Habari ya leo wanajukwaa?
Leo ningependa tushirikishane kidogo au tupeane uelewa juu ya kwa nini uchumi wa Tanzania unakua lakini bado wananchi wengi wanaishi katika dimbwi la umasikini.
Kitu vitu viwili ambavyo ningependa wanajukwaa wenzangu mvielewe.
Kuna kitu kinaitwa KUKUA KWA UCHUMI, kwa tafri isyo rasmi wanaitwa ''ECONOMIC GROWTH''. Economic Growth au kukua kwa uchumi (kwa tafsiri isiyo rasmi na nitaendelea kitumia) ni ile hali ya kuongezeka kwa HUDUMA na BIDHAA zinazozalishwa nchini kwa kipindi fulani.(Hii mjumuiko wa tafsiri mbili za Charles P. Kindleberger na Simon Kuznet.
Kumbe tunaposema kukua kwa uchumi tunazungumzia ile hali ya kukua/kuongezeka kwa uzalishaji wa bidhaa na huduma katika nchi.
Hali hii hupimwa kwa takwimu, kwa mfano uchumi wa pato la ndani la Taifa kwa mwaka 2013 ni trilioni 19.8, mwaka 2014 trilioni 21.2 (kwa robo tatu za mwaka) na mwaka 2015 (robo ya kwanza) ni trilioni 21.9. Ukiangalia takwimu hizo utaona ni kweli kuwa pato la ndani linakuwa siku hadi siku.
KWANINI BADO WATANZANIA NI MASIKINI?
Katika uchumi kuna kitu kingine (ambacho ndio cha pili) kinaitwa ''Economic Development'', kukua kwa uchumi(sio pato la taifa, ingawa lenyewe ni sehemu). Hapa unazungumizia maisha ya watu, ubora wa maisha watu wanayoishi, wanapata mahitaji ya muhimu (Chakula, Mavazi, Malazi, Afya na Ulinzi), Je, binadamu huyo anaheshimika na wengine, anathaminika? Ana uhuru wa kweli juu ya kujiamulia mambo yake?(Ili mradi havunji sheria)?
Kwa hiyo kama mwanadamu ana vitu vitatu yaani
1. Anapata huduma za muhimu kama nilivyoeleza hapo juu
2. Anathaminika na kuheshimika na wengine
3. Ana uhuru wa kweli juu ya kujiamulia mambo yake. Kama haya yote yapo, ndipo tunasema MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA (Msome mwandishi Todaro).
Kwa hiyo, watanzania wanapewa takwimu za kukua kwa uchumi (Pato la Tiafa) sio maisha yao.Kukua kwa uchumi wa kweli ni kuwepo kwa nafasi za ajira, kupungua kwa umasikini na kuwepo kwa usawa.
Yaani wanaelezwa ECONOMIC GROWTH na sio ECONOMIC DEVELOPMENT.
Asanteni.