Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,672
- 1,814
Ni wimbo maarufu kuliko hata wimbo wa taifa - umasikini. Inafahamika wazi jinsi kila serikali inayokuwa madarakani inavyokuja na maneno mengi na mambo chungu nzima yanayoitwa "mikakati ya kupambana na umasikini" lakini miaka nenda rudi umasikini wa Mtanzania unazidi kuongezeka.
Ziko sababu kadhaa za kwa nini watu wetu wengi ni masikini wa kutupa lakini niongelee chanzo kikuu kimoja tu cha ufukara huu. Taifa lolote ambalo halina nia au haliko tayari kuboresha vipato vya kaya zake (household incomes) haliwezi kushinda vita dhidi ya umasikini.
Hapa nchini serikali ndiyo muajiri mkuu lakini viwango vya vipato vya wafanyakazi wake ni mzaha mtupu, na hii imesababisha hata sehemu zingine binafsi zilizoajiri watu kuwalipa mishahara midogo mno yenye mateso. Katika hali ya kawaida kipato cha familia kinatakiwa kikidhi mahitaji yote muhimu na ibaki akiba kila mwezi ambayo mwisho wa mwaka familia inaweza kuitumia kwa mambo yao binafsi ya kujiliwaza (leisure) kama vile kuamua kusafiri kwenda hata nchi jirani kutembea.
Ni kawaida kusikia watu wakisema kuwa Watanzania hatupendi utalii wa ndani, lakini binafsi naamini siyo kutokupenda bali ni kutokuwa na uwezo kifedha. Serikali za nchi hii zimetengeneza tabaka kubwa mno la mafukara ambao wamechotwa akili na kuaminishwa kuwa nchi yetu ni masikini na hali yao ya maisha ndivyo Mungu alivyowapangia. Hakuna uongo ulio mkubwa kuliko huu.
Kwa kumalizia niseme tu mpaka pale ambapo vipato vitaangaliwa upya na sheria za ajira kubadilishwa ili zimpe nguvu mfanyakazi tutaendelea kuwa taifa masikini mpaka mwisho wa dunia.
Mimi nataka u=kuelimika tu. Kulikuwa na haja gani ya kuandika ' hatutakuja' Kwa nini kichwa cha habari hiki kisingetosheleza " Kwa nini hatutaushinda umaskini " hiyo kuja imeongeza nini? Au unafasiri kutoka Ki....Haya?