Tumekuwa tukiambiwa kuwa nchi yetu Tanzania ni nchi masikini, tena umasikini wake ni ule uliopindukia. Wengi wetu hatujawahi kulinganisha umasiki wa nchi yetu na nchi zinazotajwa kuwa ni nchi tajiri. Kwa kifupi, hatujui utofauti uliopo kati ya nchi tajiri na nchi masikini kwa sababu hatujawahi kwenda kwenye nchi zilizoendelea tukaona jinsi maisha yanavyokuwa ukilinganisha na hapa nyumbani.
Tunaambiwa kuwa Tanzania ni nchi tajiri, tena ni nchi oliyojaaliwa kuwa na kila kutu kinachoweza kuifanya iwe miongoni mwa nchi tajiri. Lakini bado ni nchi masikini.
Je, kwa mtazamo wako, ni kitu gani kifanyike ili nchi yetu Tanzania iwe ni nchi Tajiri kama zilivyo nchi tajiri duniani? Kama kwa sasa hatunufaiki na Tanzania kuwa nchi masikini, je ikiwa nchi tajiri tutanufaika na nini? Je kuna haja ya kuikomboa nchi yetu ili ifikie kuwa nchi tajiri kama zilivyo nchi tajiri duniani. Nini kifanyike?
Tupia mchango wako hapa unaoona tukifanya hivi Tanzania itakuwa inchi Tajiri. Je, rais aliyepo madarakani ataweza kutimiza matakwa ya mapendekezo yako?