Hivyo vitu wanaovipa thamani ni nani? Sisi au wazungu?
Kwa vitu hivyo unatakiwa kusali waendelee kuwa matajiri ili wapate ziada ya kuja kuangalia nyumbu ambao si hitaji kubwa sana la binadamu, wakapande mlima ambao si lazima upande ndo uishi, wanunue madini ambayo si chakula kwamba watakufa wasipovaa Vito vya thamani.
NB: hivyo vyoote ulivyotaja vinahitaji wenzetu wawe na pesa za ziada kuvihitaji, Yaani wawe matajiri.
Hii nchi tuna jambo moja kubwa sana la thamani kuliko vyote na hatulioni, Ardhi yenye rutuba.
Tukifanya mapinduzi ya kilimo nchi zingine zikawa zinaleta meli kununua chakula hapa ambacho kimepakiwa vizuri kwenye vifungashio tutapata mafanikio makubwa.