Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Hakuna wasomi nchi hii ni wote ni wababaishaji msomi utakubali ukuu wa wilaya uache kuifanyia Kazi taaluma yako?
 
unajua wa TZ wanafikili umasikini au utajiri ni kua na Gari kunywa Bear sana hapa kinacho takiwa kwa binadam ni kuamua kile unacho kiwaza kwa wakati muhafaka mfano mwaka kesho nataka kufanya A.B.C. yanawzekana kuyafanya lakini je utamaduni wa Baget tunao je tunajua kupanga na kuamua
...? tofauti na watu Weupe Mfano hai we Angalia hata Watalii wanaokuja hapa wengi sio matajiri lakikini walipanga na kuwekeza kati ya watalii 20 ni 1 ndio mweusi wanao panga na kuamua watu weusi tuna matumizi ya Fujo na ya ovyo hata ukiwa na mayai 20 tunataka tuyatumie siku 3 kilamtu akujue leo umesaza wenzetu weupe hayo 20 atakula kila siku 2 mpaka yaishe hspo ndipo tunapo kosea mipangilio hatuna ila ni ufahali na kujionyesha
 
Usiseme Watanzania ni MASKINI,Sema Watanzania WEUSI ni MASIKINI Wa kutopea sababu kubwa ni hizi.
1.Ni wavivu,wanapenda kukaa tu kupiga POROJO NA KULALAMIKA.
MTU ANAKAA 24/7 ANATUKANANA MTANDAONI.
In short WATU WEUSI WANA UMASIKINI KWENYE DNA ZAO.
 
VIJANA WA TANZANIA WALIVYO

Kijana wa miaka 17 nchini China ana shahada ya Udaktari
Kijana wa maika 17 nchini Japan ana shahada ya makenika
Kijana wa miaka 17 nchini Marekani ana utajiri kupitia kipaji chake
Kijana wa miaka 17 nchini Urusi ni mwana jeshi mwenye eshima yake
Kijana wa miaka 17 nchini Uingereza ni mwanasheria
Kijana wa miaka 17 nchini Brasil ni mwanasoka
Kijana wa miaka 17 nchini Tanzania ni Admin wa magroup 7 kwenye mitandao ya kijamii.
 
Tatizo Wasomi wa nchi hii tatizo wapo very reluctant.
Ukisema wasomi ambao idadi yao haifikii hata 5% ina maana hawa wafanye kazi kwa niaba a 95% wasio na elimu na wasiopenda au walionyimwa elimu ili nao kuwa 'wasomi'.
Kwa maana hiyo hapa ni kuwa tatizo letu ni ujinga na hilo tukubali makosa ya Mwalimu huku tukimuenzi kwa kuutambua UJINGA kama mmoja wa maadui wakuu wa Mtanzania.
Watu waelewa (mfano Kenya au SA) wanaweza kutambua haki ya kikatiba ya kuandamana na kustage maandamano ya kuwakataa wakuu wa tume ya uchaguzi. Hii inapelekeaa baadhi yao kupigwa risasi za moto na kufa lakini mwishowe rais anakubali kuunda tume kupata mwafaka wa tatizo. Sababu ya uerevu wa watu hawa wanajua kuwa huwezi kuwaua wote kwa kudai wanachostahili, wanauawa kama 15 huku matokeo ya kukubaliwa madai yao yakiokoa maelfu ya wanaokufa na ambao wangekufa kwa umasikini na matokeo ya ufisadi.
"elimu, elimu, elimu" ...huyu jamaa pamoja na kuwa na rekodi zisizoridhisha lakini hapa alinena!
 
Kwa sababu neema hizo zinaishia kujaza matumbo ya wachache, ndio maana hata nisikie Tz kumegunduliwa mvua ya almasi hata moyo haunipasuki na kusubiria mabadiliko.
 
Tumekuwa tukiambiwa kuwa nchi yetu Tanzania ni nchi masikini, tena umasikini wake ni ule uliopindukia. Wengi wetu hatujawahi kulinganisha umasiki wa nchi yetu na nchi zinazotajwa kuwa ni nchi tajiri. Kwa kifupi, hatujui utofauti uliopo kati ya nchi tajiri na nchi masikini kwa sababu hatujawahi kwenda kwenye nchi zilizoendelea tukaona jinsi maisha yanavyokuwa ukilinganisha na hapa nyumbani.

