Tatizo ni mifumo yetu ya kielimu na mapokeo yetu. Kubadilika toka umasikini kwenda kwenye utajiri ni fikra na si vitu tumilikivyo.
Nakubaliana nawe kwenye ufikirivu mdogo unaoongozwa na ubinafsi.
Upo sawa Mkuu, tunatakiwa tubadilike kifikra kwanza kwa kutumia elimu ndipo tubadilike physically.....tatizo elimu ya kutubadilisha kifikra ipo wapi? au ni hii ya kukaririsha isiyo fikirishi?

Ona jinsi wasomi wanavyo ililia serekali iwape ajira, ina maana hawana fikra za kuwakwamua kutoka kuwa masikini hadi kuwa matajiri bila ya kuajiriwa?
 
We unaweza ezeka Nyumba kabla ya msingi?

Wewe ndiye ueleweki kwani ni lazima uchangie pita tu nenda uwezo wako wa kuchambua mambo ni mdogo .

Waache wenye uwezo wachangie
 
We unaweza ezeka Nyumba kabla ya msingi?

Wewe ndiye ueleweki kwani ni lazima uchangie pita tu nenda uwezo wako wa kuchambua mambo ni mdogo .

Waache wenye uwezo wachangie
Isome South Korea
Isome China
Isome Singapore
Isome Malaysia
Nchi zote hizi zimekuwa kwa dimensions karibu zote sio kakitu kamoja.
Shida iko wapi kama una DASH 8 inayotua viwanja vingi tu, wakati vingine vinafanyiwa renovation.
Kuna aproach nyingi za kutatua matatizo sio lazima zote ziwe
Hierarchical .
 
Sawa
 
Haya sasa ni mawazo ya mwendokasi unaleta mifano ya nchi ambazo zimeendelea kabla ya kuzaliwa kwako
 

Jibu moja tu: Tanzania itaendelea kuwa poor kwa sababu ya low investment in people. Kila kiongozi anayekuja yeye pia ni product ya low investment kwa hiyo anakuwa na low capacity ya kufikiri. Ndiyo maana wanafikiri kuendelea ni vitu. Mwendeleze mtu ili ajiendeleze, hapo yatapatikana maendeleo. Sidhani kama kuna taifa duniani lenye mawazo finyu juu ya maendeleo kama sisi. Hebu nenda vijijini kwetu utaweza kufananisha na vijiji vya nchi gani nyingine duniani, jinsi ujinga, ukiwa, umaskini wa mawazo ulivyopamba. Labda South Sudan.
 

Nilikuwa naifuatilia hii mada kimya kimya ila umenifanya nicomment. I think this is one of the most important point. Kati ya mataifa yaliyopiga hatua one thing they did right ni kuinvest heavily in human resource.
Through this utapata intellectuals who will actually have an impact kwenye society, reasearch zitafanyika which are actually meaningful am sure 90% ya research zinazofanyika in tz at any given moment ni general ones, no ground breaking researchs being done.Taifa ili liweze kuadvance you need a highly specialized society/workforce na hiyo haipatikani without investing kwenye human resource.
 
Umejitahidi kuandika lakini mimi na mtazamo tofauti kama ifuatavyo;

Katika jamii zilizoendelea tangu wakiwa masikini kuliko sisi mfano Waingereza, Wayahudi na hata Wajapani hakujawahi kutokea mtu akawa na mawazo ya kushindwa kama wewe. Karibu wote hulitakia mafanikio Taifa na hushiriki katika kulipeleka mbele.

Watu huja na mawazo ya kuleta mabadiliko katika nyaja tofauti tofauti na kutekeleza lengo likiwa kuziokoa jamii zao.

Kauli unazozitoa kuhusu kushindwa kwa Taifa zinakurejea mwenyewe hivyo sitegemei kukukuta ukiwa umefanikiwa.

Mabadiliko huwa yanaanza na mtu mmoja. Hata wewe unaweza. Si lazima uwe mwana siasa. Ukifikiri kwa mtazamo chanya kwa lengo la kuiondoa nchi katika umasikini unaweza.

Siri ya mafanikio kama Taifa ni uzalendo wa wananchi husika.

Nawasilisha.
 
