Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Mleta mada umechambua vizuri sana. ila kwa utamaduni wa ccm waliozoeshwa kuwa zidumu fikra za viongozi na taswira ya ccm mbele kwa mbele. wengi watalifumbia macho hili NIA NI kukiludisha Chama hiki kinachoitaji ukarabati mkubwa. CCM kikikarabatiwa ni chama kizuri. ila ukarabati wake sharti kipaki gereji kwa 10 yrs kikijipanga upya.
Tuingize mfumo mpya kama wenzetu Kenya walivyofanya
 
Tanzania got its Independence on 1961 and Kenya got theirs on 1963.
Kenya is already a Second World Country while Tanzania is still on the list of Poorest countries.
Fact 1:
Pato la Mtanzania kwa mwaka ni Tshs. 1,996,000 na Pato la Mkenya kwa mwaka ni Tshs. 3,176,000..
Pato la nchi (Tanzania) ni Tshs. Trillion 98.36 na Pato la nchi kwa Kenya ni Tshs. Trillion 140.
Fact 2:
Tanzania kuna madini ya kila aina, Tanzanite, Dhahabu, Rubi, Uranium, Makaa ya Mawe, Chuma, Kenya hawana madini ya aina yoyote lakini bado wametuzidi pakubwa kwenye pato la Taifa. Sekta ya madini inachangia 3.3% kwenye pato la taifa kutokana na mikataba mibovu iliyowekwa na viongozi wa CCM.
.
Fact 3:
Kenya taratibu inautawala Uchumi wa Tanzania, tayari wana Bank mbili zinazofanya kazi nchini Tanzania (KCB and Equity Bank), Tanzania bado hatuna Bank yoyote Kenya.
Supermarkets za Kenya tayari zimeingia nchini Tanzania na kuuwa zetu (Nakumat tayari imeshainunua Shoprite (T), UCHUMI Supermarkets).. Sisi Imalaseko Supermarkets zilishakufa kule Kenya.
Soko la Hisa Dar Es Salaam (DSE) lina Jumla ya Kampuni 21, kati ya hizo Kampuni 7 ni za Kikenya lakini Soko la Hisa la Nairobi (NSE) lina zaidi ya Kampuni 64 na hakuna kampuni hata moja ya Kitanzania.. Hii ni mbaya sana kiuchumi..
Fact 4:
2004 Tanzania tulikuwa na Ndege mbili za serikali (Air Tanzania) na Kenya walikuwa na Ndege 19 (Kenya Airways-KQ)..
2015 Tanzania tuna Ndege 1 ya kukodi kwa ajili ya kupigia Kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Kenya wana Ndege 47 zinazotua katika viwanja 62 vya mabara yote duniani...
Tukumbuke bila kuwa na Shirika letu la Ndege, Utalii tuna ongelea ni kazi bure..
Fact 5:
Wakenya wanacheza smart games na Watanzania bado tumelala..
After Precision Airlines (PA) kuwa threat kwa operation za Kenya Airways (KQ) route za Tanzania na Kenya, KQ wakaingia ubia na PA very smartly na wakawa wanaihujumu undercover. Leo hii PA iko hoi na tayari Operations za Jomo Kenyatta-KIA, Mwl. Nyerere zimerudi kwa KQ.
Pili, baada ya TBL kuruhusiwa kuuza bia Kenya, na Kenya walete bia zao Tanzania. TBL wakakaribia kuuwa bia za Wakenya huko kwao wakati huo bia yao TUSKER ikawa haifanyi vizuri hapa Tanzania. Wakavunja makubaliano, ili kila mtu afanye biashara yake kwake. After years EABL ya Kenya ikaingia ubia na SBL na wakaipa License ya kuzalisha na kusambaza TUSKER hapa nchini.. Smartly EABL wanauza hapa kwetu wakati sisi TBL haiuzi kule kwao..
Wakati hayo yote yanafanyika Watanzania tunalazwa na fikra dhaifu za viongozi wetu wa CCM. Education Matters a lot ndio maana UKAWA tukaja na 1.ELIMU 2.ELIMU 3.ELIMU, tumeona mbali sana.
Fact 6:
Wakati Kenya wao wakifungua mipaka yao na kwenda kufanya Biashara na uwekezaji na kutafuta ajira kila mahali, Serikali ya CCM imetufundisha uoga na kutojiamini.
