Kwanini masikini hupenda sifa na matanuzi? Naangalia bunge la UK ukumbi wao ni wa kawaida sana, hauna mbwembwe licha ya utajiri wao.Inakuwaje pale Dodoma ukumbi wa bunge mi wa kifahari as if sisi tuna uwezo mkubwa kiuchumi?
It is human nature ya masikini kujitutumua ili aonekane sii masikini, ndio maana kuna ile methali ya "masikini akipata, ..ta.. hulia mbwata!".

Angalia hata jinsi wenye nazo wanavyoendesha maisha na ulinganishe maisha ya huku kwetu uswazi!, nenda Masaki, Osterbay na Mikocheni na Mbezi beach, kahesabu, guest, bar na vibanda vya chips!. Kule maeneo ya wenye nazo, guest ni za kuhesabika, bar ni za mahoteli, na vibanda vya chips kuku ni vya kutafuta!. Nenda Uswazi, kila kona ni kibanda cha chips kuku, kila kona ni guest!, (sio kwa ajili ya wageni, bali 'mapumziko'), na kila kona ni bar na zote zinajaa!. Kufuatia umasikini uliotopea, masikini hupenda kujifariji kwa ile 'starehe', kula kuku, na kunywa sana bia!.

Familia masikini ndizo zenye watoto wengi kufuatia kujifaiji kwa ile starehe!, makabila masikini ndio huongoza kwa kujitutumua!, hali hiyo ni hata kwa wanawake wetu!, angalia wanawake matajiri wenye uwezo wa kununua na kuvaa dhahabu, utakuta amevaa ka simple chain, bangili moja na hereni!, nenda Uswazi, mtu anavaa micheni kibao, mipente kibao tena mikubwa ya kuonekanika, anatoga masikio mitundu kibao!, tena vingine vya kuazima!, ili tuu aonekane!.

Hivyo ndivyo taifa letu tulivyo, Tanzania ni ka nchi masikini wa kutupwa, lakini tunataka mambo makubwa kwa kujiinua kutaka kufika mbinguni!. Angalia Marekani ji nchi likubwa ajanu, lakini lina mawaziri 6 tuu!. Angalia ka nchi ketu!, hesabu idadi ya mawaziri!. Kati ya mawazii hao 6, watano wanafanya kazi kwenye jengo moja tuu la serikali, Capital Hill, isipokuwa Wazii wa Ulinzi, yeye ndio anafanyia Pentagon!. Sisi kanchi kadogo masiki wa kutupwa, angalia seikali ilivyo tapakaa!.

Waingereza wenyewe licha ya utajiri wao, hawana li rada kama lile walilotuuzia!, walitujengea kutokana na mahitaji yetu!. Ununuzi wa ile Gulf Stream, ni white elephant ili rais wetu aonekane!. Kuna wakati nikiwa newsroom nilipangwa ziara za rais za nje!, rais wa nchi masikini, anasafiri na msafara wa ujumbe wa watu 100!. Wote wanafikia Five Star Hotel!.

Kiukweli umasikini ni sheedah!, umasikini uliotopea ni balaa, na "umasikini mbaya zaidi ni umasikini wa fikra!" Mwl. J.K Nyerere!.

Pasco
 
Tusiangalie kwa macho yawezakana thamani yake ni kubwa kuliko tunavyofikiri.
 
Sasa kwani Tanzania maskini sisi siyo maskini bwana tuna Mali kibao so ukionacho bungeni mwetu ni ishara ya utajiri wetu TE="Gulwa, post: 16661469, member: 11032"]Kwanini masikini hupenda sifa na matanuzi? Naangalia bunge la UK ukumbi wao ni wa kawaida sana, hauna mbwembwe licha ya utajiri wao.Inakuwaje pale Dodoma ukumbi wa bunge mi wa kifahari as if sisi tuna uwezo mkubwa kiuchumi?[/QUOTE]
Sasa
 
Nashindwa kuamini kuwaona wananchi wa Nchi yenye Rasilimali nyingi kuliko nchi yeyote Afrika Mashariki Na Kati ni Masikini walala hoi.Nchi ina Gesi, Mbuga za wanyama, Bahari, Maziwa,Mlima Kilimanjaro, Mabonde yenye rutuba, Madini aina mbalimbali lakini Watanzania in Masikini.Ukienda vijijini hali ni mbaya zaidi watu wanaishi kwenye Nyumba za tembe, nyasi Na udongo Na ni miaka zaidi ya 54 toka Uhuru.Jamani hivi tatizo in nini?

Mie nadhani kuna haja ya kujitathimini ili tujue tumekosea wapi Na nini.Pia in wakati muafaka Viongozi wetu wakakubali tuwe Na Midaharo ya Kitaifa bila kujali vyama wananchi wakiongozwa Na wachumi wetu hata ikibidi wa nje waalikwe tujadili kwanini pamoja Na utajiri uliopo watanzania in masikini hatuwezi kupiga hatua Kwa kulipa kodi kutoka Kwa watanzania masikini.

Naomba michango yenu Kwa faida ya Tanzania.
 
Bad Gorvenance
Tatizo mkuu ni watawala wetu, ambao hata kidogo hawakuonesha nia ya dhati ya kuwasaidia watz wenzao, wamezifanikisha na kuzitajirisha familiya zao, wee itazame SA nchi changa tulioisaidia kufikia uhuru wao, Tazama china 1960's we were both the same chakushangaza wametuovertake na kuwa moja kati ya mataifa Tajiri duniani.
 
Tatizo ni Rushwa.
Pamoja na viongozi "wasomi " wasio na uchungu
Na nchi yao bali matumbo yao. Na wana wathamini wazungu kuliko wa TZ wenzao.