Tunaambiwa kuwa Tanzania ni nchi tajiri, tena ni nchi oliyojaaliwa kuwa na kila kutu kinachoweza kuifanya iwe miongoni mwa nchi tajiri. Lakini bado ni nchi masikini.

Je, kwa mtazamo wako, ni kitu gani kifanyike ili nchi yetu Tanzania iwe ni nchi Tajiri kama zilivyo nchi tajiri duniani? Kama kwa sasa hatunufaiki na Tanzania kuwa nchi masikini, je ikiwa nchi tajiri tutanufaika na nini? Je kuna haja ya kuikomboa nchi yetu ili ifikie kuwa nchi tajiri kama zilivyo nchi tajiri duniani. Nini kifanyike?

Tupia mchango wako hapa unaoona tukifanya hivi Tanzania itakuwa inchi Tajiri. Je, rais aliyepo madarakani ataweza kutimiza matakwa ya mapendekezo yako?
 
Nchi ina mali lakini maskini.
Uchumi bado unadag hakuna ukombozi.
Viongozi wapo lakini wengi wao wapo kimaslahi.
Je cc wanajamii tutaishije?
 
Kwa muda mrefu nimekua nikitafakari mitizamo yetu kama watanzania ikoje katika kupambanua mambo mbalimbali, nimegundua adui wetu mkubwa kwa sasa ni ushabiki kwa kundi fulan pasipo kujali athari za kundi hilo.

Niende kwa mada husika. Tanzania tumekua mskin ambapo kuna wakati mwingine viongoz walipoulizwa sababu ya sisi kuwa maskin wakasema hata wao hawajui kwann sisi ni maskin. Sasa je kwann Tanzania ni maskin? Hebu tujiulize tena.

Je umaskini wa Tanzania umesababishwa na huyu anayeitwa mheshiwa Lowassa. Fisad?

Kwa sasa kila ukionekana ni upinzan et umekua mtetezi wa mafisadi. Kisa Lowassa yuko upande wako. Je tatizo la nchi hii ni Lowassa? Amekua upinzani kwa sasa ni takriban mwaka. je ndani ya muda huo ndipo wana ccm wametambua huyu ni tatizo ndan ya Taifa?

Je huyu Lowassa ndio chanzo cha umaskini wetu? Kwann tunapenda kutoa majibu mepesi kwenye maswali magumu? Kwa nn hatutak kujadili tatizo la taifa letu bila ushabiki wa makundi yetu kama taifa?? Je kabla ya Lowassa hajawa kiongozi Tanzania ilikua tajili na yeye ndio kaifilisi? Je Lowassa akiondoka Tz asiwepo kabisa Tz tutakua kama ulaya? La hasha. Sisi umaskin uko kwenye akili zetu. Niwakumbushe kuna wakati marekan iliwaaminisha walimwengu, Sadam hussen ni tatizo. Leo hii hayupo matatizo ya Iraq ni makubwa kuliko awali.

Tatizo kubwa liko kwenye akili zetu. Tumeruhusu akili ndogo ifanye maamuzi kwa niaba yetu. Tumeruhusu wanasiasa watuamulie hatima ya Taifa letu.
Mara zote tumeruhusu watu wale wale watuamulie hatima yetu. Yaan maswali yale yale majibu yale yale tunategemea matokeo tofaut.

Umaskini wetu unatokana na kuruhusu viongoz wetu watuamulie namna ya kuendesha nchi na sio sisi wananchi kuwapa viongoz wetu mwongozo wa kufuata. Kama taifa hatuna mpango wa Muda mrefu wala mfupi ambao viongoz wanatakiwa waufate. Bali viongoz wanatuletea mipango kede kede huku sisi bila kuuliza ule mpango wa awali umeishia wap? Leo hii tunaambiwa Tanzania ya wiwanda, mpango wetu kama taifa kwa hivyo viwanda hakuna. Et wawekazaji waje wajenge, je wasipokuja? Tumeruhusu akili ndogo iamue mambo makubwa!