Serikali ya CCM inatuambia tukiingia kwenye soko la ajira la Afrika Mashariki Wakenya watatupiga bao. Swali ni kwa nini? Ni kwasababu serikali ya CCM inajua haitoi elimu bora, wanafunzi tunaishia kukaririshwa na walimu wetu wanataka uandike alichokariri yeye kinyume na hapo umefeli na ili akili zetu zisifunguke na kuanza kufikiri sawasawa.. Mfumo mzima wa elimu unatakiwa kuwekwa sawa, na hicho ni kipaumbele cha kwanza cha mh. Edward Lowassa, Kipaumbele kikubwa cha Magufuli ni kugawa Laptops kwa walimu wote nchini kana kwamba ndio hitaji lao.
Fact 7:
Serengeti National Parks ni mbuga bora iliyoshika namba moja kwa Afrika, na Ngorongoro ikiwa namba 5.. Masai Mara ya Kenya ni namba 8. Lakini pia Tanzania tuna Mlima Mrefu zaidi Afrika Mlima Kilimanjaro ambao pia ni kivutio kikubwa cha Utalii..
Lakini maajabu ni kwamba Kenya wanakusanya pato kubwa sana kwenye Utalii kuliko Tanzania. Mwaka 2013 pamoja na matukio ya kigaidi Kenya ilitembelewa na watalii million 1.4 wakati Tanzania yenye amani tele ilitembelewa na watalii million 1.04.. Amani wanayoihubiri CCM na vivutio vyetu vya Utalii bado havijatufaidisha chochote..
Fact 8:
Bandari ya Dar ambayo ina feed Tanzania, Rwanda, Burundi, DRC, Zambia na Malawi ina wastani wa kuingiza Kontena Million 12 kwa mwaka, wakati Bandari ya Mombasa inayo-feed Kenya, Uganda na Sudan pekee inaingiza Kontena Million 22 kwa mwaka.
Hivyo bandari ya Mombasa inayolisha nchi 2 pekee (kwa kiasi kikubwa) inaingiza pato kubwa kuliko Bandari ya Dar ambayo inalisha nchi 5.. Tatizo ni nani?? kama siyo CCM.
Fact 9:
Kiwanda cha General Tyre cha Arusha kilikuwa kinazalisha TYRE bora kabisa za gari ,Kilikuwa na Soko kubwa Afrika Mashariki na kati. Gari zote za Tours zinazotembea porini Afrika Mashariki yote na Afrika ya Kati zilikuwa zinafunga TYRES za GENERAL. Hata wale wapigana vita za msituni huko Kongo na Sudan walikuwa hawaendi kupambana bila kuhakikisha Land Rover yake imefungwa Tyre ya General. Magari ya serikali yote yalikuwa yanafunga Tyres za General..
Kiwanda kilikuwa kinalipa kodi isiyopungua Billion 100 kila mwaka.. CCM wakafanya hujuma kukiua, Wakenya walivyo smart wakaiba ile Technology ya Tyre za General wakafungua kiwanda chao huko kwao kikaitwa YANA Tyre ambaye sasa ndiye Supplier mkubwa wa Tyre Afrika Mashariki na Kati.. Kampeni zinaanza wamejifanya kuifufua General Tyre, Je, wataweza kupambana na Yana Tyres ? Kenyans are always SMART kuliko akili za CCM.
CCM wanasema hapa ni Kazi tu.. hahahaaaa......!!
Fact 10
Yote kwa Yote.. Kenya wametuzidi kila kitu, almost everything..
Mpaka mwaka 2002, Tanzania na Kenya hatukuwa na gap kubwa sana kiuchumi. Kenya wameanza kukimbia kwa Speed baada ya kukiondosha Chama cha KANU madarakani. Watanzania wenzangu, Change is INEVITABLE.. Nchi yetu kwa RASILIMALI tulizonazo tunapaswa kuwa kwenye League na South Africa na Nigeria. Wakenya walipaswa wawe wanazamia hapa TZ kama Wa-Mozambique wanavyozamia kule South Africa.
Mwaka 1992, Uchaguzi Mkuu wa Kwanza wa Vyama vingi ZAMBIA Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zambia alikwenda kwa Rais wa wakati huo wa Zambia KENNETH KAUNDA na kumpa matokeo halisi ya kura zilizopigwa na waZambia na matokeo ya kura zilizochakachul
iwa. Mwenyekiti wa Tume akamwambia KAUNDA wanaenda kutangaza matokeo yaliyochakachuliwa. KAUNDA akawaambia wasubiri, akatoka akaenda bustanini kwake, akapiga magoti akamwomba MUNGU. Kisha akarudi kwa Mwenyekiti wa Tume akamwambia aende akatangaze matokeo yaliyopigwa na Wazambia. TANZANIA tunahitaji busara kama hii iwaingie viongozi wetu, wakubali kutangaza matokeo ya kura zilizopigwa na WATANZANIA.. Viongozi wetu wakumbuke tu, sote tutapita lakini Daima TANZANIA itabakia.[

