Mimi nataka u=kuelimika tu. Kulikuwa na haja gani ya kuandika ' hatutakuja' Kwa nini kichwa cha habari hiki kisingetosheleza " Kwa nini hatutaushinda umaskini " hiyo kuja imeongeza nini? Au unafasiri kutoka Ki....Haya?
 
Mimi nataka u=kuelimika tu. Kulikuwa na haja gani ya kuandika ' hatutakuja' Kwa nini kichwa cha habari hiki kisingetosheleza " Kwa nini hatutaushinda umaskini " hiyo kuja imeongeza nini? Au unafasiri kutoka Ki....Haya?
Nimetumia neno "hatutakuja" kwa sababu mantiki yangu ilizingatia kipimo dhahiri cha muda, yaani ninamaanisha kuna malengo huwa yanawekwa kwamba ikifika mwaka fulani tutakuwa tumefanikiwa jambo hili au lile. Sasa basi kwa sababu serikali zetu ni za miaka kumi kumi na kila moja inadai kupambana na kuumaliza umasikini, hoja yangu imezingatia hilo.
Ningesema "hatutaushinda" ingeleta picha ya kwamba basi hata juhudi nilizozitolea mfano hazihitajiki.
 
Series to work on:-

1) Elimu ya Vitendo

2) Mapinduzi ya Kilimo

haswa pembejeo kama tractors, planters ba harvesters na mbegu bora.

3) Nishati,

haswa gesi na umeme.

4) Viwanda vikubwa

5) Teknolojia na Skills,

Kwa vijana wa kitanzania..hata kwa kusomeshwa nje kisha warudi nchini na kupewa nafasi

6) Kazi /Utendaji zaidi kuliko Siasa za vyama.
 

Hard to swallow, ila umejitahidi. Ni miongoni mwa waandishi wachache humu wenye mantiki!
 
Kwanza lazima niweke wazi kwamba Tanzania ni kati ya nchi 30 masikini zaidi ulimwenguni.
Kwanini Tanzania ni masikini?
Tanzania ni masikini kwa sababu ya mambo makuu mawili

1: Ability in thinking for change for both Leaders and citizens.
Uwezo wa Kuplan kwa viongozi wa kitanzania kwenye mambo ya maendeleo na kuzisimamia hizo plan zao uko chini mno muda mwingi wanautumia kuhubiri siasa pasipo kufanya kazi za kimaendeleo .
Kama ilivyo kwa binadamu tumepewa akili 100% lakini katika theory za kibinadamu unapoweza kutumia akili yako hata kwa 25% kabla uwe mweu unaweza kuwa umeshafanya jambo angalau hata moja la nchi au dunia kukukumbuka.

Hata mnaosoma Vitabu ukipitia "Thinking for change" cha John Maxwell utanielewa kidogo namaanisha nini.
"Taifa limeamua kumuacha mtu mmoja alisaidie kufikiria wakati nchi ina watu zaidi ya 50milion +

Anatutengenezea vicious cycle of poverty na sisi tunamwangalia tu.......tuendelee kuwa masikini wa vipato je tutakuwa na akili wakati tuna umasikini wa kipato na njaa ambayo inatokana na kuishi chini ya dollar moja?

Tunazunguka na kurudi pale pale clockwise and anticlockwise.
Kwa style hii tutaendelea kubadilisha marais hata aje Malaika kutoka mbinguni tutashindwa tu.

Sera ya Serikali haitakiwi kuwa Sera ya chama inatakiwa kuwa Sera ya taifa ndani ya Katiba ya nchi au Vitabu vya Sera.
Ndio maana unaona Sasa hivi tunacheza na aina zote za vicious cycle kwa sababu ya kutokua na Sera ya taifa ambayo tunaifuata kabla hata na baada ya ya uchaguzi.

A: Supply side of vicious cycle:
Low income - Low saving - low investment - low productivity- low income
Kama kipato ni kidogo - tutawezaje Ku save - tutawezaje kuwekeza - Tusipowekeza tutapataje product jibu ni hatutapata ndio maana tutaendelea na kuwa na kipato kidogo hivyo kuendelea kuwa masikini.



B : Demand side of vicious cycle:
Low income - low demand - low investment - low productivity then low income
Kutoka kwenye kipato chetu kama ni kidogo ,hatutanunua vitu kuliko kipato chetu,tutawekeza kidogo, na kuzalisha kidogo tutarudi palepele kipato chetu kitakuwa kidogo.



C : Vicious cycle of market imperfections


Na mpaka hapo utagundua ni kwanini biashara imekuwa ngumu kufanyika Tanzania sasa hivi .

2: Poor utilization of natural Resources:
Hili ni tatizo la Africa karibu yote lakini kwa nchi yetu imekuwa to much.
Kwa shehena ya madini tuliyonayo tungeweza kuacha kufanya biashara nyingine kama nchi tukawa tukiuza madini tu na tukatajirika.

Kwa gesi tuliyonayo tungeweza kuuza gesi tu tukatulia hata kwa miaka 5 bila kufanya biashara yeyote na nchi ikaendelea..
Kwa Maji tulionayo tungeweza kuwekeza kwenye Kulimo, ufugaji na Uvuvi tusifanye kazi yeyote na tutaendelea.

Kwa utalii tulionao Milima,mabonde,mbuga za wanyama ,Fukwe za Bahari tungeweza kuwekeza kwenye utalii bila kufanya kitu kingine na tungetoboa maisha yangeenda . Lazima tuamue kuchagua tunaanza na kipi ambacho tutakifanya kwa ufanisi wa hali ya juu kuliko kufanya juu juu kwa kulukia mambo....

