Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
It is human nature ya masikini kujitutumua ili aonekane sii masikini, ndio maana kuna ile methali ya "masikini akipata, ..ta.. hulia mbwata!".Kwanini masikini hupenda sifa na matanuzi? Naangalia bunge la UK ukumbi wao ni wa kawaida sana, hauna mbwembwe licha ya utajiri wao.Inakuwaje pale Dodoma ukumbi wa bunge mi wa kifahari as if sisi tuna uwezo mkubwa kiuchumi?
Angalia hata jinsi wenye nazo wanavyoendesha maisha na ulinganishe maisha ya huku kwetu uswazi!, nenda Masaki, Osterbay na Mikocheni na Mbezi beach, kahesabu, guest, bar na vibanda vya chips!. Kule maeneo ya wenye nazo, guest ni za kuhesabika, bar ni za mahoteli, na vibanda vya chips kuku ni vya kutafuta!. Nenda Uswazi, kila kona ni kibanda cha chips kuku, kila kona ni guest!, (sio kwa ajili ya wageni, bali 'mapumziko'), na kila kona ni bar na zote zinajaa!. Kufuatia umasikini uliotopea, masikini hupenda kujifariji kwa ile 'starehe', kula kuku, na kunywa sana bia!.
Familia masikini ndizo zenye watoto wengi kufuatia kujifaiji kwa ile starehe!, makabila masikini ndio huongoza kwa kujitutumua!, hali hiyo ni hata kwa wanawake wetu!, angalia wanawake matajiri wenye uwezo wa kununua na kuvaa dhahabu, utakuta amevaa ka simple chain, bangili moja na hereni!, nenda Uswazi, mtu anavaa micheni kibao, mipente kibao tena mikubwa ya kuonekanika, anatoga masikio mitundu kibao!, tena vingine vya kuazima!, ili tuu aonekane!.
Hivyo ndivyo taifa letu tulivyo, Tanzania ni ka nchi masikini wa kutupwa, lakini tunataka mambo makubwa kwa kujiinua kutaka kufika mbinguni!. Angalia Marekani ji nchi likubwa ajanu, lakini lina mawaziri 6 tuu!. Angalia ka nchi ketu!, hesabu idadi ya mawaziri!. Kati ya mawazii hao 6, watano wanafanya kazi kwenye jengo moja tuu la serikali, Capital Hill, isipokuwa Wazii wa Ulinzi, yeye ndio anafanyia Pentagon!. Sisi kanchi kadogo masiki wa kutupwa, angalia seikali ilivyo tapakaa!.
Waingereza wenyewe licha ya utajiri wao, hawana li rada kama lile walilotuuzia!, walitujengea kutokana na mahitaji yetu!. Ununuzi wa ile Gulf Stream, ni white elephant ili rais wetu aonekane!. Kuna wakati nikiwa newsroom nilipangwa ziara za rais za nje!, rais wa nchi masikini, anasafiri na msafara wa ujumbe wa watu 100!. Wote wanafikia Five Star Hotel!.
Kiukweli umasikini ni sheedah!, umasikini uliotopea ni balaa, na "umasikini mbaya zaidi ni umasikini wa fikra!" Mwl. J.K Nyerere!.
Pasco