Umaskini wa Tanzania unasababishwa na mambo matatu makubwa kwa mtazamo wangu.Kwanza ni watawala wetu kukumbatia,kuabudu na kusujudia sera kandamizi za mashirika mumiani ya Btettonwoods yaani WB na IMF ambapo watawala wetu hugeuka. mawakala wa sera hizi za kibeberu zinazofukarishatt nchi yetu.Pili ni kukithiri kwa wizi serikalini,mashirika ya umma,idara na taasisi za serikali na halmashauri.Tatu ni kukosekana kwa uwajibikaji,hasa uzembe,kufanya kazi kwa mazoea na kutojali.
 
Mi nakubaliana na wewe , sehemu moja tu ukawa mmechemsha ni kukubali kuweka watu waliokuwa sehemu ya uozo huo kwa miaka 30, Leo wanasimama wanaisema ccm wakati na wao walikuwa viongozi wakuu na hawa ndio mnataka muwape nafasi za juu , aww hapa mmechemsha ila mengine yote nakubaliana na wewe
 
Sababu kubwa ni lowassa,Rostam la mtajiri wengine walioko nyuma yao kujilimbikizia mali la kuwafanya watanzia pamoja la serikali yao kuwa maskini

Sababu kubwa ni ccm na mtambo wake wa kupika mafisadi wadogo na wakubwa kuanzia ngazi za mitaa hadi taifa
 
Mfumo wa kifisadi umepumbaza watu walionadhamana ya kusimamia na pia kupumbazwa kwa watanzania kumefanya watu wasione na kuelewa namna tunavyoweza kuuondoa umaskini wetu kwa kutumia resources zetu
 
uwezo wa kuyachimba mnao?,technology mnayo ili myachimbe wenyewe.
unadhani mtu aje na vyote hivyo,awekeze mabilioni ya dola kisha nyie mchukue hela?,,,,
 
uwezo wa kuyachimba mnao?,technology mnayo ili myachimbe wenyewe.
unadhani mtu aje na vyote hivyo,awekeze mabilioni ya dola kisha nyie mchukue hela?,,,,

Ni serikali dhaifu ya CCM inashabikia mawazo ya kipumbavu kama yako.

Kwahiyo nchi nyingine za Afrika kama Botswana wana vifaa na utaalamu?
 
wanajamvi amani iwe kwenu. kama ni kusema ukweli taifa letu linafanana na ile nchi ya ahadi ya wana wa israeli, ina kila uzur wa kupendeza na ardhi yake yote ni mali ina madini haina mfano, mito, maziwa na bahar hakika mungu aliziumba mbingu na dunia ametupendelea ila umaskin wetu unatia aibu sana ebu hawa walioko madarakan mda mrefu tuwatoe jaman kwa miaka mitano tujaribu wengine, mana tunadhalilika dunian
 
Serikali ya CCM iliwathamini sana wawekezaji kutoka nje hata ikafikia hatua ya kuwapa miaka 5 kufanya biashara bila kulipa kodi (grace period) lakini raia waTanzania anatakiwa kulipa kodi fast mara tu anapoanza biashara yake bila kujali ni ndogo au kubwa wakati mwingine inatia hasira.
 
Juzi juzi nilifika ofisi za TRA lindi ili niweze kukadiriwa kodi kwaajili ya biashara yangu ndogo niliyotaka kuianzisha, lakini kilichinishangaza ni pale nilipoambiwa niiende bank nikalipe kodi kabla ata sijaanza biashara, tena ni vijana wenzangu wanaoitwa tax officers ndo walikuwa wakinikomalia kwa nguvu zote
 
Unaposema atii wataka anzisha biashara, ni biashara gani weye waweza hata ya kuuza ukwaju?? Profesa Muongo kamwambia Dr Mengi kuwa na vijisenti vyake anachoweza ni kuuza juice tuuu. Yaani, unakadiriwa kodi ya kuzidi hata ile hela yako ya mtaji ili ukimbie tuu usiingie kwenye vitabu vyao vya kodi. Yaani hii ni ajabu kabisa. Badala ya watu kupeleka fedha za kodi zijenge nchi wanaona heri kuzila kuliko kulipia kodi kwani hawaoni inachofanya kodi yao.
 
Back
Top Bottom