Yani mtachambua na kuchambua ila ukweli ni kwamba ktk nchi yoyote ile uchumi husababishwa na bidii za wananchi wenyewe ktk kujikwamua kutoka kwenye umasikini,ni lazima tuwe busy busy busy busy.viongozi ni kiunganishi cha kuhamasisha tu na kutulea semina za hapa na pale za kukuza uchumi kwa njia ya kuwajibika,yote kwa yote lazima tubadili mawazo kama wananchi,kufanya kazi kwa bidii na yoyote ile halali bila aibu wala uvivu
 


Mkuu "CHARMILTON", mfumo uliotengeneza elimu hii tuliyonayo umetengenezwa kiusahihi na kiuficho sana ili kila auonaye kwa mtazamo wa kawaida aone ni rafiki mwema lakn yeyote atakayeutafakari vema auone katika uhalisia wake. Naomba nikuulize haya:
1.Ni kwa nini watoto wadogo hupendana na hawakotayari kuona wenzao wakikosa lakini watu
watu wazima wanapiga dili hata zile za huduma za afya na kupelekea wenzao kufa?
2.Ni kwa nini watoto wadogo wanatamani kumiliki vitu vyao (mfano kila mtoto husifia kitu kizuri
kuwa chake) lakini watu wazima hutamani kufanya kazi za wengine na si kubuni zao ili wawe
huru?
3.Ni kwa nini mijadala yetu hata hapa jamii forums huonyesha ushabiki na si uhalisia?

4.Ni kwa nini viongozi wengi wa nyanja mbalimbali hawapo tayari kuwaambia ukweli
wanaowaongoza na badala yake huwaeleza yawapendezayo huku wakiwaumiza wale
waliowaamini kuwa wangewaongoza na badala yake wakawatawala?

5.Ni kwa nini viongozi wengi hupanga mipango ambayo pamoja na kuwekeza fedha nyingi
lakini huwa haifanikiwi?
6.Ni kwa nini tafiti nyingi hufanyika,na kazi kufanyika lakini mafanikio hayafikii?


YOOTE HAYO,NI MATOKEO YA MFUMO WA ELIMU TUNAOUPOKEA NA KUWA PROGRAMDE NAO
AMBAO MALENGO YAKE NI KUTUFANYA TUISHI KAMA TEGEMEZI.SI SISI TU BALI DUNIA
NZIMA. SINA TAFITI LAKINI NAAMINI SI ZAIDI YA ASILIMIA SABA YA WANA DUNIA WANA ELIMU SAHIHI YA KUJITEGEMEA NA HAWA NDIO WANACONTROL DUNIA KWA MAARIFA HAYO.
 
Asante nimekuelewa sana umeongea bila siasa na ndio lengo la Uzi huu.
 
 
Umasikini hautaondoka kwa kuwa tumeamua kuweka nchi rehani,rasilimali zote kwa wageni. Mada nzuri hii.

nchi imekuwa tegemezi kwa wawekezaji kwa kushindwa kuwa na mtaji, teknolojia za kisasa, mitambo, wataalam wenye uzoefu nk.

People are living in poverty if their income and resources (material, cultural and social) are so inadequate as to preclude them from having a standard of living which is regarded as acceptable by general society - VERY TRUE

tatizo ni usimamizi na utekelezaji wa shughuri za maendeleo...

tatizo kubwa ni ukosefu wa sera, tafiti nyingi hazikidhi mahitaji, watalaam kufanya shughuri tofauti na utaalam wao...
 
Duh....baada ya kusoma huu uzi nimejifunza kitu kimoja. Watu wawe na kumbukumbu ya maneno na mitizamo yao!

Ni hilo tuu!
 
Aman ya bwana iwe nanyi wapendwa

Husika na kichwa cha habar hapo juu

Nimekuwa mara nyingi nikisikia kutoka kwa wanasiasa wakiwambia wafuas wao kuwa umasikin walio nao umeletwa na ccm, mimi huwa sielewi ccm kasababisha vp watu wawe masikin,

Sizan kama ni sahihi kuaminisha watu kuwa umasikin wao umeletwa na ccm

Je wewe mwenzangu una ona ni sahihi kuwa umasikin wa taifa letu na watu wake umesababishwa na ccm

LONDON BABY

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…