Mfano ununuzi wa ndege ungekuja moja kwa moja na plan ya kupanua viwanja vya ndege vilivyopo karibu na maeneo ya utalii ili utalii ufanye kazi pamoja na Usafirishaji.

Nafikiri utakuwa umepata mwanga kwa nini Tanzania ni masikini na kwa nini tutaendelea kuwa masikini miaka mingi ijayo kama hatutachukua hatua na kuwa specialization "
Kwani nchi zote zilizopiga hatua za kimaendeleo zime Specialize kwenye mambo Fulani.....
Israel ni nchi iliyopo kwenye jangwa lakini inaendeshwa na kilimo cha matunda.

Isome South Korea
Isome China
Isome Singapore
Isome Malaysia

Mungu ibariki Tanzania.
 
Duuuuh haya mambo mpaka uwe mchumi kiasi kuyachambua
 
Mataifa uliyoyatolea mifano ni mataifa ya viwanda, ni wazalishaji....wanauza kuliko kununua.

Na wanauza man made products, kwa hiyo wanauwezo wa kuwepo sokoni na kuuza kwa muda mrefu.

Sasa wewe unasema tuwe kama wao kwa kuuza natural resources(mf. madini)? mimi sikubaliani na wewe, nafikiri tungeanzisha viwanda ili tuuze bidhaa kamili na siyo malighafi itokanayo na maliasili.

Sera ya Magufuli ya Tanzania ya viwanda ni nzuri kwa nchi yetu ingawa nadhani ameikacha.
 
Umasikini utaendelea kuweko kwasababu watafiti na maprofesa na doctors wachumi wote wamekuwa wachumia tumbo na kujipendekeza kwa chama tawala na kusahau kutumia Elimu yao kuwasaidia Watanzania.

swissme
 




Tatizo ni mifumo yetu ya kielimu na mapokeo yetu. Kubadilika toka umasikini kwenda kwenye utajiri ni fikra na si vitu tumilikivyo.
Nakubaliana nawe kwenye ufikirivu mdogo unaoongozwa na ubinafsi.
 
Hapo ndipo tunakosea haitakiwi kuwa Sera ya Magufuli inatakiwa kuwa. Sera ya taifa
 
Umasikini utaendelea kuweko kwasababu watafiti na maprofesa na doctors wachumi wote wamekuwa wachumia tumbo na kujipendekeza kwa chama tawala na kusahau kutumia Elimu yao kuwasaidia Watanzania.

swissme
Yes exactly hili nalo ni tatizo kubwa sana msomi kiwango cha profesor anagombea abaki kwenye kiti chake kwa garama yeyote ........

Baada aandae business plan aende bank wampe mkopo ajenge chuo awe lecture wa uchumi.....
 
Hapo ndipo tunakosea haitakiwi kuwa Sera ya Magufuli inatakiwa kuwa. Sera ya taifa
JIBU NI HILI TU AMBALO NDIYO UKWELI....

UMASKINI TANZANIA UNATOKANA NA KUWEPO NA VIONGOZI AMBAO SIYO WAADILIFU,WAONGO,MAFISADI,WANAFKI

OVA
 
Umasikini utaendelea kuweko kwasababu watafiti na maprofesa na doctors wachumi wote wamekuwa wachumia tumbo na kujipendekeza kwa chama tawala na kusahau kutumia Elimu yao kuwasaidia Watanzania.

swissme


Hao maprofessors na doctors wamefundishwa kutafuta ajira na si kutengeneza mifumo ya ajira. Kuwalaumu ni sawa na kumlaumu samaki kuishi majini. Tatizo ni malengo/mitazamo ya elimu zetu.
 
Hapo ndipo tunakosea haitakiwi kuwa Sera ya Magufuli inatakiwa kuwa. Sera ya taifa
Mkuu una mawazo mazuri sana.Kwa sasa hatuna sera za taifa(kama nimekosea nirekebishwe) ndio maana kila anayekuja anakuja na yake.

Nchi kama TZ tulitakiwa tuwe na sera za taifa zilizobeba malengo ya kimaendeleo ya taifa walau kwa miaka 50. Yaani kwa kila Rais anayekuja akute kuna sera za taifa za kutekeleza, ndipo achanganye na za chama chake plus na za kwake mwenyewe.

Lakini hicho kitu kwa sasa hakipo ndio maana kila anayekuja anakuja na yake.Ilitakiwa Rais akiingia madarakani awe ni wa CCM au CDM akute sera za taifa za kutekeleza.

Tatizo hizo sera zitaandaliwa vipi bila kuingiza itikadi za kichama na kimasilai?
 
Hueleweki,
Kwa karne ya Sasa Inawezekana kwenda nayo yote na ukafanikiwa.
Mbona plan ya ndege na viwanja imetamkwa na Mkuu wa nchi na budget ipo kwa maelezo yake. Au huwa ufuatilii taarifa rasmi.
Kwa nini Low income, Low Suppy Low Purchasing power. Je unauhakika hii hali ni temporary au Permanent
 
Yes exactly hili nalo ni tatizo kubwa sana msomi kiwango cha profesor anagombea abaki kwenye kiti chake kwa garama yeyote ........

Baada aandae business plan aende bank wampe mkopo ajenge chuo awe lecture wa uchumi.....
chukua mfano huyu jamaa ni mchumi wa juu PHD.check hapo utafikiri mwizi ananyemelea kukwapua simu

swissme
 
Tuna kituo cha uwekezaji Tanzania ,Tuna wizara ya mipango chini ya wizara ya fedha ,Tuna TBS tuna taasisi ya vyuo zinazo Fanya research huru zisizofungamana na upande wowote hawa tukiwatumia kwa pamoja watengeneze taasisi moja inayoweza kuishauri Serikali jinsi ya kutengeneza Sera endelevu....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…