Mtizamo wangu tukitaka kujikomboa hapa tulipo kama taifa tukubali kujadiliana na kukubali mawazo ya watu tofaut tofaut pasipo kujali itikad yake. Cheo chake wala dini yake.
Sahz tumekua na uadui mkubwa kat yetu. Wazo jema likitoka upinzani linakua baya, likitoka ccm linakua baya. Likitoka kwa mwanadin fulan ambaye jana alitupinga basi kuanzia hapo mawazo yake yote yatakua mabaya! Hatuwezi kufika kama taifa.

Tuondoe dhana ya kufikiri tatizo la nchi hii ni Lowassa. Leo hii Lowassa hata tukimfilisi asibakie na hata mia mbovu! Hakuna kitakacho badirika katika nchi yetu. Tatizo liko kwa viongoz wetu wanajiona wao pekee ndio wenye kuamua hatima yetu. Mfumo mzima ndio tatizo. Leo hii ukiingizwa pale ukawa na mawazo tofaut na yao utaondolewa. Utaonekana ni msaliti. Hii nchi ni yetu sote hakuna mwenye hati miliki.

Mwisho tupiganie katiba mpya itupe mamlaka wananchi ya kuamua hatima yetu. Na kamwe tusiruhusu watu wale wale majibu yale yale yalete matokeo tofaut.
 
Mkuu,C.C.M na Serikali Wanapenda Blame Games!Upenda Kuwasingizia Watu Fulani Madhaifu Yao!
Kama Haitoshi Walienda Mbali Hata Kuianzisha Mahakama ya Mafisadi Ili Tu Kuwachota Watu Akili na Kuwaaminisha Kuwa Lowasa ni Fisadi!
Ila ebu ona leo,Washampeleka Mahakamani?
 
mahakama ya mafisadi ianze Na Lowassa, vinginevyo majengo watafugia popo.
.....Lissu aliwaambia, "mbona mahakama hiyo IPO?".
 
Msijitoe fahamu, miaka yote 8 mlikuwa mnasema chanzo cha umaskini wetu ni nini? Kitu gani kiliwapeleka Mwembeyanga?
 
Ni wimbo maarufu kuliko hata wimbo wa taifa - umasikini. Inafahamika wazi jinsi kila serikali inayokuwa madarakani inavyokuja na maneno mengi na mambo chungu nzima yanayoitwa "mikakati ya kupambana na umasikini" lakini miaka nenda rudi umasikini wa Mtanzania unazidi kuongezeka.
Ziko sababu kadhaa za kwa nini watu wetu wengi ni masikini wa kutupa lakini niongelee chanzo kikuu kimoja tu cha ufukara huu. Taifa lolote ambalo halina nia au haliko tayari kuboresha vipato vya kaya zake (household incomes) haliwezi kushinda vita dhidi ya umasikini.
Hapa nchini serikali ndiyo muajiri mkuu lakini viwango vya vipato vya wafanyakazi wake ni mzaha mtupu, na hii imesababisha hata sehemu zingine binafsi zilizoajiri watu kuwalipa mishahara midogo mno yenye mateso. Katika hali ya kawaida kipato cha familia kinatakiwa kikidhi mahitaji yote muhimu na ibaki akiba kila mwezi ambayo mwisho wa mwaka familia inaweza kuitumia kwa mambo yao binafsi ya kujiliwaza (leisure) kama vile kuamua kusafiri kwenda hata nchi jirani kutembea.
Ni kawaida kusikia watu wakisema kuwa Watanzania hatupendi utalii wa ndani, lakini binafsi naamini siyo kutokupenda bali ni kutokuwa na uwezo kifedha. Serikali za nchi hii zimetengeneza tabaka kubwa mno la mafukara ambao wamechotwa akili na kuaminishwa kuwa nchi yetu ni masikini na hali yao ya maisha ndivyo Mungu alivyowapangia. Hakuna uongo ulio mkubwa kuliko huu.
Kwa kumalizia niseme tu mpaka pale ambapo vipato vitaangaliwa upya na sheria za ajira kubadilishwa ili zimpe nguvu mfanyakazi tutaendelea kuwa taifa masikini mpaka mwisho wa dunia.
 
Kweli kabisa mkuu hasa hapo kwenye sheria za ajira hapo ni
Shidaa.
Wasomi ni wengi hawana kazi za kueleweka na wengine wapo tuu mtaani.
Ambao ni nguvu kazi ya Taifa.
 
Back
Top Bottom