Kwanza lazima niweke wazi kwamba Tanzania ni kati ya nchi 30 masikini zaidi ulimwenguni.
Kwanini Tanzania ni masikini?
Tanzania ni masikini kwa sababu ya mambo makuu mawili
1: Ability in thinking for change for both Leaders and citizens.
Uwezo wa Ku plan kwa viongozi wa kitanzania kwenye mambo ya maendeleo na kuzisimamia hizo plan zao uko chini mno muda mwingi wanautumia kuhubiri siasa pasipo kufanya kazi za kimaendeleo .
Kama ilivyo kwa binadamu tumepewa akili 100% lakini katika theory za kibinadamu unapoweza kutumia akili yako hata kwa 25% kabla uwe mweu unaweza kuwa umeshafanya jambo angalau hata moja la nchi au dunia kukukumbuka.
Hata mnaosoma Vitabu ukipitia "Thinking for change" cha John Maxwell utanielewa kidogo namaanisha nini.
"Taifa limeamua kumuacha mtu mmoja alisaidie kufikiria wakati nchi ina watu zaidi ya 50milion +
Anatutengenezea vicious cycle of poverty na sisi tunamwangalia tu.......tuendelee kuwa masikini wa vipato je tutakuwa na akili wakati tuna umasikini wa kipato na njaa ambayo inatokana na kuishi chini ya dollar moja?
Tunazunguka na kurudi pale pale clockwise and anticlockwise.
Kwa style hii tutaendelea kubadilisha marais hata aje Malaika kutoka mbinguni tutashindwa tu.
Sera ya Serikali haitakiwi kuwa Sera ya chama inatakiwa kuwa Sera ya taifa ndani ya Katiba ya nchi au Vitabu vya Sera.
Ndio maana unaona Sasa hivi tunacheza na aina zote za vicious cycle kwa sababu ya kutokua na Sera ya taifa ambayo tunaifuata kabla hata na baada ya ya uchaguzi.
A: Supply side of vicious cycle:
Low income - Low saving - low investment - low productivity- low income
Kama kipato ni kidogo - tutawezaje Ku save - tutawezaje kuwekeza - Tusipowekeza tutapataje product jibu ni hatutapata ndio maana tutaendelea na kuwa na kipato kidogo hivyo kuendelea kuwa masikini.
View attachment 409094
B : Demand side of vicious cycle:
Low income - low demand - low investment - low productivity then low income .
Kutoka kwenye kipato chetu kama ni kidogo ,hatutanunua vitu kuliko kipato chetu,tutawekeza kidogo, na kuzalisha kidogo tutarudi palepele kipato chetu kitakuwa kidogo.
View attachment 409095
C : Vicious cycle of market imperfections
View attachment 409097
Na mpaka hapo utagundua ni kwanini biashara imekuwa ngumu kufanyika Tanzania sasa hivi .
2: Poor utilization of natural Resources:
Hili ni tatizo la Africa karibu yote lakini kwa nchi yetu imekuwa to much.
Kwa shehena ya madini tuliyonayo tungeweza kuacha kufanya biashara nyingine kama nchi tukawa tukiuza madini tu na tukatajirika.
Kwa gesi tuliyonayo tungeweza kuuza gesi tu tukatulia hata kwa miaka 5 bila kufanya biashara yeyote na nchi ikaendelea..
Kwa Maji tulionayo tungeweza kuwekeza kwenye Kulimo, ufugaji na Uvuvi tusifanye kazi yeyote na tutaendelea.
Kwa utalii tulionao Milima,mabonde,mbuga za wanyama ,Fukwe za Bahari tungeweza kuwekeza kwenye utalii bila kufanya kitu kingine na tungetoboa maisha yangeenda .
Lazima tuamue kuchagua tunaanza na kipi ambacho tutakifanya kwa ufanisi wa hali ya juu kuliko kufanya juu juu kwa kulukia mambo....
Mfano ununuzi wa ndege ungekuja moja kwa moja na plan ya kupanua viwanja vya ndege vilivyopo karibu na maeneo ya utalii ili utalii ufanye kazi pamoja na Usafirishaji.
Nafikiri utakuwa umepata mwanga kwanini Tanzania ni masikini na kwa nini tutaendelea kuwa masikini miaka mingi ijayo kama hatutachukua hatua na kuwa specialization "
Kwani nchi zote zilizopiga hatua za kimaendeleo zime Specialize kwenye mambo Fulani.....
Israel ni nchi iliyopo kwenye jangwa lakini inaendeshwa na kilimo cha matunda.
Isome South Korea
Isome China
Isome Singapore
Isome Malaysia
Mungu ibariki Tanzania.