Nikimanisha atakuja mzungu mwenye elimu duni
Watamuamini na kuingia mikataba ya kiuholela.
Akija Muafrica na idea nzuri tu na mwenye elimu hatasikilizwa.

Labda uwe na utajiri wa Dangote. Hapo utasikilizwa.
 
NIGERIA yenye uchumi wa MAFUTA, ANGOLA pia yenye uchumi wa MAFUTA Hali za wananchi ni mbaya Tena sehemu nyingine kuliko TANZANIA.
 
USA na UINGEREZA nchi hizo pia zina watu wenye hali mbaya kabisa....
Ongezeko la OMBAOMBA na WATU WASIO NA MAKAZI (homeless) ni kubwa
 
Asilimia 90 ya watanzania ni wavivu hawafanyi kazi kwa nguvu...asilimia 99 ya wasomi wa tanzania ni tegemezi wote wanawaza kutumwa(kuajiliwa-utumishi) kuliko kujituma(kujiajiri) kwa maana hiyo ni ngumu wananchi kuendelea sababu hata wasomi waliotakiwa kua mfano wanakatisha tamaa wananchi
 
Kwahiyo unataka kusema nchi zenye utajiri mkubwa, wananchi wake kwa % kubwa wamejiajiri?????[emoji144]
 
Kwahiyo unataka kusema nchi zenye utajiri mkubwa, wananchi wake kwa % kubwa wamejiajiri?????[emoji144]
ndiyo kiongozi,kuna kipindi Dubai ilibidi iombe wasomi wake waajiliwe na serikali angalau mwaka mmoja kabla ya kujiajiri maana serikali ilikosa watumishi kabisa...Marekani yenyewe iliamua kulegeza masharti ili wahamiaji waweze kupewa uraia mapema ili waajiliwe kufanya kazi serikali maana nchi ile watu wengi wanajiajiri sana hasa wasomi
 

Ni nani amekwambia huu upuuuzi kwamba Tanzania yetu ndiyo nchi tajiri klk zote? Hivi ninyi watu ni lini mtaacha kujidanganya? Hizo Takwimu za kwamba TanZani yetu ndiyo nchi tajiri klk zote mnazipata wapi?

TanZania yetu ni nchi ya kawaida sana linapokuja swala la Rasilmali, ndiyo tuna Rasilimali nyingi lkn siyo za kipekee, kwa maana ya kwamba wengine pia wanazo, Kongo wana rasilimali nyingi tu, Uganda wana rasimali nyingi tu, Kenya wana rasilimali, Msumbiji wana Rasilimali, Malawi na hata Rwanda wana madini mengi tu kama ulikuwa haujui, hivyo acheni hizo blah blah TanZania yetu ni nchi ya kawaida sana tu!
 
Nadhani kabla ya kuanza kujiuliza kwanini nchi yetu maskini anza kwanza kujiuliza kwanini wewe ni maskini na unaishi kwenye nchi yenye rasilimali nyingi,umezitaja rasilimali zote ila hamna hata moja uliyo itaja maligafi yake inapatikana dar,nchi yetu itakuwa tajiri iwapo tu watu kama nyinyi wenye mawazo ya kulalamika kila siku mtakapo chukua hatua na kuzifwata hizo rasilimali unazozitaja na kuzifanyia process then kuziuza,then baada ya kufanya hivyo ludi tena hapa tuone kama utakuwa na hizo complain.
 
Umasikini wa Tanzania umeletwa na CCM.
Siku ccm akitoka tukapata kiongozi mwenye maono na kujua ni nini cha kufanya basi tutapiga hatua na kufika uchumi wa kati.
Lakini tukiendelea kujidanganya na hii ccm eti itatukomboa wakati wanalindana ni sawa na kusubiri meli airport
 
Nashindwa kuamini kuwaona wananchi wa Nchi yenye Rasilimali nyingi kuliko nchi yeyote Afrika Mashariki Na Kati ni Masikini walala hoi. Kwa kulipa kodi kutoka Kwa watanzania masikini.

Naomba michango yenu Kwa faida ya Tanzania.

Vyote ulivyosema ni nani wa kuwekeza uko kama si wewe ambaye unasema sisi ni masikini...Tunalalamika sisi ni masikini tuna kila kitu ukimuuliza mtu we jitiada yako nini? amna.........

Mwisho wa siku unategemea nani wa kukutoa kwenye uo umasikini ikiwa ata public company kuanzisha kutoa mlicho nacho chini jitiada amna so unafikiri nini kinafuata.... na si kila tulicho nacho ni investable kwa mtu kutoka nje kuja kuwekeza nchini.....
 
•Tunawaona katika ujenzi wa mabarabara.
•Tunawaona wakitujengea mashule yenye nyufa.



NO TIME OF EXPERIMENTS ON PUBLIC FUNDS,Eti tuwajaribishe wataalamu wetu kwanza.../
•kinachotakiwa hapa ni "COMMITMENT"kazi hii naiweza,nitakaposhindwa nitafidia hasara na muda.
 
Mkuu mbona wengi tu hawafahamu, hata baadhi ya wazee maarufu hawafahamu
 
Mh.Rais amesema Nchi Yetu in Tajiri,Rais Kagame juzi amesema Tanzania in nchi Tajiri Mimi najiuliza kwanini Watanzania ni Maskini sana?Hivi kinachosababisha hali hiyo ni nini?Wachumi wetu mbona hamuisaidii Tanzania Na watanzania kuwa Na hali nzuri kutokana Na nchi yao kuwa Tajiri kweli wachumi wetu mmekubali Na nyie mwiishi kimaskini ? Haya bwana .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…