Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Najua jf Kuna majibu yote naombeni nisaidieni hili suala langu kwanini tunakufa tukiwa masikini wakati tuna utajiri usio na kifani.
 
Kuna jamaa mmoja alikuwa anahojiwa somewhere na certain media abroad akaulizwa swali linalofanana na hili Kwanini nchi yako ni masikini; Jibu lake lilifanana na hili Hata mimi sielewi;
Back soon ngoja nijipange
 
Kuna jamaa mmoja alikuwa anahojiwa somewhere na certain media abroad akaulizwa swali linalofanana na hili Kwanini nchi yako ni masikini; Jibu lake lilifanana na hili Hata mimi sielewi;
Back soon ngoja nijipange
Misuli yake ya ubongo itakuwa ilikuwa na matatizo...jibu alikuwa nalo akaamua kuzuga
 
Misuli yake ya ubongo itakuwa ilikuwa na matatizo...jibu alikuwa nalo akaamua kuzuga
Nafikiri hilo jibu ambalo hakutaka kulitoa ndio lingekuwa muafaka kumjibu ndege JOHN, lakini lingine mtukufu anko kipindi anaingia kama kumbukumbu zangu ziko sawa kuna watu alikuwa anawasema kuwa wametufikisha hapa (kwenye huo umasikini), hadi tukawatengenezea mahakama yao ingawa aliomba tumuombee pengine aliwaogopa kwa namna moja au nyingine, sijui, lakini hii nchi sasa imekuwa dona kantri, sio masikini tena. Ndege jonh aache kuota.
After all nae pia ni shabiki kindaki ndaki wa mtukufu anko na pati kwa ujumla.
 
Mtazunguka sana lakini jibu ni moja tu na sababu ya jibu hilo pia ni moja tu
Jibu: Ni masikini kwa kuwa tumeamua wenyewe kuwa masikini.
Sababu: Miaka yote nchi inaongozwa kiholela hatuna misingi na sheria dhabiti za namna ya kuongoza nchi na ndo maana kila mtawala akija anakuwa na mambo yake aliyojisikia kufanya badala ya kuongozwa na sheria. Hapa namaanisha mimi na wapambe wangu kwanza, Tanzania baadae.
 
Umaskini wetu unatokana na ainaya uongozi na viongozi tulionao. Kuanzaia enzi za ukoloni wakoloni walikuja kutafuta mali na sio kutuletea maendeleo. Baada ya ukoloni viongozi wetu wamekosa weledi wa kuondoa umaskini bali wamekumbatia madaraka yaani kutawala hadi chama kinatumia slogan kama "kidumu chama" Kazi kubwa ya vyama ni kutawala heti kushika dola.

Kuondoa umaskini si kazi rahisi. Inahitaji umoja wa kitaifa na kumfanya kila mmoja wetu kushiriki siyo ya viongozi kujifanya wanatoa fadhila kwa wanowapenda. Tunahitaji bongo za waliojaliwa kuwa na akili kutumika kuleta maendeeleio sio ya sasa ya wanasiasa kujifanya wanajua kula kitu.

Mfumo wa upngozi wa nchi yetu unawapa viongozi mamlaka makubwa na kuwanyang'anya walio wengi na hivyo wananchi kuwaachia viongozi kazi ya kuleta maendeleo. Uhuru wa raia katika kushiriki kuleta maendeleo kwenye yao ni mdogo sana.
Mfano: Nguvu kubwa ya rais haiwezi kuruhusu raia kujiletea maendele - angalia rais anakuwa kama simba nyikani anateua kuanzia waziri mkuu hadi DAS. Na hawa wateule wanafanya kwa matakwa ya rais, anaweza kuwafukuza muda wowote wanakaaa kwa hofu.
Kwa leo ngoja niishie hapa maana...
 
Hii nchi haiwezi kuendelea chini ya mchwa ccm ,mafisadi ,wezi majambazi wakutupa waliojivika ngozi ya kijani kibichi wakijifanya wanasiasa kumbe wachumia tumbo hatari political entrepreneur .
 
Orodha hii ya utajiri wamewaamsha wazungu. ndo wanajua matumizimwanana wa hayo ya vitu ulotaja,

Hata ukipewa hizo dhahabu na almasi zenu richa ya kuzichimba, utazifanyia nini? Africa hii hakuna nchi inanunua.
 
TRUMP : Amewahi kusema " Ukiwachukua Waafrika wote ukawaweka bala la Ulaya na Ukawachukua wa Ulaya (Wazungu) ukawaweka Afrika , bado Waafirka wakiwa Ulaya wataomba msaada kutoka Afrika ."

PUTINI : Naye amewahi kusema Afrika itakapoanza kujitambua uwingi wa rasilimali zake na Viongozi wake kubadilika , ndipo itakapoanza kuendelea ".

Kwa mitazamo wa watu hao wakubwa wawili basi umepata majibu .

Binafsi naona umaskini wa Afrika unatoka na Waafrika wenyewe . Tatizo la uongozi mbaya Afrika linaeleweka na Waafrika wote , lakini halichukuliwi hatua .
 
Mimi nilishawahi kusema,Nchi yetu igawanywe kwenye Zones,kila zone iijitegemee kimapato na matumizi,,ita stimulate watu wa zone husika kuexplore opportunities zilizopo ndani ya hizo zones
 
Tuna mlima wa pili kwa urefu Duniani baada ya Mount Everest tuna ziwa lenye kina kirefu zaidi Duniani, tuna Ziwa kubwa zaidi Duniani lenye maji baridi yaani fresh water, ni nchi ya tatu Duniani japo baadhi ya data zilizofichwa zinaonyesha kuwa Tanzania ni nchi ya kwanza Duniani kwa kuwa na madini mengi na ndio maana Tanzanite inapatikana Tanzania peke yake sisi ni nchi tajiri tubadilishe fikra we are a donor country
 
Hivyo vitu wanaovipa thamani ni nani? Sisi au wazungu?
Kwa vitu hivyo unatakiwa kusali waendelee kuwa matajiri ili wapate ziada ya kuja kuangalia nyumbu ambao si hitaji kubwa sana la binadamu, wakapande mlima ambao si lazima upande ndo uishi, wanunue madini ambayo si chakula kwamba watakufa wasipovaa Vito vya thamani.

NB: hivyo vyoote ulivyotaja vinahitaji wenzetu wawe na pesa za ziada kuvihitaji, Yaani wawe matajiri.

Hii nchi tuna jambo moja kubwa sana la thamani kuliko vyote na hatulioni, Ardhi yenye rutuba.

Tukifanya mapinduzi ya kilimo nchi zingine zikawa zinaleta meli kununua chakula hapa ambacho kimepakiwa vizuri kwenye vifungashio tutapata mafanikio makubwa.
 
Unaweza ukawa na hivyo vitu vyote na unatamani sana uvitumie kufikia mafanikio lakini bado ukashindwa na kufail.. Kama umeshindwa kuifanya 50+ population kama manpower inayojielewa basi hivyo vyote vitakuwa mapambo na kila siku tutaendelea kugombana na wazungu..
 
Back
Top Bottom