr Mengi kuwa na vijisenti vyake anachoweza ni kuuza juice tuuu. Yaani, unakadiriwa kodi ya kuzidi hata ile hela yako ya mtaji ili ukimbie tuu usiingie kwenye vitabu vyao vya kodi. Yaani hii ni ajabu kabisa. Badala ya watu kupeleka fedha za kodi zijenge nchi wanaona heri kuzila kuliko kulipia kodi kwani hawaoni inachofanya kodi yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…